Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
SEPTEMBA 5: CHAUMA KUFUNGUA RASMI KAMPENI MANZESE, DAR
Mgombea Urais kupitia CHAUMMA, Hashim Rungwe ametangaza kufungua rasmi kampeni za chama chake viwanja vya Bakhresa vilivyopo Manzese Dar es Salaam, Septemba 5
Awali chama hiko kilipanga kufungua kampeni zake mkoani Mara, zoezi ambalo limesitishwa kwa sababu ambazo hawajaziweka dhahiri, lakini wamewaomba radhi wafuasi wao
Rungwe anawakaribisha watu mbalimbali kuhudhuria ufunguzi huo ili kusikiliza sera zinazogusa wananchi moja kwa moja ambazo kwa kiasi kikubwa amekuwa akiizungumza zaidi sera ya wali kuku
AGOSTI 15: UCHUKUAJI WA FOMU NEC KUOMBA UTEUZI KUWANIA URAIS
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mh. Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akikabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais kwa Mgombea wa CHAUMMA, Hashim Rungwe na Mgombea Mwenza, Mohammed Masoud katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 10, 2020.
Chama hicho kinakuwa cha kumi na moja (11) kuchukua fomu. Uchukuaji fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza Agosti 5 hadi 25, 2020.
AGOSTI 25: KUIDHINISHWA NA NEC KUGOMBEA URAIS
Tume ya Taifa ya Uchaguzi( NEC) imempitisha Hashim Rungwe kuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHAUMMA baada ya kutimiza masharti ya uteuzi
Naye Mohamed Masoud ameteuliwa na Tume hiyo kugombea nafasi ya Makamu wa Rais kwa tiketi ya chama hicho.
-----
Mgombea Urais kupitia CHAUMMA, Hashim Rungwe ametangaza kufungua rasmi kampeni za chama chake viwanja vya Bakhresa vilivyopo Manzese Dar es Salaam, Septemba 5
Awali chama hiko kilipanga kufungua kampeni zake mkoani Mara, zoezi ambalo limesitishwa kwa sababu ambazo hawajaziweka dhahiri, lakini wamewaomba radhi wafuasi wao
Rungwe anawakaribisha watu mbalimbali kuhudhuria ufunguzi huo ili kusikiliza sera zinazogusa wananchi moja kwa moja ambazo kwa kiasi kikubwa amekuwa akiizungumza zaidi sera ya wali kuku
AGOSTI 15: UCHUKUAJI WA FOMU NEC KUOMBA UTEUZI KUWANIA URAIS
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mh. Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akikabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais kwa Mgombea wa CHAUMMA, Hashim Rungwe na Mgombea Mwenza, Mohammed Masoud katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 10, 2020.
Chama hicho kinakuwa cha kumi na moja (11) kuchukua fomu. Uchukuaji fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza Agosti 5 hadi 25, 2020.
AGOSTI 25: KUIDHINISHWA NA NEC KUGOMBEA URAIS
Tume ya Taifa ya Uchaguzi( NEC) imempitisha Hashim Rungwe kuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHAUMMA baada ya kutimiza masharti ya uteuzi
Naye Mohamed Masoud ameteuliwa na Tume hiyo kugombea nafasi ya Makamu wa Rais kwa tiketi ya chama hicho.
-----
HOJA KUHUSU CHAKULA NI YENYE NGUVU, TUSIICHUKULIE KIMZAHA
Habari wadau.
Mgombea wa Urais wa CHAUMA ndugu Hashimu Rungwe alikuja na hoja ya chakula kwa watoto wa shule na wagonjwa hospitalini.
Ukimsikiliza ana mantiki,imagine watoto wa shule kukaa shule masaa takribani 10 huku hajala chochote sijui mtoto wa hivi ataachaje kuwa na utapiamlo na kudumaa kiakili na kimwili. Wote mnakumbuka ishu ya vijana wa Taifa stars kule Afcon, Watanzania tulionekena kuwa wafupi na wenye vimiili vidogo vidogo hivyo kushindwa kuhimili mashindano mbalimbali.
Leo hii uwezo wa watu kufikiri ni mdogo sana kutokana na lishe duni,uzoefu unaonesha kwamba mtoto huanza kudumaa kimwili na kiakili pindi akiachishwa kunyonya na kuanza kulishwa chakula ambacho sio balanced diet kutokana na maisha ya kuunga unga na kubabaisha ya watanzania wengi.
Naomba vyama makini hasa vya upinzani viichukue hii hoja na kuinadi kwa wananchi maana ni hoja ya msingi sana na yenye mashiko ikizingatiwa kwamba hapo awali miaka ya nyuma watoto walikua wanalishwa mashuleni na wagonjwa na wauguzi kupewa chakula.
Badala ya kila siku kunadi madaraja sijui barabara nk mambo ambayo ni wajibu wa serikali na bunge kuyaratibu kwenye bajeti ya kila mwaka,vyama vije na policy direction kwenye sekta za afya na lishe kama anavyofanya Mzee Rungwe, technicalitie za namna ya kuzitekeleza ndio itakuwa wajibu wa serikali iliyonadi sera husika. Watanzania tuache kuichukulia siasa kama mizaha ya utani wa jadi wa yanga na simba,siasa ni hatima ya maisha yetu. Tutafakari na tuchukue hatua.
KWANINI SIKUBALIANI NA UBWABWA WA HASHIM RUNGWE
_____________________
_Na Godfrey Kassim, PhD (Sayansi ya Chakula)_
______________________
Tulivyokua wadogo tulikua tukikatazwa kula sehemu yoyote isipokua nyumbani tu. Hayo ndio mafundisho halisi ya kiafrika tuliyorithishwa na wahenga.
Nilipoanza kusomea elimu ya sayansi ya chakula nikafahamu kwanini wazee wetu walikua wapo sahihi.
Wataalamu wa elimu ya chakula husema "You Are What You Eat" yaani chakula kina nafasi kubwa katika kumjenga mwanadamu.
Wataalamu wamebaini kwamba chakula hujenga afya ya mwili na akili sambamba na kuathiri tabia ya mwanadamu.
Kuna baadhi ya vyakula hudhoofisha akili hivyo kuathiri ufaulu katika elimu.
Vipo vyakula vingine vinadhoofisha afya ya uzazi na kusababisha ugumba hivyo kupunguza idadi ya watu.
Vipo vyakula vinavyochangia kupunguza/kufuta aibu hivyo kuchangia kwenye mporomoko wa maadili unaosababisha ongezeko la uhalifu.
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba vyakula vinavyotolewa mashuleni si salama kwa mtoto kwasababu hubeba madhara mengi sana.
Kuna visa vingi vya vifo mashuleni katika nchi mbalimbali ulimwenguni vinavyosababishwa na kula chakula cha shuleni.
Sambamba na hayo, watafiti wanaeleza kwamba usalama wa chakula hupungua katika harakati za kuandaa chakula cha watu wengi kutokana na uangalifu kuwa mdogo.
Hata hivyo, ni rahisi kwa muhalifu kufanya hujuma ya kudhuru wanafunzi endapo chakula kinaandaliwa mashuleni.
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Stanford huko Uingereza mnamo mwaka 2015 unaonesha kwamba chakula cha mashuleni ni hatari kwa sababu huwa na kiwango cha sumu hatari (Stanford study indicates school meals may expose children to unsafe levels of BPA).
TUREJEE MAFUNDISHO YA WAHENGA*
HASHIM RUNGWE: NITAPELEKA BAHARI DODOMA
Kuelekea uchaguzi kila mgombea anakuja na sera zake. Kama bado hukuisikiliza sera za Hashimu Rungwe hizi hapa.
1. Watoto kula ubwabwa shuleni
2. Kupeleka bahari ya Hindi Dodoma
Kwa sera hizo IKULU ataingia?
RUNGWE: MAFAO YA WAFANYAKAZI LAZIMA YALIPWE KWA WAKATI
Mgombea Urais Mh. Hashim Rungwe: Mafao ya Wafanyakazi lazima yalipwe kwa wakati.
Huyu Mzee ana hoja nzito, Laiti wafanyakazi wangejua siri kwenye hii mifuko yao ya akiba? Duh! wangeingia barabarani kuitoa CCM madarakani mapema sana.
Hivi ni wanini Ukaguzi huru wa Mahesabau ya NSSF na PSSSF haifanywi na wafanyakazi kupewa ripoti kila mwaka?
Malipo ya Mafao (Fao la Kukosa Kazi/kujitoa) na Fao La Wazee kipindi hiki hayatoki. Watu wanasumbuliwa, miezi 3 mpaka 4 hadi 6.
Kipindi hiki wafanyakazi wanasumbuliwa, fao la kukosa ajira na wazee. Pesa zimeenda wapi?
Usikute mmeshafanya yenu Tena eeh
LISHE BORA KAMA SERA YA CHAUMMA ISIPUUZWE
Mgombea Urais kwa tiketi ya CHAUMA, Bwana Hashim Rungwe ana hoja ya msingi anayotaka kutuambia watanzania, tusimpuuze na kauli yake ya lishe Bora na kula ubwabwa.
1. Lishe bora hutatua changamoto za maradhi ya mara kwa mara. Hivyo kuipunguzia serikali mzigo wa kujenga hospital, kununua vifaa vya tiba na madawa. Naamini ubwabwa ambao watu wa vijijini hula siku ya sikukuu tu, ukitumika vema tutakuza uchumi kwa kupunguza bajeti ya wizara ya Afya na kupeleka kwenye viwanda.
2. Lishe bora huongeza kuzaliana, watu watazaliana na kukua bila shida, hapa nchi itapata nguvu kazi ama rasilimali watu ya kutosha. Hawa ndiyo watakaoipeleka Tanzania kuwa donor country huko mbeleni.
3. Ubwabwa huu huu ambao tunaudharau, utawafanya watanzania waishi kwa furaha sana. Ukizingatia hiki ni chakula pendwa kwa Watanzania wa rika zote. Furaha ni chimbuko la fikra chanya. Mwenye njaa siku zote hawezi kuwaza maendeleo. Atawaza chuki, unafiki, wivu na visasi. Lakini ukishiba, Wala huwazi hayo.
4. Watanzania wengi sasa hivi ni legelege, watoto wao wanaozaliwa ni lege lege. Tunakaribia kupoteza ile spishi ya majayanti. Kwasababu, wazazi wao kwa kukosa lishe wanatoa sperms na mayai yasiyo bora kwa kukosa Lishe. Tusiipuuze hoja ya Mh. Rungwe ili tuzae watoto kama akina Goliath na Samson.
Wachache sana tumemwelewa huyu mzee. Ana hoja za msingi kabisa.
HASHIM RUNGWE ANAWEZA KUMZIKI KURA LISSU
Wapendwa
Tangu tarehe 26 Agosti 2020 kipenga kimepulizwa na kampeni zimeanza kwa wagombea wa vyama vyote kuelekea Oktoba siku itakapopigwa kura za kumpata Rais, Wabunge na Madiwani.
Naenda kwenye hoja moja kwa moja. Mgombea wa chama cha Chauma ndg Hashim Rungwe Spunda ameonesha uwezo mkubwa wa kuleta hamasa kunogesha kampeni zake kuelekea uchaguzi wa Rais.
Lisilokwepeka ni kwamba Umma wa Watanzania ambao wengi hawapo humu mitandaoni wanaona na kishuhudia namna ambavyo mgombea wa CCM ndg John Pombe Joseph Magufuli ameitendea zaidi ya haki nafasi ya Urais wa Jamhuri, pamoja na namna alivyoliongoza taifa kwenye vita dhidi ya Covid19 hawana uchaguzi mwingine zaidi ya kumpa ushindi wa kishindo kwenye huu uchaguzi.
Lolote linaweza kutokea kwa wagombea wengine, lakini kwa mara hii kura za mzee Rungwe zinaweza kuvuka idadi ya kura atakazopata Tundu Lissu kwa sababu mgombea huyo wa CHADEMA anakosa uwezo wa kujenga hoja za kisiasa na badala yake anatumia uwanja wa siasa kutoa lugha za matusi na kudhalilisha huku akionyesha kuwadharau wapiga kura huku akitishia yeye na chama chake kufanya lolote hata kwa kuvunja amani endapo hawatapewa ushindi hapo Oktoba.
Ahadi ya kuwapatia chakula watoto mashuleni na kusisitiza mlo kamili kwa wananchi inaonekana kabisa anaweza kuibua hoja maridhawa tena fikirishi zaidi ya mgombea wa CHADEMA.
Hashimu Rungwe Spunda ataibuka na kura nyingi zaidi ya Tundu Antipas Lissu ambaye mpaka sasa hoja yake kuu ni kwamba alipigwa risasi hivyo anafaa kupewa kura.