Speech ya Mkurugenzi wa kampuni ya Mawasiliano kwa Vijana

Zee la shamba

Member
Oct 17, 2007
55
3
Mkurugenzi wa kampuni moja kubwa ya MAWASILIANO alikaribishwa kutoa
speech katika tamasha moja la vijana lililokuwa limeandaliwa kuhusu
kujiepusha na vitendo vyenye kuweza kusababisha MARADHI ya KISASA.
Speech ya mkurugenzi huyu ilinukuliwa kama ifuatavyo:


"Hali ni ngumu sana vijana kwa sababu kila mmoja anataka kuonja uzuri wa
maisha ya kisasa. MTANDAO wa ugonjwa huu ni mkubwa, mimi nashauri muwe
makini, Jitahidini sana kukaa bila KUPIGA.


Ni muhimu SIMU zenu mzitunze sana na wala si KUPIGA PIGA kwani hii
GHARAMA yake ni KUBWA. Kama shida ya kupiga itakuwa kubwa, basi hakikisha
simu yako iko kwenye KIPOCHI, na hivi vinapatikana kwa wingi na gharama
yake si kubwa.Hii inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata madhara
yanayoweza kupatikana kutokana na MIONZI iliyoko katika simu hizi za
kisasa.


Ni mwiko kabisa kupiga VODA kwa VODA, CELTEL kwa CELTEL,TIGO kwa TIGO,
hata
TTCL kwa TTCL kwani hii ina hatari kubwa mno.


Watu wengi simu zenu zina fanya kazi vizuri tu, na mna hamu angalau ya
KUBEEP TU, lakini hii nayo ni HATARI ZAIDI ,kwani mwenzako akionyesha
UTASHI
wa
KUPOKEA ni rahisi sana kwako kuamua KUPIGA KABISA.


Msifikiri mkikaa bila kupiga muda mrefu, eti simu zenu zitamaliza CHARGE,
hii SI KWELI. Hakikisha tu kwamba SIMCARD yako iko katika hali nzuri,hii
ndio
ina KUMBUKUMBU zote na ndio inaongoza MAWASILIANO yote.


Simu ni simu tu, na madhumuni yake yanafanana.
Usidanganyike na simu kuwa eti ina KAMERA au eti DOUBLE SCREEN.....No..!!
Hizo ni
MBWEMBWE tu. Kuna simu nyingi sana FEKI siku hizi zinauzwa zimevishwa
COVER JIPYA,usidanganyike....!!


Ukiona maisha bila kupiga hayawezekani, basi KWA MSAADA WA MUNGU tafuta
sehemu INAYOAMINIKA na NA YA KUDUMU,
uwe unapiga hapo tu, hii inasaidia sana, kwani simu ukitumia peeke yako
INADUMU zaidi kuliko ile yenye SUBSCRIBERS WENGI....
ASANTENI SANA KWA KUNIELEWA, NAWATAKIA MAISHA MEMA YA KUMTEGEMEA MUNGU
KATIKA KUZITUNZA NA KUZIHIFADHI SIMU ZENU."
 
Back
Top Bottom