Special thread: Kwa waombaji wote wa mikopo 2017/2018 (HESLB)

kama tunavyo jua tarehe 6/08/2017 HESLB inafungua mfumo wake kuruhusu wanafunzi kuomba mikopo, na mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 4/09/2017.

Huu uzi uwe special kwa matatizo, maswali, dukuduku au misunderstanding yoyote ile inayo husiana na HESLB wakati wa ku apply na baada ya kuapply kwenye mfumo wao wa OLAS.

Kama unashida yoyote ya mikopo/HESLB/OLAS uliza hapa wazoefu na huo mfumo/walio kwisha apply watakujibu hapa.

Kwa wazoefu wote tushirikiane kujibu/kutoa ushauri kwa yeyote atakaye kuwa na tatizo linalo husiana na mikopo/HESLB/OLAS.

.....NAWASILISHA......


Websites za HESLB hizi hapa chini:-
www.heslb.go.tz
www.olas.heslb.go.tz


.......................UPDATES.....................

Dar es Salaam.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa wanafunzi kuwasilisha maombi ya mikopo.
Hatua hiyo imeelezwa inalenga kutoa nafasi kwa wanafunzi walioshindwa kufuata masharti kuyakamilisha.
Mkurugenzi Mkuu wa bomwananchi Abdul-Razaq Badru amesema muda huo umeongezwa hadi Septemba 11 badala ya Septemba 4.
"Tumesogeza mbele kwa siku saba zaidi ili walioshindwa kufuata vigezo wakati wa kujaza fomu wafanye hivyo," amesema.
Amesema hadi kufikia jana Agosti 29, wanafunzi waliojitokeza walikuwa 49,282 lakini ni 15,473 waliokamilisha maombi kwa njia ya mtandao.

mwananchi


...............UPDATES.............

MASWALI NA MAJIBU KWA WAOMBAJI WA MIKOPO KWA 2017/2018. Fungua link hapa chini
MASWALI NA MAJIBU KWA WAOMBAJI WA MIKOPO KWA 2017/18



...........UPDATES..........


Hii hapa Orodha ya majina ya wanafunzi watakaopata mikopo ya HESLB



Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru
Dar es Salaam. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema baada ya uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018, orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo imekamilika.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Jumatano Oktoba 18,2017 amesema Sh34.6 bilioni zimetengwa kwa ajili ya wanafunzi hao 10,196.
Amesema kwa jumla Sh108.8 bilioni zitatolewa kwa wanafunzi 30,000 wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
Badru amesema orodha ya awamu ya kwanza inapatikana kwenye tovuti ya Bodi ya Mikopo http://www.heslb.go.tz/ na itatumwa kwa vyuo husika.
Amesema orodha nyingine (batches) zitafuata kwa kadri utaratibu wa udahili na uchambuzi unavyokamilika.
“Lengo ni kutoa majina ya wote waliofanikiwa kupata mkopo kabla ya vyuo kufunguliwa mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba, 2017,” amesema.
Mkurugenzi mtendaji huyo amesema orodha hiyo ya wanafunzi 10,196 imepatikana baada ya kupokea na kuchambua awamu ya kwanza ya majina ya wanafunzi 32,495 waliopata udahili katika chuo kimoja.
“Itakumbukwa kuwa moja ya sifa kuu za kupata mkopo ni mwombaji kupata udahili katika taasisi ya elimu ya juu inayotambuliwa na Serikali,” amesema.
Amesema wanafunzi waliopata udahili katika chuo zaidi ya kimoja na ambao wana sifa za kupata mikopo, watapangiwa mikopo baada ya kuchagua na kuthibitisha chuo watakachojiunga kwa ajili ya masomo.
Wakati huohuo, Badru amesema wanatarajia kuanza kutuma vyuoni fedha za mikopo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao wamefaulu mitihani yao kuanzia leo Jumatano, Oktoba 18, 2017.
Amesema Sh318.6 bilioni zitatolewa kwa wanafunzi 93,295 wanaoendelea na masomo kwa mwaka 2017/2018.
“Tayari Serikali imeshatoa fedha hizo na lengo la Bodi ni kuhakikisha zinafika vyuoni kabla ya kufunguliwa kwa vyuo ili kuwaondolea wanafunzi usumbufu,” amesema.
Bodi imewasihi waombaji wa mikopo kuwa na subira wakati ikiendelea kukamilisha maandalizi ya orodha zinazofuata za wanafunzi waliopata mikopo.
Kwa
Amna watasoma ila hawatapata mkopo, kam wanaweza kujlpiwa degree wanasoma tu
Kwa ambao wame kosa mkopo wakaomba tena majibu lini
 
Msaada please kuhusu diploma wanaomba mkopo kuna kipengere hiki cha awards verification mwenye ufahamu anisaidie
 
Kwa mtu aliyemaliza form six kupitia private candidate(PC) atapata mkopo?
 
msaada nimefungua account tayari nahitaji kulipia
baada ya kufungua unacho takiwa kukifanya ni kuingia kupitia account yako (log in) utakutana na hatua ya kwanza ambayo ni kulipia pamoja na ma hatua zote za ulipaji asante!
 
baada ya kufungua unacho takiwa kukifanya ni kuingia kupitia account yako (log in) utakutana na hatua ya kwanza ambayo ni kulipia pamoja na ma hatua zote za ulipaji asante!
nimelipia lakini bado inanionesha kama cjalipia inachukua mda gani kufynguka
 
WAKALA WA UNLIMITED DATA
Ndugu ,uwapo wakala utaweza kuuza packages (unlimited data&bandwidth) Kwa watu na kujipatia faida kubwa saana .
Kuwa wakala ni sh.40,000.tu
Data hi ni Kwa mitandao yote dunian,..utaweza kuingiza kipato cha chini sana kila siku sh.31,000.
Kwa kusajiliwa papopapo utaanza kazi
Kwa Maelezo zadi

Nipigie au WhatsApp sasa hivi 0621 072 026
 
Msaada please kuhusu diploma wanaomba mkopo kuna kipengere hiki cha awards verification mwenye ufahamu anisaidie
Nenda tovuti ya nacte, uende kwenye awards verification kuna process. Ila utalipia 10000 online
 
Back
Top Bottom