Kuna msemo usemao “When life gives you lemons, make lemonade”

Kwa wale ambao tunaishi mjini na tuna wazazi, ndugu, jamaa na marafiki waliopo vijijini, tutumie mabango ya CCM kuwahamasisha hao watu wetu waliopo vijijini kuhakikisha hawapigi kura hata moja kwenye picha hizo zilizo zagaa kwenye makazi yao. Badala yake tuwahamasishe wapige kura ya urais kwa Tundu Lissu na zile za wabunge na madiwani ziende kwa Chadema.

Kazi yetu ni imerahisishwa na hayo mabango. Ni kuwaeleza wenzetu kwamba katika sura zilizopo kwenye hayo mabango, wasiweke kura zao.
 
Kuna mtu ameshikwa jugular vein anataka kufa sasa pumzi inaenda kukata anatupatupa miguu

Kamateni hapo hapo msiachie kabsaaaa
 
Kuna msemo usemao “When life gives you lemons, make lemonade”

Kwa wale ambao tunaishi mjini na tuna wazazi, ndugu, jamaa na marafiki waliopo vijijini, tutumie mabango ya CCM kuwahamasisha hao watu wetu waliopo vijijini kuhakikisha hawapigi kura hata moja kwenye picha hizo zilizo zagaa kwenye makazi yao. Badala yake tuwahamasishe wapige kura ya urais kwa Tundu Lissu na zile za wabunge na madiwani ziende kwa Chadema.

Kazi yetu ni imerahisishwa na hayo mabango. Ni kuwaeleza wenzetu kwamba katika sura zilizopo kwenye hayo mabango, wasiweke kura zao.
😂😂😂😂😂😂
,🤭
 
Mkuu umefanya jpili yangu ianze vizuri point kubwa sana
 
Safi sana hizo hela za kutengeneza mabango zingeenda kununua madawa hospitalini kusaidia wazee wetu. WATANZANIA WAMEKUWA NA AKILI HAWAANGALII TENA MABANGO.
 
Mhe. Lissu salaam, pole na majukumu na mizungunguko yako ya kunadi sera zinazotugusa sie tulio wanyonge haswa. Binafsi nimekuwa nikikufutilia kwa karibu kampeni zako popote kwa njia ya mtandao na agharabu niliwahi kuhudhuria kwenye uzinduzi wa kampeni moja mkoa wa nyanda za juu kusini, hakika Mungu akulinde.

Kuna mambo mengi yakuleta matumaini umekuwa ukiyaeleza vizuri namna utakavyo yashughulkia kwa kweli inatia moyo. Lakini kuna jambo moja bado hujaliweka wazi sana namna utakavyo shughulika nalo na hili unalijua lina kundi kubwa la watu na unalijua vizuri.

Binafsi pia ningependa uliongee kila pahala unapokwenda kunadi sera (nitalieza). Kwakifupi niorodheshe mambo unayoyaeleza vizuri na hayana shaka ili uliongeze na hilo liwe miongoni mwa haya(msomaji waweza ongeza ambayo nimesahau) .

1. Kila mtanzania kumpatia bima ya afya
2.Kuongeza mishahara kwa watumishi(mujibu wa sheria)
3. Kulipa malimbikizo kwa watumishi.
4. Kurudisha fao la kujitoa
5. Kupunguza makato bodi ya mikopo mpaka 3% ya awali
6. Kutoa mikopo kwa waombaji/ wanafunzi wote elimu ya juu.
7. Kulipa fidia kwa wahanga waliobomolewa nyumba zao kupisha ujenzi wa barabara na kuwafariji wahanga wa tetemeko Kagera.
8. Kuondoa kitambulisho cha ujasiliamali kwa machinga na wengineo
9. Kuwapatia watanzania katiba mpya(ya Jaji Warioba).
10. Kurudisha ardhi iliyopokwa kwa wananchi.
11. Kuwatoa magerezani Mashehe wa uamsho(na wanaharakati waliobambikiwa kesi).
12. Kuunda tume ya maridhiano kwa viongozi waliojihusisha kunyanyasa raia bila makosa ukiwemo wewe, kuuweka bayana wa mambo hayo na sababu ya kufanyika kwake na kisha kusamehana.
13. Kuondoa vikwazo kwa wakulima (kundoa kodi za magetini, kuwa na soko huru na upatikanaji rahisi wa pembejeo za kilimo pamoja na bei zake).
14. Kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara(kuondoa kodi mpaka kufika 10%, kuifumua upya TRA, nk).
15. Kuweka mazingira safi ya Uwekezaji ili kukuza uchumi na kuongeza ajira.
16. Kurekebisha mfumo wa elimu ili uweze kumpa maarifa mwanafunzi na sio kuongeza ufaulu tu bila kuwa na maarifa. (Kuaandaa wasomi watakaoajirika popote duniani na kuwa katika soko la ushindani).
17. Kuzipa nafasi sekta binafsi kuratibu shughuli zao kwa uhuru na kuifanya serikali kuwa msimamizi na kuzipa mazingira safi ya shughuli zao.
18. Kuwa na serikali za majimbo na viongozi wake kupatikana kwa kuchaguliwa ama kuondolewa na wananchi(kurudisha nguvu na mamlaka kwa wananchi).
19. Kulinda na kutetea haki, utu, na uhuru wa kila raia.
20. Kujenga uhusiano mzuri na mataifa mengine(Diplomacy Restoration)ambayo pengine yamezorota hivi karibuni.
21. Kuondoa laana ya rasilimali(wananchi kutobugudhiwa/kubezwa kwa rasilimali zinazopatikana maeneo waliopo/yanaowazunguka). Raia kuwa wanufaika kwa rasilimali zinazopatikana mahala walipo.
22. Kurudisha uhuru wa vyombo vya habari (kuondoa sheria kandamizi za utoa aupokeaji wa habari)
23. Kuondoa kinga ya viongozi na kupunguza mamlaka ya Rais. (Kuweza kushtakiwa akifanya makosa). nk nk

Kwa uchache hayo ndiyo nayasikia mara nyingi na yanatugusa mojakwamoja. Sasa hitaji langu nitajikita kwenye namba 16 kwa sababu kwa namna moja ama nyingine vijana na wazazi wameathiriwa vibaya mno na hili.

MFUMO WA ELIMU na AJIRA kwa VIJANA
------------------------------------------------------
Mh. T. A. Lissu kama unavyojua mfumo wa elimu umekuwa ukituandaa vijana kuwa tegemezi(dependents) yaani soma, faulu, na uandaliwe ajira. Mfumo huu hautupi uwezo wa maarifa na kisha kupambana na mazingira bali uajiriwe baada ya kuhitimu. Hiki ndicho kinachogharimu wasomi wengi na kufifisha matumaini kwa wazazi wanaosomesha vijana wao. Nimeridhika na namna unavyotaka sekta binafsi zipunguze tatizo la ajira lakini ujue kuna kundi lililomaliza vyuo toka 2015-2020 almost 6years halina ajira rasmi na liliandaliwa na mfumo huo tegemezi wa elimu.

Hivyo basi ningependa katika kampeni zako ungeliongelea katika kila mkutano wa kampeni ipi mipango mikakati ya dharura ya kushughulika na kundi hili kabla ya kuanza na mfumo mpya wa elimu. Kumbuka hawa vijana ni kundi kubwa wao na wazazi/walezi wao wanataka kujua hatma yao na namna utawafanya wawe kwenye ajira rasmi.

Serikali ya sasa nikama haina mipango yoyote juu ya hili na ndio maana kumekuwa na ukosefu mkubwa wa ajira kwa miaka hii mitano. Hawa ni vijana waliosomeshwa na wazazi maskini kwa kuuza mazao yao, mali zao, mashamba, mifugo ili tuu wapate elimu.

Katika kundi hili ni wachache wanaopatiwa ajira rasmi agharabu kwa wale wenye ndugu walio na nafasi kubwa serkalini ila the rest wapo mitaani. Kwa heshima yako naomba utoe mwongozo kwa vijana, wazazi au walezi kila mkutano wako wa kampeni maana ni tatizo la nchi nzima.
Asante na kila la kheri katika mapambano yako. (Nashuku katika kampeni zako jana 27/09/2020 Musoma umeanza kuliongelea kiundani, ningependa liwe ni endelevu kwa kila mkutano wako).
Naomba kuwasilisha.
 
Haikutegemewa na CCM wala vyombo vingine vinavyousapoti CCM kwamba Lissu angepokelewa kwa bashasha kubwa kiasi kile mikoa ya Geita na Mwanza. Ukiangalia video za mapokezi ya Lissu unaona tofauti kubwa kati ya mapokezi ya Lissu na yale ya Magufuli.

Mapokezi ya Lissu yamejaa raia wenye bashasha, shangwe na vifijo huku mapokezi ya Magufuli yakitawaliwa na ukimya na protokali za serikali.

Matokeo ya mwenendo huu yametoa ishara mbaya kwa CCM kwamba kwa uhalisia mambo sio mazuri kwa CCM.

Tumeona ukimya wa muda kwa mgombea wa CCM wiki hii na ghafla katibu mwenezi wa CCM akiibuka na kuzungumza kwa taharuki na hata kwa hasira na kumtusi Lissu kwa kumuita msukule. Tumeona NEC nao wakianza kupoteza uvumilivu na kuanza kuingilia kampeni za Lissu kwa kumtaka ajieleze na afike ofisini.

Haya yote na mengi yajayo ni matokeo ya kimya cha mgombea CCM wiki hii na tutashuhudia mengi zaidi kuanzia sasa kwani watumishi waneonekana kupwaya na kufanya mambo kuwa magumu upande wa CCM.
 
Ni wingi wa watu kujitokeza kumsikiliza LISSU angalia hapa ni Tarime Vijijini Leo hiii

1601219127852.png
 
Eti ""Mapokezi ya Lissu yamejaa raia wenye bashasha, shangwe na vifijo huku mapokezi ya Magufuli yakitawaliwa na ukimya na protokali za serikali. ''"
Sasa utamfananisha Jpm na huyo tundu wenu ! JPM bado ni Rais wa nchi ulitaka apokelewe kihuni kama huyo kibaraka wenu!
 
Back
Top Bottom