Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Atawaeleza nini wana kagera???


Kawatukana, kala hela zao za tetemeko, kamtesa mtoto wao Kabendera hadi mama yake amefariki na mbaya zaidi hakumruhusu hata kwenda kumzika
Safari hii anaenda wakati kuna shule imeungua moto na watoto kadhaa wamepoteza maisha (RIP) na wengine kujeruhiwa vibaya (get well soon), je ataenda 'kuwananga' wana Kagera tena?
 
Eh!Eh!Eh!Eh! Yule Mzilankende anaenda tena huko? Na sasa mmeongeza maafa ya moto! Sijui wasanii wataendelea na burudani zao wakati kuna msiba? Je bila wasanii wananshomile watakuja kusikiliza vidonge vyao? Nadhani habari ya MV Victoria Hapa Kazi Tu itakuwa imewafuta machozi ya tetemeko, ukimwi, Katerero, mto ngono, vita ya kamera na huo moto wa shule ya Byamungu Islamic?!!?!? Poleni wana Kagera kuweni na moyo wa upendo na subira!
Naona upo mbagala unapiga porojo.. Haya, kachukue bk 7
 
Sizungumzii kampeni nazungumzia kwenda kwenye ziara za kikazi,na ata akienda Leo atapokelewa tu na watu wote muwe mnajaribu basi kufanya uchunguzi mitaani kuuliza wananchi nani watamchagua maana mitandaoni upotoshaji ni mwingi sana,nakushauli nenda vijiweni,masokoni,migahawani,kwenye bodaboda na mitaani kila eneo wahoji watu kwa siri angalau 10 kila eneo alafu utapata majibu,unaoona wamejaa kwenye mikutano hao ni wale wale tuliowazoea ambao wanamsemo wao 'BORA KUZALIWA ULAYA MBWA KULIKO AFRIKA BINADAMU" hivyo jipe home work ya muda mfupi alafu lete mlejesho.
Magufuli akipata kura elfu moja tu Kagera akashukuru Mungu.
 
Wenye chuki mnawasemea mioyo wahaya.

Mngejua wahaya wepesi kusamehe na kufocus na maendeleo ndio maana wengi ni wasomi,,,


Ukiishi nao karibu utajifunza mengi.
 
Mhe. Rais kwa vile unaenda Mkoa wa Kagera ingependeza kama ungewasaidia Tshs.50,000,000 (Millioni Hamsini) kuirudisha shule hiyo katika hali yake iliyokuwa nayo hapo awali. Nawasilisha.
Kwani yeye ndiye aliyeichoma moto shule hiyo? Kuchoma mchome nyie, kuikarabati mumwachie yeye?
 
Magufuli akipata kura elfu moja tu Kagera akashukuru Mungu
Kagera ina wilaya zisizopungua 06 na kati ya hizo ccm uchukua 04 sasa nauliza kama mnazungumzia kauli yake ambayo iliwalenga wahanga wa tetemeko,vipi kuhusu shule iliyojengwa pale kutokana na pesa hizo itazalisha watu wasomi kiasi gani kulinganisha na kama wangepewa mkononi wakazitafuna,na ikumbukwe kwamba pesa walipewa lakini nyingi ziliangalia huduma muhimu,kifuta jasho,nitolee mfano wa nchi iliyolipa fidia kwa wananchi waliokumbana na majanga asili duniani.
 
Back
Top Bottom