Speed ya Prof. Tibaijuka yaanza kupata vikinza

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Mmiliki Palm Beach ampa Tibaijuka siku saba Thursday, 16 December 2010 20:51

Nora Damian
BADALA ya kuendelea na mkakati wake wa kupambana na watu waliojenga klwenye maeneo ya wazi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka atalazimika kutumia siku saba kutafakari barua ya mmiliki wa moja ya viwanja hivyo anayetaka aombwe radhi ndani ya muda huo kwa madai kuwa amechafuliwa.

Mmiliki huyo wa kiwanja hicho kilicho karibu na Hoteli ya Palm Beach jijini Dar es Salaam, Taher Muccadam pia ametishia kwenda mahakamani kudai fidia ya Sh2 bilioni iwapo Prof Tibaijuka, hatamuomba radhi.
Kiwanja hicho ni moja ya viwanja kadhaa ambavyo Prof Tibaijuka alisema ni vya serikali lakini wajanja wakavichukua kwa kutumia kisingizio cha viwanja vya wazi na hivyo kutaka virejeshwe serikalini.

Tibaijuka, ambaye aliambatana na katibu mkuu wa wizara wakati wa kukagua viwanja hivyo vilivyo ufukweni mwa Bahari ya Hindi, pia alitoa historia ya kila kiwanja hadi kilipovamiwa na kuwekwa majengo mapya.
Lakini Muccadam alifanya mkutano na waandishi wa habari jana na kuwaeleza kuwa maelezo ya Tibaijuka, ambaye alikuwa mkurugenzi wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UNHABITAT), alimvunjia heshima mbele ya jamii na sasa anataka aombwe radhi ndani ya siku saba.

Notisi hiyo ya siku saba iliyotolewa jana na wakili wa kampuni ya Decoram attoneys imeeleza kuwa Waziri Tibaijuka alimvunjia heshima mmiliki huyo kwa kutamka kuwa alitoa rushwa ili kukipata kiwanja hicho.
“Amenivunjia heshima ndani na nje ya nchi na mimi nikiwa kama mwanasheria, nimeumia sana. Naamini sheria ni msumeno na inaweza kutoa haki kwa mtu yeyote,” alisema Muccadam katika notisi yake hiyo.
Muccadam alieleza kuwa alipata kiwanja hicho kihalali kutokana na uamuzi wa Mahakama Kuu baada ya pande zote mbili kufika mahakamani hapo na kuafikiana.

“Hii inaonyesha dhahiri kwamba wizara imekula matapishi yake kwani ndiyo iliyotoa vibali vyote halali, vikiwemo vya kubadilisha ramani na kupima tangu mwaka 1975,” alisema Muccadam.
Katika notisi hiyo Muccadam ameeleza kuwa kama waziri huyo hataomba msamaha katika muda huo aliompa, atamfikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Kiwanja hicho namba 1006 kilicho Upanga jirani na Hoteli ya Palm Beach ni kati ya viwanja ambavyo Profesa Tibaijuka alisema kuwa ni vya wazi na kwamba haviruhusiwi kuwa makazi.
Kwa mujibu wa Muccadam, kiwanja hicho kilikuwa kinamilikiwa kwa hati namba 186164/25 iliyotolewa Januari Mosi mwaka 1975 kwa wamiliki wa kwanza ambao ni Shantaben Narottambahi Patel na Nilaben Girishumar Patel.
Alisema kiwanja hicho kilimilikishwa na Manispaa ya Ilala na miliki hiyo ilidumu kwa miaka 99 kabla yeye hajakinunua mwaka 2000.

Aliendelea kueleza kuwa mwaka 2000, kiwanja hicho kilifutwa kwa makosa na suala hilo likapelekwa Mahakama Kuu na kufunguliwa kesi namba 70/2004.
Baadaye Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ilipendekeza mgogoro huo umalizwe nje ya mahakama.
Aliendelea kueleza kuwa wizara na Manispaa ya Ilala vilishindwa kutekeleza makubaliano hayo hivyo ilimlazimu kufungua kesi nyingine Mahakama Kuu namba 107/2006.

"Niliendelea na malumbano hayo Mahakama Kuu kwa muda wote huo na hatimaye nilishinda kesi na kurudishiwa kiwanja hicho na kwamba, mahakama ilikubali nilipwe fidia ya dola 6 milioni za Kimarekani kama gharama za ujenzi huo," alisema Muccadam.

Muccadam alieleza kuwa alinunua kiwanja hicho ili ajenge jengo la ghorofa 22, lakini tangu wakati huo ameshindwa kuanza ujenzi kutokana na kuwepo kesi mbalimbali mahakamani.
 
Hii hoja ndiyo inamweka pabaya mmiliki huyu wa Palm Beach.......................kama kuna kesi zinazomzuia kujenga ghorofa tajwa sasa ana ubavu upi kudai kavunjiwa heshima................................................yabidi asubiri kesi zote za ummiliki wa eneo hilo zitakapokuwa zimekwisha ndipo atakuwa kwenye nafasi ya kudai fidia tajwa.............................

Mfano mathalani mahakama zikasema alipata miliki hiyo kinyume na sheria sasa hoja yake kuwa kavunjiwa heshima yatoka wapi?
 
*********. Nasikia yule Chavda aliyepewa masaa 24 kutoka nchini kwa sasa ni mtu maarufu sana kwa Kabila, ni ni mfadhili aliyetukuka kwa serikali na jumuia za kijamii kibao hata polisi wanajitolea kumlinda yeye na mali yake kwani pesa ipo. Kabadilisha jina kule, sijui Mwavda?
 
BADALA ya kuendelea na mkakati wake wa kupambana na watu waliojenga kwenye maeneo ya wazi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka atalazimika kutumia siku saba kutafakari barua ya mmiliki wa moja ya viwanja hivyo anayetaka aombwe radhi ndani ya muda huo kwa madai kuwa amechafuliwa.

Mmiliki huyo wa kiwanja hicho kilicho karibu na Hoteli ya Palm Beach jijini Dar es Salaam, Taher Muccadam pia ametishia kwenda mahakamani kudai fidia ya Sh2 bilioni iwapo Prof Tibaijuka, hatamuomba radhi.

Kiwanja hicho ni moja ya viwanja kadhaa ambavyo Prof Tibaijuka alisema ni vya serikali lakini wajanja wakavichukua kwa kutumia kisingizio cha viwanja vya wazi na hivyo kutaka virejeshwe serikalini.

Tibaijuka, ambaye aliambatana na katibu mkuu wa wizara wakati wa kukagua viwanja hivyo vilivyo ufukweni mwa Bahari ya Hindi, pia alitoa historia ya kila kiwanja hadi kilipovamiwa na kuwekwa majengo mapya.

Lakini Muccadam alifanya mkutano na waandishi wa habari jana na kuwaeleza kuwa maelezo ya Tibaijuka, ambaye alikuwa mkurugenzi wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UNHABITAT), alimvunjia heshima mbele ya jamii na sasa anataka aombwe radhi ndani ya siku saba.

Notisi hiyo ya siku saba iliyotolewa jana na wakili wa kampuni ya Decoram attoneys imeeleza kuwa Waziri Tibaijuka alimvunjia heshima mmiliki huyo kwa kutamka kuwa alitoa rushwa ili kukipata kiwanja hicho.

“Amenivunjia heshima ndani na nje ya nchi na mimi nikiwa kama mwanasheria, nimeumia sana. Naamini sheria ni msumeno na inaweza kutoa haki kwa mtu yeyote,” alisema Muccadam katika notisi yake hiyo.
Muccadam alieleza kuwa alipata kiwanja hicho kihalali kutokana na uamuzi wa Mahakama Kuu baada ya pande zote mbili kufika mahakamani hapo na kuafikiana.

“Hii inaonyesha dhahiri kwamba wizara imekula matapishi yake kwani ndiyo iliyotoa vibali vyote halali, vikiwemo vya kubadilisha ramani na kupima tangu mwaka 1975,” alisema Muccadam.

Katika notisi hiyo Muccadam ameeleza kuwa kama waziri huyo hataomba msamaha katika muda huo aliompa, atamfikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Kiwanja hicho namba 1006 kilicho Upanga jirani na Hoteli ya Palm Beach ni kati ya viwanja ambavyo Profesa Tibaijuka alisema kuwa ni vya wazi na kwamba haviruhusiwi kuwa makazi.

Kwa mujibu wa Muccadam, kiwanja hicho kilikuwa kinamilikiwa kwa hati namba 186164/25 iliyotolewa Januari Mosi mwaka 1975 kwa wamiliki wa kwanza ambao ni Shantaben Narottambahi Patel na Nilaben Girishumar Patel.

Alisema kiwanja hicho kilimilikishwa na Manispaa ya Ilala na miliki hiyo ilidumu kwa miaka 99 kabla yeye hajakinunua mwaka 2000.

Aliendelea kueleza kuwa mwaka 2000, kiwanja hicho kilifutwa kwa makosa na suala hilo likapelekwa Mahakama Kuu na kufunguliwa kesi namba 70/2004.

Baadaye Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ilipendekeza mgogoro huo umalizwe nje ya mahakama.

Aliendelea kueleza kuwa wizara na Manispaa ya Ilala vilishindwa kutekeleza makubaliano hayo hivyo ilimlazimu kufungua kesi nyingine Mahakama Kuu namba 107/2006.

"Niliendelea na malumbano hayo Mahakama Kuu kwa muda wote huo na hatimaye nilishinda kesi na kurudishiwa kiwanja hicho na kwamba, mahakama ilikubali nilipwe fidia ya dola 6 milioni za Kimarekani kama gharama za ujenzi huo," alisema Muccadam.

Muccadam alieleza kuwa alinunua kiwanja hicho ili ajenge jengo la ghorofa 22, lakini tangu wakati huo ameshindwa kuanza ujenzi kutokana na kuwepo kesi mbalimbali mahakamani.
 
Mahakama ndio muamuzi wa mwisho.

Kama alipewa umiliki kwa amri ya mahakama, hakuna anayeweza kubatilisha isipokuwa mahakahama ya juu zaidi
 
TIBAIJUKA MAGUFULI ALIONDOLEWA HUKO BAADA YA KUTAKA KUSIMAMIA KIDETE VIWANJA VYA WAKUBWA WA NCHI HIII ILI VIWANJA VIRUDI SERIKALINI,NASHAURI WASILIANA NA MAGUFULI KWANZA UPATE ABC YA wizara yako
 
Mama tiba kachemka no research no haki ya kuspeak sasa waziri mzima unajiongelesha bila data aibu,lazima aombe msamaha hana ujanja
 
Nilishasema kwenye ile thread ya mwanzo kwamba, Mama anahitaji kujipanga sana kabla hajaingia publick. She needs to do her homework first! People are not stupid. Asiongee ongee tu afikiri watu hawajui taratibu. Uozo uko huko wizarani... the problem is not the people. Asafishe na kusuka wizara vizuri. Akikurupuka kama alivyofanya ategemee mengi kwani naona amekuja publick too early!!
 
Mahakama ndio muamuzi wa mwisho.

Kama alipewa umiliki kwa amri ya mahakama, hakuna anayeweza kubatilisha isipokuwa mahakahama ya juu zaidi
Nani kakudanganya kaka mbele ya pesa?mama kuwa mwangalifu tu hawa watu hawafai hatakidogo,
 
Kama sheria ilifuatwa na kiwanja kutolewa 1975 je, sheria inasemaje kuhusu kejenga within 18 month ama sivyo umiliki unakuwa revoked, sasa techinically ni kiwanja batili na kutofanyika kwa hatua hizo ni ishara ya kuwepo rushwa
 
Sasa naanza kuamini kuwa mama hawezi hiyo Wizara. Kuwa habitat haina maana kuwa ni mtaalam . She is just a virgin politician who knows nothing about technical issues.

Pamoja na kwamba viwanja vimevamiwa itamwia vigumu sana kuvirudisha kisiasa namna hii. Hati miliki ni legal document issued under legal provisions. Kufuta hati ni swala la Rais . Utata unakuja kwamba hati zote hutolewa na Kamishna kwa niaba ya Rais . Kwa maana nyingine hati zote hutolewa na Rais . Kwa hiyo Waziri kuhoji uhalali wa hati ya kiwanja fulani unahoji mamlaka kuu . Ili Rais aweze kufuta hati kuna mambo ya msingi ya kuzingatiwa na ndio maana huyu Macadam alishinda kesi akarudshiwa kiwanja.

Suala la ardhi ni techical issue, na wataalam wa ardhi wanlijua sana ndio maana wanaweza kucheza nalo kiurahisi na halitakwisha. Imagine mfanyakazi wa ardhi analipwa fedha kidogo tu na unategemea awe msafi ndani ya huo mzunguko wa hela nyingi nje nje ni ndoto .Huyu mama ataendelea kuota ndoto hiyo kwa miaka 5 ijayo kama atakuwa na bahati ya kuwepo kwenye Wizara hii hii.
 
Mama tiba kachemka no research no haki ya kuspeak sasa waziri mzima unajiongelesha bila data aibu,lazima aombe msamaha hana ujanja
Ish! Mbona ktk maelezo ya huyo bw. anajichanganya. Kwa kama kweli ana hold the title free from any encumbrance, angeshaanza kujenga. Actishie nyau
 
Mmiliki Palm Beach ampa Tibaijuka siku saba Thursday, 16 December 2010 20:51

Nora Damian
"Niliendelea na malumbano hayo Mahakama Kuu kwa muda wote huo na hatimaye nilishinda kesi na kurudishiwa kiwanja hicho na kwamba, mahakama ilikubali nilipwe fidia ya dola 6 milioni za Kimarekani kama gharama za ujenzi huo," alisema Muccadam.

Duhhh, Inamaana jamaa kashavuna karibia Bilioni 10? Nani amelipa hizi hela?
 
Mama tiba kachemka no research no haki ya kuspeak sasa waziri mzima unajiongelesha bila data aibu,lazima aombe msamaha hana ujanja

Kachemka kwa lipi hapo! Makabwela wakichelewa kuendeleza kiwanja tu wananyang'anywa na huyu fisadi amekaa tangu mwaka 1975 bila kufanya chochote! Serikali ina haki ya kuamua kukirudisha kiwanja hicho! Acha naye aonje machungu tunayoyaonja wananchi wa kawaida. Kuna uwezekano wa rushwa kuwa ilitumika! Mama Tiba kaza uzi
 
tatizo huyu mama yeye kwake anadhani kazi ya uwaziri alopewa ni ku deal na open spaces tu...yaani sidhani kama ana vision ya kutosha
 
Sasa naanza kuamini kuwa mama hawezi hiyo Wizara. Kuwa habitat haina maana kuwa ni mtaalam . She is just a virgin politician who knows nothing about technical issues.

Pamoja na kwamba viwanja vimevamiwa itamwia vigumu sana kuvirudisha kisiasa namna hii. Hati miliki ni legal document issued under legal provisions. Kufuta hati ni swala la Rais . Utata unakuja kwamba hati zote hutolewa na Kamishna kwa niaba ya Rais . Kwa maana nyingine hati zote hutolewa na Rais . Kwa hiyo Waziri kuhoji uhalali wa hati ya kiwanja fulani unahoji mamlaka kuu . Ili Rais aweze kufuta hati kuna mambo ya msingi ya kuzingatiwa na ndio maana huyu Macadam alishinda kesi akarudshiwa kiwanja.

Suala la ardhi ni techical issue, na wataalam wa ardhi wanlijua sana ndio maana wanaweza kucheza nalo kiurahisi na halitakwisha. Imagine mfanyakazi wa ardhi analipwa fedha kidogo tu na unategemea awe msafi ndani ya huo mzunguko wa hela nyingi nje nje ni ndoto .Huyu mama ataendelea kuota ndoto hiyo kwa miaka 5 ijayo kama atakuwa na bahati ya kuwepo kwenye Wizara hii hii.

Mwacheni huyu mama afanye kazi yake! Ni wataalam hao hao ndo alikuwa nao siku anakagua viwanja Dar yaani mpaka Katibu Mkuu ambaye ndo Mtaalam aliyebobea katika maswala hayo. Hivyo sifikiri kama huyu mama anafanyakazi kisiasa, naamini anaweza kufanya makubwa katika wizara hiyo. Kwanza mama anza na huyo huyo fisadi! Rais pia hawezi kufuta hati miliki bila kushauriana na Wizara, kwa hiyo mapendekezo yote yanatoka Wizarani yeye ni kuidhiisha tu! MAMA SONGA MBELE
 
Kachemka kwa lipi hapo! Makabwela wakichelewa kuendeleza kiwanja tu wananyang'anywa na huyu fisadi amekaa tangu mwaka 1975 bila kufanya chochote! Serikali ina haki ya kuamua kukirudisha kiwanja hicho! Acha naye aonje machungu tunayoyaonja wananchi wa kawaida. Kuna uwezekano wa rushwa kuwa ilitumika! Mama Tiba kaza uzi

umedandia tiren kwa mbele hujaelewa somo,soma hiyo habari vizuri
 
Mimi sijaelewa vizuri maelezo ya Muccadam! kuna mahali amesema kuwa kiwanja hicho kilibinafishwa kwa miaka 99! sasa imekuwaje kiwe mikoni mwake au miaka hiyo 99 imeshakwisha au alikipata ndani ya huo huo mlolongo wa miaka hiyo 99?!

Naomba kueleweshwa vizuri hapo.
 
Hivi hii namba saba ina nini kila mtu namba saba

mrema namba saba zina nini hiz na we tibajuika wape 3 warejeshe hati zao walizopata kwa kuhonga huko manispaa
 
Back
Top Bottom