triga

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
502
1,000
Finland na Sweden zitajiunga na NATO tena mapema Zaid...

Erdogan emekataa kwa sababu zake binafsi
Edorgan yupo Istanbul anasema hawatajiunga na yeye ana kura ya veto kuzuia hilo

Wewe hapa msambichaka unasema watajiunga na kura yako ya veto inakupa kiburi si ndio?

Hii vita ya Omary na Edorgan huko NATO inavutia.
 

Bwana Utam

JF-Expert Member
Feb 15, 2016
8,815
2,000
Wewe jamaa ni mwelewa lakini unataka kuleta ubishi wa kishabiki, ifike muda uoneshe angalau curiosity sio ku generalize. Mkiwa front mnaweza kupewa order mbovu ikagharimu maisha ya hata ya battalion nzima. Kwenye hiyo ambush aliopigwa Russia kapoteza askari wengi, lakini wanaweza wasifike buku. Kilichowakuta wakuta russia kinaweza kilikuta jeshi lolote ikitegemea na uwezo wa adui yako.
Sasa wewe na biibiisiii nani wakuaminiwa zaidi MKUU
maana biibiisii mmetangaza majeshi 1000 mmewakata vichwa
Ila hongera zenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mtoto wa nzi

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
6,829
2,000
Wapendwa, tupunguze ushabiki kidogo. Habari za siku hizi ni hivi:
Kharkiv Warusi wanarudishwa nyuma, kuna dalili kwamba wanakusanya vikosi vipya upande mwingine wa mpakani ili wajaribu kurudi.
Kwa upande mwingine katika maeneo ya Donetsk wanasogea mbele polepole sana; bado wana mizinga mingi, wanasagasaga kijiji baada ya kijiji (hakuna dalili kwamba wanajaribu kutolenga watu raia), halafu wanasogea mbele, labda kilomita 1-2 kwa siku.
Wana matatizo kuvuka mito, hapo battle group moja iliangamizwa kabisa.
Ukraine ikifaulu kupeleka mizinga mipya kutoka Marekani hapa, hali inaweza kubadilika, kwa sababu M777 inapiga mbali kuliko mizinga ya kirusi, tena inakuja na grenedi za GPS tele. Vivyo hivyo kama ile Panzerhaubitze 2000 kutoka Ujerumani / Uholanzi inafika, hata kama si mizinga mingi.
Tuone.
We jamaa unawapinga sana wenzako PRONATOAMERICA ..... Tunachowaaambia wanakataaa unakuja kuwapapasa na kuwachua vizuriiii kuwa hali halisi ikoje.......
 

Cash Money Forever

JF-Expert Member
Mar 16, 2019
271
1,000
Hii vita itamshinda Urusi, wapambe wamekuwa wengi sana. Tuachane na hiyo operation ya kijeshi Ukraine.

Turudi zetu Moscow, kwa fundisho tuliompa Ukraine mpaka sasa sidhani kama atajaribu tena kujiunga NATO.
 

thuwainize

Senior Member
Jan 29, 2022
175
500
Kitakacho fanyika Ukraine ni ile wanasema ukiwa unampiga paka ndani ya nyumba acha upenyo kidogo mlangoni ili paka apite hapo kukimbia. Maana ukifunga milango yote huku ukimtwanga na rungu huyo paka anaweza kukujeruhi. Wataalam wa mambo ya migogoro ya kimataifa pekee ndio wanao weza kuelewa hili nililo andika.

Maadam Magharibi wameingia bila kificho kumsaidia Ukraine kamwe Russia hawezi kushinda vita hii, Putin mwenyewe anajua. Kitakacho fanyika ni kutafuta namna Russia atoke Ukraine bila kudharilika sana, vinginevyo Putin hatakubali.
Putin hana muda mrefu wa kuendelea kuwa madarakani.....soon kuna mabadiliko ya utawala yatatokea na Kiongozi mpya atakayeingia hawezi kuwa na siasa kali kama za Putin maana russia ipo hoi kwa sasa ili kuwaplease wananchi kiongozi atakayeingia atajikuta hana budi kukubaliana na masharti kadhaa ya jumuia za kimataifa. Kwa kifupi upo sahihi Putin hii vita hashindi hata afanyeje. Kadiri muda unavyokwenda ndivyo russia anazidi kupoteza Kyiev alishafurushwa, leo Kharkiv kafurushwa jana platoon yake nzima wamekufa kifo kibaya yaan ni majanga baada ya majanga. Yaan muda unavyozidi kwenda hakuna advancement yoyote ya maana Putin anayofanikiwa na ni kama vile kategewa kadiri muda unavyoenda ndivyo anavyozidi kupewa kichapo taratiibu na anajikuta hana namna lazima arudi nyuma.
 

passioner255

JF-Expert Member
Apr 22, 2019
1,918
2,000
Putin hana muda mrefu wa kuendelea kuwa madarakani.....soon kuna mabadiliko ya utawala yatatokea na Kiongozi mpya atakayeingia hawezi kuwa na siasa kali kama za Putin maana russia ipo hoi kwa sasa ili kuwaplease wananchi kiongozi atakayeingia atajikuta hana budi kukubaliana na masharti kadhaa ya jumuia za kimataifa. Kwa kifupi upo sahihi Putin hii vita hashindi hata afanyeje
Nonsense
 

Bwana Utam

JF-Expert Member
Feb 15, 2016
8,815
2,000
Siku ya 79 ya Oparesheni ya Urusi nchini Ukraine, na ni siku ya 20 ya oparesheni phase 2. Tarehe 13/5/2022.

Kwa siku tatu juzi, jana na leo, Urusi imeongeza nguvu kubwa katika mashambulizi yake Ukraine ambapo imepanua mara nne zaidi ya eneo ililokusudia kulilinda baada ya kujitangazia uhuru wa maeneo hayo katika majimbo ya Ukraine ya Luhansk na Donetsk. Upanuzi huo umefanya Ukraine kumegwa katikati ya nchi hiyo kutoka Kaskazini mji wa Kharkov hadi kusini mji wa Mykolaiv ikimega kwakukatisha katikati ya nchi hiyo hadi mji wa Zapolozhye.

Urusi imetumia mwanya Wakati dunia ya Magharibi iko kwenye mtanziko mkubwa kwa mauaji ya Israel dhidi ya waislamu waislsmu wa Palestine wenye meimamo mkali kule Al Aqsa na vurugu za mauaji yw mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Aljazeera Bi Shereen Abu Akleh. Hadi sasa Marekani, NATO, na nchi zingine binafsi kama Uingereza nk imeziba masikio na midomo hazitoi kauli yoyote kulaani au kuunga mkono mauaji haya ya Israel dhidi ya raia wa Palestine tofauti kabisa na walivyo mstari wa mbele kwa mgongo wa Ukraine.

Vvyombo vya habari Moscow hasa vile vinavyosimamiwa na jeshi la Urusi kama vile RUDENKO na vingine, Vimerejea Hotuba ya Rais Putin aliyoitoa 01.07.2016 akionya Finland isikiuke miiko na kujiunga NATO.
Rais wa Urusi Vladimir Putin ni kama alitabiri nyuma mnamo 2016 nini kitatokea ikiwa Finland itajiunga na NATO.

Kulingana na hutiba ya Rais Putin, kwa kujiunga kwa Finland katika Umoja wa Kujihami NATO, wanajeshi wa Ufini hawatakuwa huru tena. Watakuwa sehemu ya miundombinu ya kijeshi ya NATO, ambayo itaonekana ghafla kwenye mipaka ya Shirikisho la Urusi.

Putin: "NATO itafurahi kupigana na Urusi hadi mwanajeshi wa mwisho wa Kifini, Fikiria Finland inajiunga na NATO. Unafikiri tutaendelea kufanya hivi: askari wetu wameondoka hadi kilomita 1,500, kwa hiyo watabakia huko, au vipi? Tunathamini hali ya kutofungamana ya Finland na kuiheshimu, lakini sio kwetu sisi kutatua suala hili.

Ili kufafanua taarifa ya mmoja wa marafiki zangu wa Kifini, naweza kusema kwamba shirika la NATO labda lingefurahi kupigana na Urusi hadi askari wa mwisho wa Kifini. Unaihitaji?".

Hotuba hii aliitoa miaka sita iliyopita, Leo Finland inatumia mwanya wa mgogoro wa Ukraine inaamua kujiunga na NATO kwa shinikizo la Uingereza na Marekani. Nini jibu la Moscow? Tuendelee kusonga mbele.

Rais wa zamani wa Urusi na Makamu Mwenyekiti wa sasa wa Baraza la Usalama la Urusi Dmitry Medvedev ameonya Marekani na Ulaya kwa misaada wanayoendelea kuitoa kwa Ukraine na kwamba kitendo hicho ni kutangaza vita rasmi na Moscow. Amesema Moscow iko tayari kujibu iwe mchana au usiku lakini haitakaa kimya usalama wake ukitishiwa.

Mkuu wa Usafirishaji gas ya Urusi nchini Ukraine bwana Sergiy Makogon amesema wamefunga valvu mbili kati ya zile zinazosafirisha gas kwenda Ulaya. Hatua hiyo ni sehemu ya vikwazo vya Ulaya na Marekani kwa Urusi. Sergiy Makogon amesema Ukraine itaendelea kuchukua hatua zaidi kadiri muda unavyokwenda. Mataifa ya Ulaya yote yanapata gas ya Urusi kupitia mabomba yaliyotandazwa toka Urusi kupitia Ukraine hadi Ujerumani.

Ikulu ya Kremlin imesema mji wa Kherson utaunganishwa na Crimea kuwa eneo la Urusi au utaunganishwa kuwa eneo la Donetsk kulingana na matakwa ya Wananchi wa Kherson. Mji huo uko chini ya Majeshi ya Urusi tangu ulipotekwa ambapo sasa mji huo unapata huduma zote za kiserikali kijamii nk kutoka Moscow.

Msemaji wa Ikulu ya White House Bwana Ned Price amesema nchi yake haifadhili harakati za Taiwan kujitenga na China, Hatua hiyo imekuja baada ya China kuionya Marekani iache kuchochea uasi wa Taiwa kwa China. Wiki juzi China ilipewa taarifa za kijasusi kutoka shirika la Ujasusi la Urusi la FSB kwamba kuna kikao cha maafisa wa juu wa Uingereza na Marekani kimekalika kwamadhimuni ya kuinjinia uasi wa Taiwan kwa China, Taarifa hizo zilikuwa sahihi kwani Idara ya Usalama China ya Ministry of State Security [MSS] pia ilikuwa na taarifa hizo japo haikujua muda na mahali kikao hicho kitakapofanyika, hivyo Taarifa ya Moscow ilikuwa mwarobaini kwa China.

Makomandoo 405 wa Chechnia wamepelekwa uwanja wa vita huko Luhansk kuongeza nguvu, Chechnia inapigana begakwabega na Urusi kuhakikisha Jamhuri za Donetsk na Luhansk zinakuwa Huru, ambapo tayari Donetsk imeshakombolewa na iko chini ya majeshi ya Jamhuri ya Donetsk, huku Luhansk inaendelea kurindima makombora kila upande kuanzia Kharkiv, Izium, hadi mjini Luhansk.

Baada ya Finland na Sweden kuwasilisha rasmi maombi ya kujiunga na NATO, Kampuni ya INTER RAO ya Urusi ambayo ndio msambaji wa umeme nchini Finland imesema itakata huduma ya umeme kesho 14 May 2022. Hatua hiyo inafuatia Ufini kukiuka makubaliano ya kutofungamana na upande wowote.

Vatican imebadili maneno iliyoyatoa juzi ambapo ililaani upelekaji wa silaha Ukraine nw kusema ni kuchochea vita, ambapo leo Kadinali Yeptero Parolin, Katibu wa Serikali na Mjumbe wa Pili wa Vatikani, amekaririwa akisema, Kutuma silaha kwa Ukraine ni halali kimaadili, Akirejelea mafundisho ya Kanisa Katoliki, Kadinali Yeptero Parolin, Katibu wa serikali na mjumbe wa pili wa Vatikani, amesema kwamba kukidhi mahitaji ya silaha za Ukraine ili kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi ni "halali ya kimaadili chini ya masharti fulani."

Vikosi vya Urusi vimeendelea na Opareshe leo kwa kushambulia kwa nguvu kubwa maeneo ya Khakyiv, huku vikosi vinavyoendelea kushika doria kule Azovstal Steel vikiendelea kushusha mvua ya makombora na kuvuka uzio mkubwa wa kiwanda hicho tayari kuelekea ndani. Nako katika mji wa Avdiivka usiku mzima wa leo kumekumbwa na mashambulizi makali ambapo vikosi vya Urusi vilikumbana na kizuizi cha makuruta wa Ukraine, na hatimaye Majeshi ya urusi yametwaa mji huo baada ya kuvishinda vikosi vya makuruta toka Ukraine.

Kwa mara ya kwanza, Waziri wa Ulinzi wa Urusi Jenerali Shoigu amezungumza na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin katika mazungumzo ya kwanza tangu operesheni ya Urusi nchini Ukraine kuanza.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani ya Pentagon imesema upande wa Marekani ulisisitiza umuhimu wa kuweka mawasiliano wazi, na kuhimiza usitishaji wa mapigano uanzishwe. Huku upande wa Moscow ukisisitiza Marekani iache kuingilia Oparesheni ya Moscow nchini Ukraine kwakufadhili siala na Ujasusi.

Waziri wa Mashuri ya Kigeni wa Urusi Sergey Lavrov ameelezea mashaka yake juu ya ombi la Ukraine la kujiunga na EU - akisema kuwa Umoja huo unageuka kuwa mwigizaji pinzani na matamanio zaidi ya bara la Ulaya. Kimsingi Urusi itajenga ukuta wa kinchi baina yake na NATO eneo lolote penye mashaka ya kiuslama kama inavyofanya leo kuhakikisha inadhibiti kila mashaka juu yake.

Waandishi watatu wa Habari wa kituo cha runinga cha Rassia today tv, ripota wa habari Bwana Valentin Gorshenin na wapiga picha/video Vladimir Batalin na Viktor Miroshnikov wamejeruhiwa kwa riketi la Ukraine lilirushwa katika mji wa Dokuchaevsk huko Jamhuri ya watu wa Donetsk. Eneo hilo liko chini ya Urusi lakini mashambulizi ya rasharasha bado yako.

Kikosi cha Wadunguaji (Snipers) wa Urusi kutoka kikosi cha 22nd GRU Special Forces Brigade wamefanikiwa kuwadungua wadunguaji wa Ukraine waliokuwa wamejichimbia kwa muda mrefu katika eneo la Donbass, kikosi cha Urusi cha 22nd GRU Special Forces Brigade ni maalumu kwa udunguaji ambapo kimefanikiwa kusafisha maeneo mengi katika Oparesheni hii na kinasifika kwa shabaha za hali ya juu duniani.

Mizinga ya roketi ya Jeshi la Urusi imeangamiza eneo muhimu la kimbinu la Ukraine na vifaa vya Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine huko Donbass, mwelekeo wa Liman. Huko kwingineko jioni ya leo, madaraja matatu muhimu kwa uhamishaji wa vikosi vya Ukraine yalipuliwa katika mkoa wa Kharkiv, madaraja hayo ni karibu na makazi ya Stary Saltov, Pechenegi na Rubezhnoye.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan amesema Finland na Swideni ni nyumbani kwa magaidi, Na Kwamba Uturuki inapinga kwanguvu zote uanachama wa nchi hizo katika NATO. Na ikilazimu itapinga kijeshi. Tangu oparesheni ya Urusi nchini Ukraine mnamo 22 Februari 2022, maoni ya umma na vyama vya Finland na Uswidi vimeonyesha mwelekeo usio na hasi wa kujiunga na NATO, huku maafisa wa serikali ya Finland wakitangaza jana kuwa nia ya Finland ya kujiunga na muungano huo. Finland inatarajiwa kutangaza uamuzi wake kesho kutwa Jumapili.

Urusi imepuuza propaganda zinazofanywa na Shirika la Ujasusi la Uingereza MI6 kwamba leo Ukraine imeangamiza vifaru na askari wa Urusi zaidi ya 1,000 waolitaka kuvuka mto Siversky unaopakana na Donetsk na Luhansk. Kamanda wa vikosi vya Urusi nchini Ukraine Jenerali Alexander Dvornikov amesema propaganda hizo zimetolewa na Jasusi wa Uingereza anayeendesha kampuni la Ujasusi la Sibylline Ltd ambalo liko Ukraine likiendesha Ujasusi kwaajili yw Ukraine, na kusambazwa na wanamgambo wa Ukraine taarifa ambayo ni kinyume chake.

Yericco Nyerere View attachment 2223756
Hii kauli ya FSB kuhusu majeshi buku kuuliwa niyamuhimu sanaa
RTI achana na propaganda za hao wapuuzi wapuuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Bwana Utam

JF-Expert Member
Feb 15, 2016
8,815
2,000
Ukraine has spent more than $8 billion on military actions against Russia
Meanwhile Russia has a surplus of 40 billion EUR since January

In an interview with Reuters, Finance Minister of Ukraine Serhiy Marchenko said that Ukraine has already spent UAH 245.1 billion on waging war with Russia (this is about $8.3 billion).

According to Marchenko, the funds allocated for development went for everything: from the purchase and repair of weapons to emergency assistance to internally displaced persons. The government collected only 60% of the planned tax revenues for April, in May–June this figure may decrease to the level of 45-50%.

"Kiev needs foreign financial support, as Ukraine is forced to spend billions of dollars on extraordinary expenses. According to the estimates of the Ministry of Finance, $5 billion a month is needed to finance the state budget," the minister stressed.
Naeka kituo hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Adiosamigo

JF-Expert Member
Oct 2, 2013
2,963
2,000
Ila hii ambush waliyofanya Ukraine ni hatari,siku mbili zilizopita drone za Ukraine ziligundua uwepo wa hilo pantoon bridge la Urusi wakijiandaa kupitisha vifaa vya kivita Kama vifaru,magari ya mizinga,na vifaa vingine vya kijeshi jamaa wakaacha warusi wajae waanze kuvuka wakashambulia Kwa artillery karibu vifaa vyote vimeharibiwaBaada ya mashambuliziMagari takribani 73 pamoja na vifaru vimeharibiwa vibaya na artillery za Ukraine.

Kweli Marekani hakukosea alovyosema sasa NI mwendo wa kupigana mizinga tu,hizi Howitzer alizotuma US kule Ukraine zitawatesa Sana warusi

Vifaru 73 Yani wanapiga vifaru 6 wanakuambia 73
 

KIDUNUNDU

JF-Expert Member
Dec 3, 2012
572
1,000
Hii vita itamshinda Urusi, wapambe wamekuwa wengi sana. Tuachane na hiyo operation ya kijeshi Ukraine.

Turudi zetu Moscow, kwa fundisho tuliompa Ukraine mpaka sasa sidhani kama atajaribu tena kujiunga NATO.
Mrusi akikubali hili ujue akubali sera za marekani . Akubali kuwa kibarakq kama Japan na hataweza jiunga na NATO.
Halafu UN kuna issue wanapotezea kama uchunguzi wa Bioweapons utapotea itakuwa sio issue tena na AZOV watafanya watakayo ulaya mashariki. Kuna mambo mengi nyuma ya hii vita.
 

Tsh

JF-Expert Member
Aug 26, 2021
1,488
2,000
Rejea comment yako ya mwanzo uliyo ni quote.
Wewe kifupi weka orodha ya vita ambazo USA alishinda yeye kama yeye.

Hapa ni discussion ukiulizwa swali lijibu.
Tunataka kuonesha with evidences Russia vs USA
Huenda kuna mtu ameku quote ukachanganya na mm au huenda nimeku quote ukanielewa tofauti. Siwezi kubishana kati ya USA na Urusi nani mbabe ila ninapinga Urusi kuivamia Ukraine.

Hapa kinanchonifanya niingie humu ni mada hii,

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo.​


Kama unataka tubishane kwa hoja basi wewe simama katika kutetea uvamizi wa Ukraine na mm nisimame katika kupinga uvamizi wa Ukraine lakini sio tubishane nani mbabe kati ya USA na Russia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom