Special thread: Busara za wazee (mkusanyiko wa busara mbalimbali )

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
19,331
14,257
Wapendwa wana JF hbr za asubuhi...!!!!,nianze kwanza kumshukuru MUNGU mwingi wa rehema na neema aliyetuamsha salama na kutujalia kuiona siku hii ya leo tukiwa tu bukheri wa afya,kwa wale wenzetu wanao umwa tuwaombee kwa Mungu ili awape uponyaji,na kwa ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki,Mwenyezi Mungu awasamehe mapungufu yao na kuwalaza mahali pema peponi.Uzi wetu unahusu busara mbalimbali ambazo tukiziishi vizuri tutakuwa na maisha mema mbele ya Mungu wetu na binadamu wenzetu,Ninawaomba moderators muupe hadhi ya special thread kama nilivyoandika hapo juu kwenye kichwa cha habari kwasababu zitamsaidia kila mmoja wetu kuishi vema.

1. Mkumbuke muumba wako siku unazoishi duniani,wala usiseme "mimi sina muda,niko bize!!",kumbuka yeye ndiye akupaye pumzi na afya vinavyokupa uwezo wa kufanya shughuli zako na kujiona uko bize.Hivyo usijiweke mbali nae.

2. Waheshimu binadamu wenzako,usimdharau yeyote,Mungu mwenyewe amewathamini hadi akawaumba na kuwaweka duniani,wewe ni nani uwadharau?,

3. Saidia wahitaji kadiri ya vile ulivyojaliwa na Mungu na nafasi yako,kuna baraka nyingi zimejificha ktk tendo hili ambapo wengi hawajui.

4. Kuwa mnyenyekevu kwa Mungu na kwa wakubwa wako,Unyenyekevu unalipa,ndio kisa waswahili walituasa wakasema "Kiburi si maungwana",makinika sana hapa.

5. Uwapo kijana mwenye afya njema na nguvu nyingi kamwe usiwadharau wazee,kwani hata wewe utafika huko ikiwa utaendelea kuishi;uzee ni baraka.Tuwaheshimu,tuwapende na tuwasaidie wazee wetu.

6. Ukipata fursa ya kuaminiwa na watu hata kupata wadhifa au kazi fulani jitahidi uifanye kwa uaminifu ili uhitajike,siku usipokuwepo watu waone kuna pengo lako,hivyo jibidiishe kutimiza
wajibu wako mahali pako pa kazi,usikae tu km sanamu pasipokuwa na mchango wowote ule.

7. Ukiwa na cheo au mamlaka fulani au fedha kamwe usiwanyanyase watu wanyonge kwa kutumia uwezo wako,maana ole wako wanyonge hao wakimlilia Mungu,hakika atakuadhibu vikali na kukunyang'anya ulichonacho na kumpa mwingine.Cheo,pesa tunapewa na Mungu ili kuwasaidia watu wengine,wewe ni mfereji tu wa kupitishia neema za Mungu kwa watu wake.

8.Katika maisha usipende kulaumu laumu sana kwa kila kitu na kila wakati,mtu mlalamikaji sana huwa hakui kiakili,hata km wewe ni mzee wa miaka 80 kwa lawama zako unakuwa sawa na mtoto mdogo kiakili.Kifupi huwezi kukua kiakili maana unaweza kulalamika hata kwa mambo yaliyo ktk uwezo wako mwenyewe.

9.Usimwamini kila mtu,vijana wa sasa wanasema "Sura sio roho",hivyo ishi na watu kwa tahadhari".

10.Ukiwa baba wa familia timiza wajibu wa ubaba wa familia ipasavyo,usiwe mwanaume suruali,hali kadhalika ukiwa mwanamke timiza wajibu wako km mama wa familia,kinyume na hapo utamlaumu mumeo kumbe kosa lipo kwako mwenyewe.

11.Usipende kufurahia shida na matatizo ya wenzio,kumbuka usemi usemao kulia kupokezana.Siku yatakapokupata na wewe utakosa mtu wa kukufariji na kukuisaidia.

12.Achana na tabia ya kuwasemasema watu vibaya,hiyo ni dalili ya kushindwa maisha.Usipoteze muda kujadili mambo yasiyokuhusu maana hakuna mshahara wa umbea.

13.Jiepushe na tabia zisizofaa,km vile ulevi,wizi,uzinzi,uongo,uchonganishi,nk. kwani mwisho wa ubaya ni aibu.

14.Usipende dezo,jishughulishe kutafuta riziki yako,usipende sana kuombaomba ilihali Mungu amekupa nguvu,afya njema na akili.Waswahili wanasema "Cha mtu mavi" na "Nguo ya kuazima haisitiri matako".

15.Acha kuamini sana ktk ushirikina,ni kweli ushirikina upo lkn usiupe attention sana kwani hudhoofisha uwezo wa kufikiri na kufanya maendeleo.

16.Usiamini ktk imani za kuomba tu! kisha unapewa.Mtu asikudanganye kwamba unaweza kupata gari,nyumba nzuri,pesa kwa kuomba Mungu tu!!,jishughulishe ndipo umwombe Mungu,naye atakupa.Kumbuka hata "mana"ilikoma kushuka wana wa Israeli walipofika nchi ya ahadi yenye ardhi nzuri na rutuba ikabidi waanze kulima ili kupata riziki yao.Tafadhari usimjaribu Mungu kwa kumuomba mafanikio pasipo wewe kujishughulisha.Makinika sana mwanangu.

17.Waheshimu viongozi wako wa Dini na Serikali maana wanahangaika kwaajili yako,hata kama wewe huoni mchango wao lkn waheshimu.Ukitaka kujua uzito wa kazi hiyo ingia humo .

18.Jizoeze kuwa msikilizaji zaidi kuliko kuwa msemaji sana,kumbuka Mungu alitupatia mdomo mmoja na masikio mawili,ili tusikilize zaidi kuliko kuongea.

19.Jibidiishe kutafuta maarifa,yatakusaidia maishani,wazungu wanasema "KNOWLEDGE IS POWER".

20.Usitafute mafanikio ya kisiasa,kiuchumi,n.k.kwa kuwadhuru binadamu wenzako,haitakusaidia.Unaweza tu kufanikiwa bila kuwadhuru binadamu wenzako.

21.Kuwa mtetezi wa uhai kwa nguvu zako zote,kadiri unavyoweza,kamwe usifurahie wala kushabikia mauaji kwa sababu yeyote ile.Kumbuka mwenye mamlaka ya kuuondoa uhai ni

Mungu mwenyewe maana ndie aliyemuasisi wa uhai;Kamwe usichukue nafasi ya Mungu kuuondoa uhai wa binadamu mwenzako.

22.Usimfanyie ubaya binadamu mwenzako na ukadhani utabaki salama,kumbuka dunia ni duara,mambo hubadilika.

Ndugu zangu naomba niishie hapa,najua zipo busara nyingi sana,naomba kila mwenye busara aiweke hapa ili itufae sote.
 
Back
Top Bottom