Shehullohi

JF-Expert Member
Jul 21, 2020
2,545
2,000
Wakati wa Nyerere kwa Mrema mtu kama anatakubebwa kama jeneza mwacheni, shida iko wapi? Polepole kwa Lissu; ukisikia msukule umeonekana pahala utavutiwa kwenda kuushangaa.

Naambiwa wawili hawa asili yao ni mkoa wa Mara.
 

selemala

JF-Expert Member
Feb 14, 2007
230
250
😂 Sina hata nia ya kugombea na sidhani.. Kama ningekuwa na nia ningefatilia vizuri na kujua wapi pa kuanzia.. hata hizo sewage system ni jambo pia la kuangalia lkn si kila kitu chakumsukumizia rais..

Kwa bahati mbaya sana kwa mfumo wa utwala wa sasa Raisi ndio kila kitu, na hili halitekelezeki , hasa katika mazingira na utamaduni wa kiTanzania.

Kuna haja kubwa ya kubadili mfumo huu. kwa mfano, Raisi abaki na majuku ya kitaifa, wakati majukumu ya kimkoa au kikanda yapewe viongozi wa maeneo husika watakaochaguliwa na kuwajibika, sio kwa Raisi, bali kwa wananchi wa maeneo hayo, n.k
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,875
2,000
This is the right time kutumia helicopter sasa..

Kwa helicopter, ni siku 5 kwa sababu mkoa mmoja anaweza kufanya mikutano isiyopungua 5 hadi 7..

Watumie Helicopter..

Ni vyema wananchi wote wa mikoa yote wapate elimu ya URAIA kujua WAJIBU na HAKI zao..

Tundu Lissu si tu anapiga kampeni, pia anafundisha somo muhimu la Uraia na sheria wananchi wote ili waweze kutambua HAKI na WAJIBU wao...

This man is very good motivational Speaker. This man is a true revolutionalist...
 

m4cjb

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,367
2,000
Vimba pasuka, Mwamba anafungia dar na kusafisha kabisa nzi wa kijani
Mleta mada una wenge,

Dar si ndio Lissu alikofungua kampeni yake viwanja vya Mbagala ikafuatia na Tanganyika packers.

Naona mmevurugwa mpaka mnarudia rudia mikoa.
 

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
4,934
2,000
Tusipende wala tusipende ukweli ni kwamba Watanzania wanapenda zaidi ya Chama kimoja na bunge halionyeshi ukweli wa nchi ilivyo na Lissu, Lowassa hata Seif wamethibisha hilo.

Ushauri hawa watu wengi hivi mkiwapuuza na kuwazuia wasiongee baada ya uchaguzi ni kutunza usaa. Mfano angalieni kanda ya ziwa walivyo mshabikia lissu tofauti na mategemeo ya watu hata upinzani wenyewe. Malalamiko ya Tanapa sio ya kupuuza maana sio ya kisiasa ni watu kweli wanalalamika, kazi kwa vijana ni tatizo kubwa. Lakini Watanzania wengi kuliko yote wanaonekana wamechokwa kuonewa. Halafu kibaya kuna video mazuri ya Polisi yameonekana na mabaya yameonekana.
 

daktari feki

Senior Member
Jun 25, 2020
166
250
Wananchi hawana muda was kwenda kumsikiliza mouth piece ya mabeberu.

Lisu kaletwa na mabeberu ili aende ikulu kuwapatia rasilimali za nchi hii.

Hatumtaki.
Wewe utamsikiliza mnunuzi wa korosho za kusini siyo! Tusipangiane. Mimi nitawasikiliza wote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom