Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Unajua bei ya bango ww?.unadhani utaweka mabango kwa utapeli za bukubuku za kuomba mikutanoni.

ccm walijipanga kwa nidhamu ya kutunza pesa za kampaini nyie mlitapanya pesa kwa kulewa na kuvunja miguu.
 
CCM chini ya rais Magufuli walitamba Sana kwamba mwaka huu hakuna haja ya kufanya kampeni kwani mgombea wao anakubalika Sana na wananchi...

Ni njia ya Matapeli kujipatia mlo , Msimu umefika , huku Zanzibar tunaita Bamvua hili wacha wavuvi wajivulie samaki.

WAJINGA NDIO WALIWAO
 
Unajua bei ya bango ww?.unadhani utaweka mabango kwa utapeli za bukubuku za kuomba mikutanoni.

ccm walijipanga kwa nidhamu ya kutunza pesa za kampaini nyie mlitapanya pesa kwa kulewa na kuvunja miguu.
Wambie sio bei ya bango tu ila hata hayo mabango yanayowekwa "yanalipiwa kodi"

sasa wajichanganye waweke mambango TRA wayakute hayajalipiwa,halafu waone "what next"
 
Ndugu zangu,

Nawatakia asubuhi njema, Kama ilivyo ada yetu ya kuangazia mambo kadhaa yanayohusu mwenendo wa Kampeni zetu leo nitafanya tathmini fupi ya robo ya mzunguko wa Kampeni. Nitazungumza katika namna ya Ulinganifu katika maeneo yafuatayo;

Hoja za Wagombea;
Kwa uchache wa muda leo nitazijadili Hoja za wapinzani hasa Vyama vikuu vya Upinzani (CHADEMA, CUF na ACT)
CHADEMA mgombea wao MHE TUNDU amezungumza hoja kuu zifuatazo:
1. Hoja ya kushambuliwa kwa risasi, imekuwa hoja kuu ambayo anaamini itampa kura za huruma.
2. Kuhakikisha masoko yanafanya biashara 24/7 bila kufungwa.
3. Atatoa Bima ya Afya kwa wote tena bila malipo - bure
4. Atafuta kodi kwa wafanyabiashara
5. Ataruhusu mifugo kulisha kwenye mbuga na hifadhi
6. Watumishi wa Umma wameokotwa majalalani
7. Vyombo vya Habari havina nafasi katika Kampeni zao
8. Watatoa ajira bila kutaja ngapi na wapi.
9. Miradi yote mikubwa itafanywa na Sekta Binafsi.
10. Atanyang'anya viwanja vyote vya mipira vya CCM

Hizo ni hoja alizozitoa akiwa majukwaani maeneo mbalimbali katika Kampeni zake, zipo hoja alizotoa akifanya mazungumzo na waandishi wa habari, nazo ni;

1. Chama kichangiwe Kampeni, gharama ni kubwa na Chama hakina fedha.
2. Wamejipanga wapambane wakiibiwa kura.
3. Serikali ya Awamu ya tano haijafanya kitu, deni la taifa limepanda na diplomasia ya kimataifa imeshuka
4. Chadema itamuunga mkono Maalim Seif Zanzibar


Ukizipima hoja hizi unagundua kuwa CHADEMA tayari wameshakata pumzi na kwamba wanaona mbele giza.

Inaendelea.
 
IMG-20200910-WA0074.jpg
 
Ndugu zangu,
Nawatakia asubuhi njema,
Kama ilivyo ada yetu ya kuangazia mambo kadhaa yanayohusu mwenendo wa Kampeni zetu leo nitafanya tathmini fupi ya robo ya mzunguko wa Kampeni. Nitazungumza katika namna ya Ulinganifu katika maeneo yafuatayo..!
Wewe akili yako ndiyo imefika mwisho wa kufikiri.
 
Nilitaka nikutukane nikaona jina lako Lumumba son nikakumbuka serikali haijakupa ajira unanjaa ndio maana hukumbuki Sera za lissu
Nenda kwa rungwe upigwe ubwabwa utaelewa vizuri sera
 
Sijuhi ni kwa nini ukiwa ccm akili zinahama, sasa huyu sijui kaandika nini, unaitajika utafiti kugundua uwezo wa akili kufanya kazi ukiwa ccm.
 
Ndugu zangu,
Nawatakia asubuhi njema,
Kama ilivyo ada yetu ya kuangazia mambo kadhaa yanayohusu mwenendo wa Kampeni zetu leo nitafanya tathmini fupi ya robo ya mzunguko wa Kampeni. Nitazungumza katika namna ya Ulinganifu katika maeneo yafuatayo;

Hoja za Wagombea;
Kwa uchache wa muda leo nitazijadili Hoja za wapinzani hasa Vyama vikuu vya Upinzani (CHADEMA, CUF na ACT)
CHADEMA mgombea wao MHE TUNDU amezungumza hoja kuu zifuatazo:
1. Hoja ya kushambuliwa kwa risasi, imekuwa hoja kuu ambayo anaamini itampa kura za huruma...

CCM wamewazidi wenzao kwa FEDHA.

..cdm wamewazidi wenzao kwa HOJA.
 
Imeisha hiyo! Anasubiri kuapishwa tena, pia hii ndio Time ya wananchi kuonja keki ya ruzuku za vyama moja kwa moja.
Hatuna haja na keki ya dhuluma, kama ni haki ya vyama kupewa ruzuku basi wapewe haki yao kama walivyopewa tangu awali, dhuluma siyo jambo jema.
 
Haya maneno nimewahi kumsikia akiyasema tangu alipokuwa Waziri katika Serikali ya JK.

Kama mtakumbuka zile hotuba zake maarufu za " aliselema. "

Huenda uelewa wake wa katiba, sheria, na demokrasia ya vyama vingi, ni kwamba miundombinu inayojengwa nchini ni mali ya CCM kwasababu ndio chama tawala.

Hata madai yake kuwa wapinzani wakichaguliwa watavunja miundombinu na kuuza screpa, huenda anaamini hivyo kwa dhati ya moyo wake.

Wako waliojisemea kwamba tuna raisi wa ajabu haijapata kutokea.

cc Richard, Chige, Nguruvi3, Mag3, @Erythrocite, tindo
 
Back
Top Bottom