Speech za Viongozi wa TZ

Kishazi

JF-Expert Member
Nov 14, 2007
539
259
Kumekuwa na tabia ya viongozi wetu kutoa speech za kiswahili panapokuwa na mgeni toka nchi au taasisi za kimataifa kama IMF, UN, World Bank bila ya hata kuwepo kwa vifaa vya kutafsiri au wakalimani. Natambua kuwa viongozi wetu wanajaribu kuonyesha umuhimu wa lugha ya taifa ila wanasahau kuwa wageni wetu pia wanapenda kuelewa speech wanazoongea. Sidhani kama JK au kiongozi mwingine wa serikali, atafurahi akienda China, akasikia wanaongea Kichina tupu kwenye speech ya kumkaribisha, bila vifaa vya kutafsiri au mkalimani.

1. Mama Kikwete alikuwa alitoa speech ya kumkaribisha Mama Laura Bush (first lady wa US), kwa kiswahili, bila mkalimani wala kifaa chochote cha kunyambua anayoongea. Mama wa watu, akabakia kujichekesha, bila kujua anatukanwa au la.

2. Said Mwema jana alikuwa anatoa speech ya kumshukuru Mwakilishi wa UNHCR kwa kiswahili, the same bila mkalimani wa kifaa chochote.

Kifupi ni kuwa, hata kama wapambe / wenyeji wa wageni hawa watamtafsiria baada ya speech, sidhani kama itakuwa ina-make any sense as muda muhimu wa kuilewa speech, ni wakati inatolewa. Wenzio wanacheka, nawe unacheka, wenzio wanahuzunika, nawe unacheka, la sivyo hukawii kubehave differently.

To me, naona haijatulia, labda wadau nipate maoni yenu.

Maoni Pllllzzzzzzzzzzzzzzzz...!!
 
Nina mashaka na uzalendo wako!
Kiongozi anapokuwa anazungumza/anawakilisha taifa katika mazungumzo yoyote, anapaswa aongee lugha ambayo wananchi wake wanaifahamu (Kiswahili). Hapa kinachotakiwa ni kuwepo mtafsiri rasmi mweledi kuwezesha mgeni kuelewa kinachozungumzwa kupitia lugha anayoiweza. Nchi zote zenye kufuata mfumo bayana wa utawala bora wanafanya hivyo. Kitendo cha kiongozi kuongea lugha za kigeni wakati wa kuongea na wageni wa taifa ni kufanya kzi ya ukarani (kutafsiri). Kazi ya kutafsiri lugha ni kazi ya ukarani, haipaswi kuwa kazi ya kiongozi anayewakilisha taifa.
Kinachokosekana kwa hap Tanzania ni kutokuwepo kwa sera rasmi ya kuelekeza na kuratibu suala hili.
Ni aibu kiongozi kuongea lugha za kigeni katika shughuli rasmi za serikali. Sharti wananchi wafahamu anazungumza nini!
karagabaho!
 
Ndugu Sophist; kuhusu Uzalendo, mimi ni mzalendo ndio maana sijapinga hawa viongozi kuongea kiswahili. Pia ndio maana nilikuwa mmoja wa waliokerwa na swala la JK kutoa speech ya kumkaribisha Kibaki in English. Swala linalonikera hapa ni kuongea kiswahili mbele ya kiongozi mfano wa Marekani, bila ya kuwepo kwa mkalimani / vifaa ya kutafsiri.

Wewe unamkaribisha mgeni nyumbani kwenu Mbeya, mgeni mwenyewe ni mpare, then unatumia lugha ya Kinyakyusa kumkaribisha na kumshukuru kwa kuja. Obviously atabaki akikushangaa. Ila kama utamwekea mnyakyusa mmoja akawa anamtafsiria kwa pembeni, hiyo kwa kweli itakuwa imetulia, as utakuwa unakipandisha chati kinyakyusa but bila kukwaza unaowatangazia kinyakyusa.

The issue here ni translation, translation, bin kutafsiri. Wazee wa logistics/itifaki wanalala, viongozi husika nao wanalala, wapambe nao wanasinzia kabisa.
 
Back
Top Bottom