Urembo wa nywele, mitindo mbalimbali ya kusuka na kunyoa

Jamani. Mi mke wangu akisuka nywele zinakatika usoni. Akiweka wigi zinaisha usoni. Akiachia tu zinaanza kuota.

Afanyeje maana nataka aonekane mrembo
Kama aliziweka dawa mshauri akate aanze upya...na wewe sasa anaglia comment huko ujue atumie mafuta gani
 
Habari Mabibi na Mabwana!!! Natumai muwazima wa afya njema,.kwa ndugu zangu waislam mwenyezi Mungu azidi kuwapa wepesi mmalize salama funga yenu inshaallah..

Jamani warembo wenzangu na watanashati mm kwa sasa nimekuwa mpenzi wa nywele fupi,huwa natumia wave au dawa laini kulainisha nywele zangu na kuzipaka curl activator sio siri napendeza na kuvutia mnoo

Sasa tatizo linakuja nikiwa naweka dawa nywele zangu yaani dawa haikai hata dakika 10 kichwani yaani inauma sana na nikisema nivumilie vumilie naweza ungua so unakuta muda mwingine haishiki vile ninavyotaka,tofauti na wengine anaweza kukaa na dawa kichwani hadi lisaa....hivyo naombeni ushauri nitumie wave/dawa gani ili nisisikie Maumivu upesi au nifanye nn kabla kuepuka Maumivu na kuu gua??? Shukrani.

Mumu.
 
Usizidishe kiasi, weka kulingana na urefu na wingi wa nywele.

Dawa ikishika kwenye ngozi ndiyo matatizo yake hayo, kuwasha kulikopitiliza.

Hata hivyo, sina utaalamu wowote ila nimehisi tatizo lako ndilo hilo.
 
ukiwa unapaka jaribu kupaka kwa juu juu yaan wakat unaanza usianzie chin...weka juu juu then massage kwanza kabla ya kuzichana n hata ukichna usikandamize kitana/chanuo hadi kwenye ngozi kwani kuna uwezekano wa kuikwangua ngozi hivyo kuweza upenyaji wa dawa ndani ya ngozi na kukusababishia maumivu.....
 
Tafuta dawa itakayo endana na wewe mm wenyewe mwanzo nilikuwa naweka dark & lovely nikawa naungua kweli hata kbl sijamaliza kuwekaa, nikabalisha now naweka movit iko pouwa kbs naweza kuvumilia mda mrefuuu na nywele zangu nashukuru mungu mashaalah
 
Salam ndugu
Nna swali,ivi dread zikiwa nene na unataka kuzipunguza inawezekana? je nifanyaj dread zangu zimekuwa nene sana na nataka ziwe size ndogo
 
Naombeni msaada nilikua nataka curl hair lakini haya mafuta ya afrogel yamefanya nywele zinyanyuke na zimekua mbaya watabe naombeni maelekezo labda nimekosea matumizi
 
Curl hair ya Natural hair au relaxed hair??? na kama unaona mafuta flani hayajakukubali basi badilisha mbona kuna mafuta ya curl mengi tu mfano CANTU.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom