Special Intro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Special Intro

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Neemah, Mar 1, 2009.

 1. N

  Neemah Member

  #1
  Mar 1, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi ndimi Invisible, katu hutoniona,
  Hata ukipiga chabo, unajisumbua kijana,
  Wala hakuna kizibo, tena kweupee, mchana!
  Nahodha wa jahazi hili, lenye abiria wengi.

  Nahodha wa hili jahazi, wapo wengi abiria,
  Kuliendesha ni kazi, lakini twavumilia,
  Ufisadi aina ya wizi, huo twaukaripia,
  Hima tushirikiane, kulikokota jahazi.


  Na mimi ni Painkiller, kiboko ya maumivu,
  Siwaogopi wasela, hata wale wapumbavu,
  Ukileta zako hila, nakufungia laivuu!!
  Utakaa tu jela, ili uwe msikivu.


  Mimi chini sikai, sijatulia kitako,
  Najaribu ku-survey, mara huku, mara huko,
  Vipi, bado hunijui, mzee wa mihangaiko?
  Ni cheo cha kimasai, hebu kuna kichwa chako.


  Jamani mimi Farida, sauti yangu ni ndogo,
  Sijui ni hizi soda, au ni hii mihogo!
  Bado ninavuta muda, vumilieni kidogo,
  Subira ina faida, nitakuja kwa mikogo.


  Unasema humjui, kijana mwenye bidii?
  Ndimi mimi buibui, tovuti naitalii,
  Sibagui, sichagui, kila fani naitii,
  Before saying bye bye, mimi ndiye SteveD.


  Mimi mzee wa shamba, nadhani wanitambua,
  Sikwambii nakufumba, kama mjuzi tambua,
  Mashairi nayaimba, habari nazichambua,
  Je, nimekufunga kamba, au umeshafumbua?


  Maji ukiyavulia, huna budi kuyaoga,
  Ukisita nitakumwagia, bila kuwa na uwoga,
  Lakini ukitulia, sitakuvalia njuga,
  Labda umenisikia, mimi ndiye yule Ogah.

  To be continued ...
  (wengine endelezeni)
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Mar 1, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Mimi ndio shy sina shari
   
Loading...