Special thread: TSD na CWT vina msaada kwa Mwalimu? Nini maoni yako?

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,487
TSD (Teacher's Service Department) pamoja na CWT (Chama cha Walimu Tanzania) vyote vilianzishwa kwa lengo la kumsaidia mwalimu kupata HAKI zake pamoja na STAHIKI zake katika kazi yake ya Ualimu. Je idara/chama hiki vinamsaidia mwalimu ipasavyo?

Nini maoni yako, kero yako, ushauri kwa serikali juu ya chama/idara hizi?
 
Labda ungeongelea CWT lakini TSD ni chombo kinachomsaidia mwajiri kwa hiyo wewe km mwajiriwa huwezi kukiondoa kiholela. Hata kikiboreshwa kitabaki na vielement vilevile. Ni tume ya utumishi ipo chini ya ofic ya rais ambaye ndo mwajiri wa wafanyakaz wa serikali
 
sasa hivi majukumu ya TSD yanaingiliwa sana na maofisa utumishi, mfano ni huku mwanza maamuzi ya TSD hayazingatiwi na yanapuuzwa na inaonekana utumishi na TSD ni idara mbili zinazokinzana
 
tofauti yao mmoja ni pepo mwingine ni msukule, wanafaida KWA serikali si KWA mwalimu
 
Labda ungeongelea CWT lakini TSD ni chombo kinachomsaidia mwajiri kwa hiyo wewe km mwajiriwa huwezi kukiondoa kiholela. Hata kikiboreshwa kitabaki na vielement vilevile. Ni tume ya utumishi ipo chini ya ofic ya rais ambaye ndo mwajiri wa wafanyakaz wa serikali
kama inamsaidia mwajiri, je inatenda haki? Watumishi wake wanao uwezo wa kutosha kusimama katika ofc hizo?
 
kama inamsaidia mwajiri, je inatenda haki? Watumishi wake wanao uwezo wa kutosha kusimama katika ofc hizo?
Ni kweli watumishi wake wapowapo tu...hata km wanauwezo hakuna cha maana cha kufanya wanasubiri kesi za walimu na kuwathibitisha kazin na kuwapa number za TSD
 
Ni kweli watumishi wake wapowapo tu...hata km wanauwezo hakuna cha maana cha kufanya wanasubiri kesi za walimu na kuwathibitisha kazin na kuwapa number za TSD
tena wengi wao ndo chanzo cha matatizo maana hayo madaraja yenyewe hayatoki kwa wakati au hayatoki kabisa, hizo tsd namba ndo mwl anaweza akazungushwa hadi akachoka akakata tamaa kufuatilia na pia kwenye kesi wanabeba wakuu wa shule maana wanatoa hongo kwao haki isitendeke.
 
Back
Top Bottom