Special thread: Ujenzi, ushauri kuhusiana na nyumba, mafundi na makadirio

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,563
3,708
Mteja anaitaji elimu kwanza ya bidhaa au uduma kabla haja ihitaji.

Hapa ni maalumu kwa mafundi wote kutoa elimu,ushauri na mbinu za maswala mbalimbali ya ujenzi wa nyumba kuanzia msingi mpaka inakamilika.

Andika swali lolote kuhusu tatizo la nyumba yako utajibiwa na madau mbalimbali na kupewa ushauri.

Kama ni fundi umeme,kujenga,kuezeka na nk mafundi wote karibuni,weka picha ya kazi uliyofanya pomoja na melezo kidogo ya kuelimisha,mwenye kuitaji uduma yako mtawasiliana kwa ajili ya kufanya kazi.

images(7).jpg
IMG_20200620_071552_522.jpg
images(2).jpg
images(8).jpg
images(4).jpg
images(6).jpg
 
Makosa baadhi ya mafundi tiles huyafanya.

Tiles zinaweza kuzamia ndani na kuaribu kabisa ubora na kukupa hasara ya gharama wewe mwenye nyumba.

Sababu ya hili tatizo huwa sub floor(tandiko) isiyo imara na ubora kama vile vumbi,unashauliwa kabla ya kuweka tiles ni bora ukaweka msingi wa uimara kama kutanguliza zege ya kiwango kizuri pia gundi ya ya simenti iwe ni ya kuridhisha iliyojazia ujazo wa kuwekwa tiles na kuzingatia ubora,mara chache ubora wa tiles inaweza kuwa sababu lakini fundi nae anamchango wake katika hali hii.

Suluhisho wa tatizo,
Ikitokea hii hali kwenye jengo ni vyema kubadilisha palipo na hitilafu kwa kuzingatia ubora wa tiles zenyewe,mchanganyo wa simenti na utendaji kazi,tatizo likiwa kubwa bomoa tiles zote anza upya kwenye tandiko na aina mpya ya tiles.

Tafuta fundi bora kuepusha usumbufu wa gharama zisizo za lazima.
Buckled-Tiles-02-0307190001-768x576.jpg
images(14).jpg
FB_IMG_15926607041452733.jpg
 
ed66cc3e472ea7edd4d5e4db36958574.jpg
jinsi za kuondoa panya nyumbani kwako.

⏩Tafuta Paka.
⏩ziba mashimo na njia zote anazopitia kuingia ndani.
⏩usafi wa nyumba yako ni muhimu,kuna harufu zikiwepo ndani panya zinamvutia ni zakimazigira anajihisi ni nyumbani kutokana na harufu,toa na tupa kabisa mabaki ya chakula na takataka zingine kama za ujenzi mf. Gundi,rang na mbao nk nyumba iwe safi sana,panya sio msafi kwa hiyo hawezi kukaa na msafi.
⏩weka sumu na mitego ili kuwauwa zingatia usalama wa watoto unaoishi nao.
⏩andaa (Store) sehemu maalumu kwa ajili kuifadhi chakula na nafaka zingine chumba kiwe kimefungwa mda wote pasipo na ulazima kubaki wazi.
 
Rangi ya nyumba kuvimba na kubabuka au kuandika tu bila kuvimba haswa maeneo ya karibu na msingi shida ni nini na dawa yake ni nini?
 
Rangi ya nyumba kuvimba na kubabuka au kuandika tu bila kuvimba haswa maeneo ya karibu na msingi shida ni nini na dawa yake ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Je ukuta wako una fangasi? Tiba yake ni kugandua rangi yote na plaster na kupiga msasa ukuta mzima na kuanza upya kuchapia na kupaka rangi upya.
Chakuzingatia wakati wa kuchapia upya kuna simenti maalumu ya kuzuia fangasi kwenye ukuta.

Na njia nyingine kuzuia fangasi wakati wa kujenga msingi ukishamaliza unatandika kitu kama waterproof kati ya ukuta na msingi.
Mengine wasubiri watalaamu watakueleza
 
KUPAKA RANGI

Utangulizi
Mara nyingi watu hutafuta mafundi kwa ajili ya kupanga rangi nyumba zao ama sehumu za nyumba zao na kuta za ua. Hii ni sawa kabisa kwani mafundi wanauzoefu na ujuzi unaohitajika katika upakaji rangi.

Lakini upakaji rangi ni jambo linaloweza kufanywa na mtu yeyote kama atazingatia jinsi ya kupaka rangi na hatua zake. Makala hii itahusika na upakaji wa rangi ya maji.

Mahitaji
1. Rangi ya maji

2. Brashi mbili ama brashi moja na rola

3. Skrepa/kikwanguzi

4. Msasa

5. Ndoo tupu

6. Maji

7. Kipande cha godoro ama kipande cha kitambaa

8. Selotepu na magazeti.

MATAYARISHO
Ni muhumi matayarisho yafanywe siku moja kabla ya kupaka rangi ili kuwezesha ukuta kukauka vizuri kama kiziba nyufa kilitumika. Pia hii usaidia vumbi kutuama ama kuelekea nje kupitia madirisha kutokana na mzunguko wa hewa.

Hatua ya kwanza ni kuvitoa nje vitu vinavyohamishika vilivyomo ndani ya eneo husika. Ama unaweza..

Vitu vyote vinavyohamishika vilivyomo ndani ya eneo husika au la unaweza kuvikusanyia katikati ya chumba na kisha kuvifunika kwa kitambaa ama nailoni. Hii itasaidia kukupa nafasi na eneo tosha la kufanyia kazi na pia vitu vyako na hasa samani havitachafuliwa na rangi.

Kumbuka kama hutaviacha vitu hivi ndani na hautavifunika pia utalazimika kuvisafisha badae! Upotezaji wa muda na nguvu usio wa lazima! Kama unahitajika kupanga rangi dari(ceiling) ambalo lilikuwa na rangi, tumia msasa kulisugua taratibu kuondoa chembechembe zisozogandamana. Kama unalipaka rangi dari lako kwa mara ya kwanza basi hamna haja ya kulisugua kwa kutumia msasa.

Baada ya kupiga msasa dari lako sasa piga msasa kuta zako kuondoa chembechembe zote zisogandamana na uchafu ama madoa. Baada ya zoezi hili tazama vizuri kuta zako kubaini nyufa ama mashimo. Kama kuna nyufa, au mashimo basi tumia kiziba nyufa kuyaziba.
 
Back
Top Bottom