Mr Tyang
JF-Expert Member
- Sep 30, 2018
- 1,728
- 6,803
Origachi mmoja wa kirusi aishie UK, aliiambia UK baada ya kushikilia mali zake kuwa "ni ujinga pekee kufikiri kuwa maorigachi wa kirusi wanaweza kuzuia mikakati ya serikali ya Russia anaefikiria hivo atakuwa haijui vizuri Russia na namna inavyoendeshwa"Putin sio Urusi baba,
Putin atakuja kufa lkn Urusi Itabaki palepale.
Kulikua na wababe Urusi Putin ni Cha mtoto.
Kilichopo Urusi ni kuwa hawataki upumbavu.
Kulikua Kuna Marais wa Urusi hawasemi mara mbili.
Kama wangekuwepo Leo hii Ukraine Ingekua Jimbo la Urusi.
Nakupa simulizi moja ndogo TU ya unyama wa hao Marais wa Urusi waliopita.
*Magaidi wa kiarabu waliwateka maafisa wa Ubalozi wa Urusi huko moja ya nchi za arabuni.
Magaidi wakaanza kutoa masharti na madai Yao yasikilizwe la sivyo watawaua mateka.
Majasusi wa KGB wakafanya ujasusi wao, wakawajua watekaji wote.
Baada ya kuwajua magaidi nao KGB wakaenda kuwakamata au kuwateka ndugu wa magaidi hao.
Kisha wakawaambia watekaji kuwa,ndugu zenu tunao hapa,tunataka muwaachie hao Russian mliowateka,msipo waachia tutawaua ndugu zenu.
Kumbuka katika hao ndugu wa magaidi kulikua Kuna baba,kaka wadogo na ndugu wengine.
Magaidi wakazikaza shingo zao,wakakataa kuwaacha mateka.
KGB wakaanza kazi,wakaua ndugu mmoja, magaidi walipojifanya jeuri KGB wakaua ndugu mwingine.
Magaidi wakao Ohooo! haya majamaa hayatanii haya,wakawaachia mateka wote bila kuua hata mmoja.
Chezea KGB wewe?.
Usipoelewa ntakupa kisa kingine jinsi Marais wa zamani wa Urusi walikua vichwa ngumu Putin Mtakatifu.
Mgogoro wa makombora ya Urusi nchini Cuba.
Wanajeshi wa Urusi waliokuwepo Cuba na zana za nyukilia walipewa Ruhusa kabisa na Serikali ya Urusi kuweza kuyatumia makombora hayo ya nyukilia kama wataona Kuna hatari yoyote dhidi Yao na kisiwa Cha Cuba,bila kusubiri amri kutoka Kwa wakubwa zao mjini Moscow nchini Urusi.
"Hii ni Hali ya hatari sana"
Marekani kwa kujaribu kupeleleza kuhusu silaha hizo za nyukilia za Urusi ilituma mara mbili kwa nyakati tofauti ndege za upelelezi kama sijakosea ni U2.
Amini nakuambia wanajeshi wa Urusi waliokua Cuba walizipiga ndege hizo na kupoteza marubani kabisa.
Hakuna kitu USA walifanya,waliishia kupiga kimya TU na baadae kuomba mazungumzo yafanyike juu ya mgogoro huo.
Mgogoro ulikua mkali sana,ilibaki kidogo tu new York na Washington zipigwe kwa makombora ya nyukilia.
Unajua matokeo yake?
Matokeo yake ni USA ilikubali kutoa silaha zake za nyukilia Uturuki ndio Urusi nae akatoa silaha zake za nyuklia cuba.
Akifa Putin Leo, watakuja Marais watata sana Urusi, Putin Mtakatifu.
Na ongeza na kauli ya Lavrov Juzi alisema "anaezani kuwa urusi inaweza ikashindwa katika uwanja wa mapambano Ukraine huyo atakuwa na elimu duni na haijui urusi nini na historia yake"
Kwakweli ukifuatilia historia ya viongozi wa Russia tangu ikiwa kwenye Soviet union mpaka leo, basi utaona Putin ndo mpole na mtakatifu kuliko watangulizi wake.
Tujaribu tu kujiuliza hivi Rais angekuwa Dmitry Medvedev halafu jenerali wa majeshi ni Ramzan Akhmadovich Kadyrov (The great Chechnya warrior) Ukraine ingekuwa bado ni nchi kweli?
PUTIN IS A LEADER AND FATHER FOR EX-SOVIET COUNTRIES AS WELL AS WHOLE WORLD.