Wadau salaam kwenu,
Kwa sasa bus la Sauli ndio linaweza kuwa bas linalokimbia sana barabarani (dhania) kwa Tanzania.
Nnafikir na Mfalme Zakaria wa Mwanza Musoma hatoshi, naona tunaanza taratibu kurudi kwa kina Leina tours, City boy na Kisbo kwa njia ya Kahama Dar, Buffalo na Ngorika enzi zile.
Swali langu vidhibiti mwendo Sauli hana au nini? Naamini ana gari mpya kabisa na ni Scania but speed alizonazo huwa zinaogopesha kiasi.
Mimi nimepanda mara chache tu, watu wa Moro wanaiita ndege ya chini, kama ambavyo wale wa Mwanza na Kahama tulizoea kuyaita mabasi ya Allys miaka ya 2007 na kuendelea maana Kahama - Dar saa 1 ulikuwa unaikuta Masbine pale Oilcom inapumua toka Kahama na Dar saa 2 tu mnaingia.
Sina chuki na kampuni hii lakina usalama wa abiria wenzangu ndio unanisukuma kutaka kujua.
Sent using Jamii Forums mobile app