Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Atawaeleza nini wana kagera???


Kawatukana, kala hela zao za tetemeko, kamtesa mtoto wao Kabendera hadi mama yake amefariki na mbaya zaidi hakumruhusu hata kwenda kumzika
Hoja mfu kabisa.ni mahabusu wangapi ambao hurusiwa kwenda kuzika na kurudi mahabusu?

Halafu huyo kabendera ni mtoto wa kirundi mwenye uraia wa kuandikishwa mtoto wa Kabendera shinani aliekuwa mtangazaji wa resdio burundi.

Rais hawezi kwenda kagera kufanya kampeni wakati kagera ina msiba nzito wa wanafunzi kumi na majeruhi saba walioungulia kwenye bweni lililochomwa na wale nia #OVU.

MUWE MNAFANYIA TAFITI BONGO ZENU KABLA YA KUPOST UJINGA.
 
Ile dose ya Mafinga ya jana ilikuwa kali sana. Kila baada ya Lissu kuhutubia wanaoamua kumpigia kura wanaongezeka.
 
Mhe. Rais kwa vile unaenda Mkoa wa Kagera ingependeza kama ungewasaidia Tshs.50,000,000 (Millioni Hamsini) kuirudisha shule hiyo katika hali yake iliyokuwa nayo hapo awali. Nawasilisha.
Me nadhani hilo itapendeza zaidi likifanyika baada ya uchunguzi ili chanzo cha ajali kijulikane. Anapaswa kutoa rambirambi.
 
Mh sana Rais na Mgombea Urais wa CCM ndugu John Magufuli pokea ushauri wangu huu wa bure kabisa.

Mosi, nakushauri sana tena sana. Usimjibu Tundu Lissu maana kwa kufanya hivyo utaendelea kutapata aibu kubwa.

Level za Lissu ni za juu sana sioni mwanaccm wa sasa wa kuweza kushindana nae kwa hoja kwahiyo kwa heshima yako na ya chama chako jikite tu kwenye sera zenu. Hilo la kwanza.

La pili nakushauri usipende kuiga na kutaka kutembelea nyota ya Lissu. Usidandie treni kwa mbele hasa ahadi ambazo chama chako haijazifanyia utafiti hivyo kutoka na uwezo wa kuzitekeleza km mlivocopy sera ya Chadema ya elimu bora na bure. Hili pia litakufedhehesha ww binafsi na chama chako iwapo utaendelea.

Ni hayo tu kutoka kwangu, kukubali au kukataa ni uamuzi wako. Ushauri kama huu huwezi kupewa na mwanaccm wao kazi yao kubwa ni kujipendekeza ili wapate vyeo kwa kukudanganga kua unakubalika unapendwa wkt hali halisi mtaani wewe mwenyewe umeshaiona.

Nukuu ya kwenye katiba: "Rais hatawajibika kufuata ushauri wa mtu yeyote"
 
Na si ajabu ukasikia kuna viongozi watakaowajibishwa. Pia kutoa amri/mchango wa kujenga shule haraka. Nina mashaka na Bw Yule.
Hiyo kesho agiza agiza na amri zitakuwa nyingi. Leo atakuwa anachambuliwa taarifa nyeti na nyoka wake wa kagera ili kesho akazimwage kwa ustadi mkubwa.
 
Hama kweli kampeni ni kazi ngumu.
Watu wananyeyekea hadi kubadilishi sauti, wanakuwa wanyonge hadi wanatia huruma.

Ila hili la kumpa mwalimu chai wakati huu wa kampeni si rushwa hiyo?
Takukuru wapo makini sana wanafuatilia.
 
yaani niko naskiliza kampeni za CCM muleba
mgombea wetu hajui kabisa kushawishi watu
hana sera
hapangilii hotuba

anarudiarudia maneno

hamna kitu hapa kwakweli

kila mda unarudia rudia unatwambia sisi masilingi utamuongezea ubalozi ili iweje sasa?

eti tibaijuka nimekataa asistaafu, halafu sisi inatusaidiaje?


hebu CCM Tuelezeni mtatufanyia nini bado hamjaeleweka
 
Leo amesema Wanamuleba mkichagua mbunge na madiwani wa CCM tutawaletea maendeleo watu wa vyama vyote. Hawa si ndiyo walituambia tusipochagua CCM maendeleo hatupati na la kuwafanya hatuna.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom