Utunzaji na Uhifadhi Endelevu wa Mazingira na Maliasili Tanzania

Conservator

Member
Jun 26, 2017
79
110
WanaJF.

Uchumi wa nchi yetu na maisha ya Watanzania yanategemea kwa kiasi kikubwa maliasili tulizonazo kama vile ardhi, maji, misitu na hewa safi.

Uwepo wa maliasili hizi kwa mahitaji yetu ya sasa na ya vizazi vijavyo hutegemea namna tunavyozingatia uhifadhi wake na matumizi endelevu. Changamoto tuliyonayo sasa ni uelewa mdogo wa jamii yetu kuhusu hifadhi ya mazingira na uwepo wa mabadiliko ya tabia ya nchi.

Athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira ni pamoja na upungufu wa mvua, kupungua kwa misitu na uoto wa asili, kupungua kwa vyanzo vya maji, uchafuzi wa hali ya hewa na kuongezeka kwa umaskini (Mh.January Makamba, Waziri wa Mazingira Alipokuwa Akiwasilisha Bungeni Makadilirio ya Bajeti ya Wizara Yake kwa Mwaka 2017/2018 )

Naam! Kwa muda mrefu kumekuwa na ripoti mbalimbali zikionyesha au kuashiria uwepo wa uharibifu mkubwa wa mazingira na matumizi yasiyoendelevu ya maliasili zetu.

Ripoti maalum ya tathmini ya rasilimali za misitu ya mwaka 2015 (National Forestry Resources Monitoring and Assessment Report,2015) inaonyesha kwamba uhitaji wa miti (demand) kwa ajili ya matumizi mbalimbali nchini kama kuni na mkaa unazidi kiwango cha miti inayoweza kuvunwa katika kiwango endelevu ( it exceed amount of woods that can be harvest at sustanaible level) kwa kwa mwaka uhitaji wa miti ni mita za ujazo miliomi 62.3 huku miti (au kuni) idadi ya miti inafaa kuvunwa kwa kiwango endelevu ikiwa ni mita za ujazo milioni 42.8 tu.

Hii Inamaanishi Nini?
Hii inaashiria kwamba, kuna upungufu wa mita za ujazo milioni 19.5 za miti (deficit) kwa ajili ya matumizi. Na Je watu wanatumia mbinu gani kutimiza hitaji hili?

Jibu rahisi ni kwamba watu huvamia misitu ya hifadhi, au kukata miti kupita kiwango kwenye misitu ambayo haipo kwenye hifadhi za taifa au halmashauri. Na huu ndio msingi mkubwa wa uharibifu wa misitu, vyanzo vya maji na matatizo mengine ndani ya hifadhi za misitu.

Je, Kwa Upande wa Miti au Misitu kwa Ujumla Nini Kinapelekea Uharibifu Mkubwa. Je ni Upande wa Matumizi (Consumption or Demand Side) kuwa tegemezi katika miti au Ni Upande wa Upatikanaji wa Miti ya Kutosha kwa Ajili ya Matumizi Mbalimbali? Na Je nini Kifanyike, Tupande Miti Zaidi ili Kuziba Gap (deficit iliyopo) au Tutafute Mbadala wa Matumizi ya Kuni, Mkaa n.k?

Hapo nimegusia kwa uchache upande wa rasilimali za mistu tu. Swala la Mazingira ni Pana Sana. Hivi karibuni tumemuona waziri wa Mazingira Mh.January akizungumzia uharibifu wa eneo kubwa la bonde la Mto Ruaha Mkuu (Great Ruaha) uliopelekea maji kukauka na kuhatarisha maisha ya viumbe wanaishi katika eneo hili.

Tumeona kikiundwa kikosi kazi (Task Force) ambacho pamoja na mambo mengine kimebaini uwepo wa uchepuaji mkubwa wa maji ya mto Ruaha Mkuu uliofanywa na watu binafsi.

Aidha Ngorongoro kumeripotiwa changamoto kubwa ya kupotea uoto wa asili ndani ya crator uliosababisha na mimea vamizi (allien invasive species) hali ambayo inatishia uhai wa viumbe wanaishi kwa kutegemea ikolojia hii ya ajabu duniani.

Aidha watu kujenga mahoteli makubwa ndani au kando kando ya mbuga na kutumia maji yale yale ambayo yanategemewa na wanyama. Je Nini Msingi wa Matatizo Haya?

Kuna uharibifu mkubwa wa maeneo oevu ambayo kwa kiasi kikubwa hutumika kwa shughuri za kilimo. Tumeshuhudia watu wanatiririsha maji machafu na kutupa taka ovyo bila kutibu wala kufuata taratibu zilizopo. Watu wanalima kando kando ya mito.

Je, Nini Kifanyike? Je Hatua Zilizokwisha kama Kupiga Faini Zinatosha? Wapi Pamelegea, Ukosefu wa Elimu? Sheria au Sera Mbovu? au Upande wa Utekelezaji wa Sheria?

Swala la Mabadiliko ya Tabia Nchi (Climate Change) linazungumzwa sana. Je Linazungumzwa Zaidi Kuliko Kuwekwa Kwenye Vitendo? Ukiangalia Tafti Nyingi za Idara za Kilimo, Ardhi, Mazingira,Misitu Kwenye Vyuo Vyetu Vikuu Zinahusu Climate Change. Kuna Maandiko ya Kutosha Kuhusu Kuhimili (Adapting) na Kupunguza (Mitigating) Athari za Madiliko ya Tabia Nchi.

Je Tafiti Zimepuuzwa? Wahanga Wakubwa (Vulnerable Group) ni Wakulima Wadogo Wadogo Wanaishi Vijijini, Je Wameelimishwa vya Kutosha Juu ya Kilimo Kinachoweza Kuhimili na Kupunguza Athari za Mabadiliko ya Tabia Nchi? Climate-Smart Agriculture?

Je Wakulima Wameandaliwa Mazingira Bora ya Kufanya Kilimo Endelevu? Mfano Kilimo Hai? Je Wakulima Wanatambua Umuhimu wa Kuboresha Ardhi Kabla ya Kufikiria Mavuno? Wanasema Feed the Soil and Soil Shall Feed the World.

After all, what does climate change means to a rural smallholder farmer? Hivi Karibuni Kumekuwa na Swala la Usalama wa Chakula (Food Security) Huku Mgogoro Mkubwa Ukiwa ni Ama Tanzania Kuna Njaa au Ukosefu wa Chakula cha Kutosha. Kwanini Tufike Huko? Nini Kifanyike?

Vipi Hali za Hifadhi Wanyama Pori Kwenye Mbuga za Taifa, Mapori Tengefu na Hifadhi Zingine? Swala la Baadhi ya Jamii Kuvamia na Kuanzisha Makazi Kwenye Hifadhi za Taifa. Ni Kifanyike?

Tunaelekea Kwenye Tanzania ya Viwanda, Kwa Ujumla, Ni Kwa Kiasi Gani Sheria, Sera na Mipango Mbalimbali ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa Zimekuwa Chanzo cha Uharibifu wa Mazingira. Vipi Upande wa Budget za Wizara Husika, ni Kwa Kiasi Gani Zina address matatizo yaliyopo?

Na Kutunza au Kuhifadhi Mazingira na Maliasili Zetu ni Swala la KIZALENDO. Je Watanzania Tuna Uzalendo wa Kutosha Kujitolea Kwa Ajili ya Mazingira Yetu? Je Kuna Utashi wa Kisiasa wa Kutunza Mazingira?

Kimataifa: Tumeona Rais wa Marekani Donald Trump Akijitoa Kwenye Mkataba wa Paris kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi. Je Hatua Hii Itaathiri Vipi Harakati za Kupambana na Mabadiliko ya Tabia ya Tanzania? Na Je Tuna Uelewa wa Kutosha KuhusuFursa Mbalimbali za Kimataifa za Kutunza Mazingira? Tunazungumzia Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Goals), Je Tuna Mwenendo Mzuei ya Kuyafikia?

Mwisho, KATIBA. Je Katiba Yetu Inatamka Wazi Kabisa Kwamba "KILA MTANZANIA ANA HAKI YA KUISHI KATIKA MAZINGIRA SAFI NA SALAMA? (Rejea Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 )

Karibuni Sana Wakuu.

1586505116112.png

===========

Mazingira nini?
Mazingira ni vitu vyote vinavyotuzunguka vyenye uhai na visivyo na uhai.
Vitu vyenye uhai ni pamoja na

  • Wanyama
  • mimea
Vitu visivyo na uhai ni
  • Hewa
  • Ardhi
  • Maji.
Mazingira yanahusisha pia vitu vyote vinavyosaidia kuendelea kuwepo kwa maisha ya mwanadamu na viumbe wengine . Hivyo basi maisha a viumbe hai wa kizazi kijachokinategemea uwepo wa mahusiano mazuri kati ya watu na mazingira.

Michango ya wadau

Tupo pamoja sana mleta mada.

Ukisoma historia ya dini mbalimbali ulimwenguni utakutana na dini moja ya miaka mingi sana (jina limenitoka) huko Asia, Marekani ya Kusini nk.

Waumini wa dini hii walihimizwa kutokukata miti kabisa, achilia mbali kuchoma misitu.Hawakukata miti kamwe ila tu kwa mahitaji ya msingi kama kujenga nk.

Kisayansi, hawakujua madhara haswa ya kukata miti ni yepi ila tu wao hawakukata miti.Walitunza mazingira na mazingira yaliwatunza.

Nchini Kenya, mwanamama/mwanaharakati prof wangari muta maathai alitunza mazingira na mazingira yakawatunza watu wa Kenya.

Akaanzisha green belt movement, hii yote kuendeleza harakati za utunzaji mazingira na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa mno japo alikutana na changamoto za hapa na pale ila alipiga moyo konde.

Mwaka 2004 akawa mwanamke wa kwanza Afrika kutunukiwa tuzo ya amani ya nobel kwa vuguvugu hili la mkanda wa kijani.Kinachosikitisha ni kwamba wanawake wa Kenya, Africa hawamjui Maathai na wala hawamtambui kabisa (so sad).

Miti ilisaidia mengi katika ardhi ya Kenya.Alisaidia kutokuchujuka kwa udongo (mmomonyoko wa ardhi), miti ilisaidia mamilioni ya kina mama kupata nishati ya kuni kwa ajili ya kupikia nk, miti ilitunza vyanzo mbalimbali vya maji na mengine mengi.

Tutunze mazingira, nayo itutunze.
----
Ndugu Conservator nakupongeza kwa kufikiria kumshika mkono yatima mazingira angalau naye apate mtetezi japokuwa sina uhakika kama atapata kweli!

Nianze kwa kusema suala LA mazingira ni mtambuka lakini u mtambuka huu umebakia kwenye maandishi tu si kwa vitendo.

Ukiweka utetezi wa mazingira katika vitendo ni ngumu kutokana na kwamba hifadhi ya mazingira ni kikwazo katika uchumi, ndio maana hata Trump kajitoa kwenye Paris accord ili kulinda uchumi wa viwanda.

Lakini si Trump tu hata Tanzania tuna rais asiyejari mazingira, kama tulivomsikia hivi karibuni kwa nyakati mbali mbali akisema "mwekezaji atakayeona ardhi inamfaa kujenga kiwanda ajenge tu halafu aone nani atamnyima kibali" hii ina maana kwamba tathimini ya athari za mazingira haitafanywa mahala kiwanda kinapojengwa Ila kibali kitolewe kwa amri ya rais tena kiwanda kikiwa tayari kinafanya kazi.

Lakini pia tumemsikia akisema mradi wa umeme wa rufiji falls lazima uendelee pamoja na kwamba unapingwa na wataalamu wa mazingira, ukiacha hayo kuna hotel nyingi za kitalii zinazojengwa mbugani na kupelekea athari za mazingira na ecology.

Suala kubwa ni mgongano wa maslahi ya kiuchumi na maslahi ya hifadhi ya mazingira.

Pili ni kwakuwa athari za mazingira social impact ni kwa mtu wa hali ya chini zaidi kuliko wa hali ya juu hivyo watunga sera na watoa maamuzi hawaguswi kwa kiasi kikubwa na athari hizi.

Kutokana na hivyo basi, hata kama kila sekta iwe ya Mali asili, iwe kilimo na uvuvi, iwe ni nishati na madini nk, na pia sheria kuu ya mazingira ya mwaka 2004 haziwezi kufanya kazi bila kuwepo utashi wa watunga sera na watoa maamuzi.

Mwisho kabisa, huwa nafikiria kuwa njia rahisi ya kulinda mazingira yetu ni kuwa mwana harakati maana kwa kufanya hivi utalazimisha hoja kuingia masikioni kwa wasiopenda kusikia.
----
Watunga sera wetu hawajawahi kusaidia kwenye uhifadhi wa mazingira. Wengi wana personal interests kwenye maeneo ya hifadhi na mara zote hupingana na mapendekezo ya wataalamu.

Bungeni Prof Tibaijuka ambaye ashawahi kuwa Executive director wa UN Habitat, Waziri wa ardhi nyumba na makazi ametoa mchango wake akisema haiwezekani 28% ya ardhi ya Tanzania iendelee kuwa hifadhi.

Huyu ni professor amekuwa msimamizi, mtunga sera na mdau mkubwa kwenye masuala ya matumizi ya ardhi kwa muda mrefu anakuja na ushauri kama huu wale wa KKK watatoa ushauri gani?

Tangu lini solution ya watu kuongezeka iwe kuwagawia maeneo ya hifadhi? Prof wa aina gani huyu? Wakati akiwa waziri wa ardhi alifanya nini kuhakikisha matumizi bora na endelevu ya ardhi?

Ama hakuliona hili? Hapo alipo anajua kabisa hifadhi zote zikigawiwa bado hazitatosha, sio kwa ufugaji wa kuhama hama na makundi makubwa ya mifugo.
----
Kwanza kabisa napenda kuwaelezea kidogo hawa jamaa. Friends of Usambara ni taasisi iliopo katika milima ya Usambara Magharibi. Taasisi hii imeanza kufanya shughuli za utalii tamaduni kwa malengo ya kutunza mazingira na utamaduni mwishoni mwa miaka ya tisini hadi hivi sasa.

Katika kipindi chote hiki tumeweza kuona manufaa makubwa ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya watalii katika milima hii kulikopelekea ukuwaji wa uchumi pamoja na vijana wengi kupata ajira.

Katika miaka ya hivi karibuni hadi leo hii tumeweza kuona walivyojikita katika kutunza mazingira wakiwa na lengo la kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya milima ikiwemo vilele vya milima, mashamba ya raia na pia kwenye misitu ya asili iliongua kutokana na sababu mbalimbali. Mpaka sasa wanasema wameshapanda miche zaidi ya milioni saba.

Kilichonivutia zaidi ni pamoja na ajira walioitoa kwa vijana zaidi ya 400 wanaofanya kazi katika shughuli nzima ya kutunza mazingira.

Nimepata kutembelea moja ya vitalu vyao vilivyoko Lushoto mjini na kujionea.

Hizi ni baadhi ya picha.View attachment 837615View attachment 837616View attachment 837617View attachment 837621View attachment 837624View attachment 837627
----
Dunia ni sehemu nzuri ya kuishi inakadiliwa imekuwepo kwa takribani miaka 4.543 billioni, dunia ni nyumbani kwetu sisi na viumbe hai.

Kupitia dunia tunayo mazingira yenye utofauti na aina mbalimbali, mazingira haya yamekuwa yenye umuhimu kwetu na viumbe hai wengine.

Licha ya kuwa tunatambua umuhimu wa mazingira yetu, pengine unaweza shangazwa na dondoo hizi;-

|- Kila siku takribani miti 27,000 inakatwa duniani kwa ajili ya kutengeneza karatasi laini za chooni maarufu kama toilet paper

|- Kama tukitumia tena (Recycle) karatasi zinazotumika kuchapa gazeti la New York Times pekee kila siku, tunaweza okoa miti zaidi ya 75,000

|- Kila unapotupa chupa au vifungashio vya plastiki baharini unaua viumbe wa baharini milioni moja kwa mwaka.

|- Chupa ya kioo (Glass bottle) unayotumia inachukua zaidi ya miaka 4,000 kuoza na kupukitika

|- Kwa wastani inakatwa zaidi ya miti 1,000 kwa kila dakika, maana yake kila ndani ya saa moja tunakata miti zaidi ya 60,000. Ukitafuta Google The World Counts, utajionea maajabu ya idadi ya miti inayokatwa. Mpaka tarehe 15 March 2020 saa 12:43 jioni miti 5,729,738.49 ilikuwa imekatwa.

View attachment 1389568

Kila mtu anatumia (Consume) vitu kadhaa iwe chakula, vinywaji, kuendesha vyombo vya moto na viburudisho tofauti na kati yetu kunawapenzi wakubwa wa chocolate. Je umewahi fikiria kuhusu madhara ya hivi vitu tunavyotumia hasa katika mazingira yetu?

|- Biashara ya mavazi ni kichocheo cha pili cha uchafuzi wa mazingira tunayoishi baada ya mafuta. Viwanda vya pamba vinatumia dawa za kuulia wadudu (Pesticides) kuliko zao lolote na zaidi ya lita za maji 20,000 zinatumika kutengeneza tisheti moja na 'pair' moja ya suruali ya pamba. Fikiria hapo nyumbani una tisheti na jinzi ngapi zenye 'material' ya pamba.

|- Magari ni chanzo kikuu cha uchafuzi wa hewa hasa katika miji na majiji, kuanzia mwaka 2010 mpaka 2035 'kwa kadri' zaidi ya magari bilioni mbili yatakuwa yamezalishwa (Manufactured). Meli moja ya mizigo inasababisha uchafuzi wa hewa zaidi ya magari milioni 50, hapo hatujataja ndege.

|- Inachukua zaidi ya lita 24,000 za maji kutengeneza kilo moja ya chocolate na lita 21,000 za maji kutengeneza kilo moja ya kahawa. Kila tunachokunywa au kula kina madhara yake kwa kutugusa ama laah! (Directly or Indirectly). Nusu ya chakula kinapotea kila siku duniani kama taka, mpaka kufikia mwaka 2050 dunia itakumbwa na uhaba mkubwa wa chakula kama mifumo ya matumizi ya vyakula isipo boreshwa. Nunua au pika chakula kinachokidhi haja yako, badala ya kukitupa kumbuka watu wanakufa au kulala pasipo kula.

View attachment 1389573

Unatambua tangu dunia kuumbwa kiasi cha maji ni kilekile ila idadi ya watu ndiyo inazidi kuongezeka. Dunia imeundwa na asilimia 75 ya maji na bahari imechukua kiasi kikubwa.

Kama tusipotunza mazingira sasa kuna hatari ya kiwango cha maji kuzidi kupungua hali itakayopelekea dunia kukumbwa na ukame na kutoweka kwa baadhi ya viumbe.

Kumbuka mpaka sasa tayari dunia imekwisha poteza aina mbalimbali za viumbe hai na mimea, takribani aina 600 ya mimea na 300 ya wanyama, ndege na wadudu. Tuliwapoteza Baiji, Dodo, Great auk, Stellar Sea Cow, Thylacine, Quagga na wengine.

Utupaji taka hovyo umekuwa tamaduni sasa, unaruka vocha unakanyaga diaper huku ukitingwa na chupa/vifungashio vya plastiki. Ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa ni kama mafunzo ya stadi za kazi sasa.

View attachment 1389626

| Suluhisho ya haya yote ni nini?

Ni kuwajibika katika kutunza na kuendeleza vyanzo vya maji, kupanda miti, kutumia taka kutengeneza bidhaa na kusitisha bunifu zilizoshindwa kujisimamia katika utunzaji wa mazingira (Plastiki).

Dunia hivi sasa inashuhudia jitihada na kujitoa kwa mashirika, taasisi na kampuni mbalimbali katika kutunza mazingira. Tutaweza kuona Parley for Oceans wakitumia plastiki katika utengenezaji wa mavazi kwa ushrikiano na adidas, BALR, Puma na timu mbalimbali za michezo pia tunaweza kuona Heartfeldt Foundation ikijitoa katika katika kuchangia vifaa wezeshi katika kupambana na uchafuzi wa mazingira.

Ni jukumu letu sote hivi sasa kutumia muda wa mapumziko katika upandaji miti, kusafisha mazingira na kubuni mbinu mpya ya kuondokana na uharamia wa kuiharibu dunia. #KeshoTutachelewa kama tusipochukua hatua madhubuti.

#WakatiNiSasa #IshiKijanja #ExperienceTheChange
 
Sababu kuu ya ukataji miti ni kutengeneza mkaa na kuni hivyo basi ili kureduse demand ya mkaa na kuni gesi na umeme vingepunguzwa bei ili watu wengi waweze kutumia kama alternative energy though nowdays nyumba nyingi hasa mijini tunatumia gesi.
 
Swala la mbadala wa kuni na mkaa likipata ufumbuzi wa kudumu laweza kusaidia sana kuokoa misitu yetu.
 
Tupo pamoja sana mleta mada.

Ukisoma historia ya dini mbalimbali ulimwenguni utakutana na dini moja ya miaka mingi sana (jina limenitoka) huko Asia, Marekani ya Kusini nk.

Waumini wa dini hii walihimizwa kutokukata miti kabisa, achilia mbali kuchoma misitu.Hawakukata miti kamwe ila tu kwa mahitaji ya msingi kama kujenga nk.

Kisayansi, hawakujua madhara haswa ya kukata miti ni yepi ila tu wao hawakukata miti.Walitunza mazingira na mazingira yaliwatunza.

Nchini Kenya, mwanamama/mwanaharakati prof wangari muta maathai alitunza mazingira na mazingira yakawatunza watu wa Kenya.

Akaanzisha green belt movement, hii yote kuendeleza harakati za utunzaji mazingira na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa mno japo alikutana na changamoto za hapa na pale ila alipiga moyo konde.

Mwaka 2004 akawa mwanamke wa kwanza Afrika kutunukiwa tuzo ya amani ya nobel kwa vuguvugu hili la mkanda wa kijani.Kinachosikitisha ni kwamba wanawake wa Kenya, Africa hawamjui Maathai na wala hawamtambui kabisa (so sad).

Miti ilisaidia mengi katika ardhi ya Kenya.Alisaidia kutokuchujuka kwa udongo (mmomonyoko wa ardhi), miti ilisaidia mamilioni ya kina mama kupata nishati ya kuni kwa ajili ya kupikia nk, miti ilitunza vyanzo mbalimbali vya maji na mengine mengi.

Tutunze mazingira, nayo itutunze.
 
Watu hawana uzalendo kwenye uhifadhi kwa sababu hawaoni direct benefits za kutunza mazingira na wanyama pori. Serikali na wadau wengine kwa muda mrefu hawakushirikisha jamii kwenye kupanga matumizi endelevu ya ardhi.
 
Mkuu hii point nimeilewa sana. Ni swala ambalo halikutuliwa mkazo sana.

Hata ukiangalia mpango wa usimamizi shirikishi wa misitu (participatory forest management) bado unatekelezwa kwenye maeneo macache
 
Tupo pamoja sana Mleta Mada.

Ukisoma Historia ya Dini mbalimbali ulimwenguni utakutana na Dini moja ya miaka mingi sana (Jina limenitoka) huko Asia, Marikani ya kusini nk.

Waumini wa Dini hii walihimizwa kutokukata miti kabisa, achilia mbali kuchoma misitu.Hawakukata miti kamwe ila tu kwa mahitaji ya Msingi kama kujenga nk.

Kisayansi, hawakujua madhara haswa ya kukata miti ni yepi ila tu wao hawakukata Miti.Walitunza mazingira na Mazingira yaliwatunza.

Nchini Kenya, Mwanamama/Mwanaharakati Prof Wangari Muta Maathai alitunza mazingira na Mazingira yakawatunza watu wa Kenya.

Akaanzisha Green Belt Movement, hii yote kuendeleza harakati za utunzaji Mazingira na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa mno japo alikutana na changamoto za hapa na pale ila alipiga moyo konde.

Mwaka 2004 akawa mwanamke wa kwanza Afrika kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa vuguvugu hili la mkanda wa kijani.Kinachosikitisha ni kwamba wanawake wa Kenya, Africa hawamjui Maathai na wala hawamtambui kabisa (So sad).

Miti ilisaidia mengi katika ardhi ya kenya.Alisaidia kutokuchujuka kwa udongo (Mmomonyoko wa ardhi), miti ilisaidia mamilioni ya kina mama kupata nishati ya kuni kwa ajili ya kupikia nk, Miti ilitunza vyanzo mbalimbali vya maji na mengine mengi.

Tutunze Mazingira, Nayo itutunze.

Mkuu asante sana. Umeeleza vizuri sana. Jitiada za mtu mmoja mmoja zinasaidia jamii nzima, kizazi cha sasa na cha baadae
 
Ndugu Conservator nakupongeza kwa kufikiria kumshika mkono yatima mazingira angalau naye apate mtetezi japokuwa sina uhakika kama atapata kweli!

Nianze kwa kusema suala LA mazingira ni mtambuka lakini u mtambuka huu umebakia kwenye maandishi tu si kwa vitendo.

Ukiweka utetezi wa mazingira katika vitendo ni ngumu kutokana na kwamba hifadhi ya mazingira ni kikwazo katika uchumi, ndio maana hata Trump kajitoa kwenye Paris accord ili kulinda uchumi wa viwanda.

Lakini si Trump tu hata Tanzania tuna rais asiyejari mazingira, kama tulivomsikia hivi karibuni kwa nyakati mbali mbali akisema "mwekezaji atakayeona ardhi inamfaa kujenga kiwanda ajenge tu halafu aone nani atamnyima kibali" hii ina maana kwamba tathimini ya athari za mazingira haitafanywa mahala kiwanda kinapojengwa Ila kibali kitolewe kwa amri ya rais tena kiwanda kikiwa tayari kinafanya kazi.

Lakini pia tumemsikia akisema mradi wa umeme wa rufiji falls lazima uendelee pamoja na kwamba unapingwa na wataalamu wa mazingira, ukiacha hayo kuna hotel nyingi za kitalii zinazojengwa mbugani na kupelekea athari za mazingira na ecology.

Suala kubwa ni mgongano wa maslahi ya kiuchumi na maslahi ya hifadhi ya mazingira.

Pili ni kwakuwa athari za mazingira social impact ni kwa mtu wa hali ya chini zaidi kuliko wa hali ya juu hivyo watunga sera na watoa maamuzi hawaguswi kwa kiasi kikubwa na athari hizi.

Kutokana na hivyo basi, hata kama kila sekta iwe ya Mali asili, iwe kilimo na uvuvi, iwe ni nishati na madini nk, na pia sheria kuu ya mazingira ya mwaka 2004 haziwezi kufanya kazi bila kuwepo utashi wa watunga sera na watoa maamuzi.

Mwisho kabisa, huwa nafikiria kuwa njia rahisi ya kulinda mazingira yetu ni kuwa mwana harakati maana kwa kufanya hivi utalazimisha hoja kuingia masikioni kwa wasiopenda kusikia.
 
Ukataji miti hovyo ni hatari sana... Yaani tusipokua waangalifu nchi nzima hali itakua kama Dar es Salaam, hali ya hewa chafu sana...
Wengu wetu hatujajua umuhimu wa miti zaidi ya kupata kivuli na matunda.... Kuna haja ya elimu kuenezwa zaidi.
 
Watunga sera wetu hawajawahi kusaidia kwenye uhifadhi wa mazingira. Wengi wana personal interests kwenye maeneo ya hifadhi na mara zote hupingana na mapendekezo ya wataalamu.

Bungeni Prof Tibaijuka ambaye ashawahi kuwa Executive director wa UN Habitat, Waziri wa ardhi nyumba na makazi ametoa mchango wake akisema haiwezekani 28% ya ardhi ya Tanzania iendelee kuwa hifadhi.

Huyu ni professor amekuwa msimamizi, mtunga sera na mdau mkubwa kwenye masuala ya matumizi ya ardhi kwa muda mrefu anakuja na ushauri kama huu wale wa KKK watatoa ushauri gani?

Tangu lini solution ya watu kuongezeka iwe kuwagawia maeneo ya hifadhi? Prof wa aina gani huyu? Wakati akiwa waziri wa ardhi alifanya nini kuhakikisha matumizi bora na endelevu ya ardhi?

Ama hakuliona hili? Hapo alipo anajua kabisa hifadhi zote zikigawiwa bado hazitatosha, sio kwa ufugaji wa kuhama hama na makundi makubwa ya mifugo.

Suala kubwa ni mgongano wa maslahi ya kiuchumi na maslahi ya hifadhi ya mazingira.

Pili ni kwakuwa athari za mazingira social impact ni kwa mtu wa hali ya chini zaidi kuliko wa hali ya juu hivyo watunga sera na watoa maamuzi hawaguswi kwa kiasi kikubwa na athari hizi.

Kutokana na hivyo basi, hata kama kila sekta iwe ya Mali asili, iwe kilimo na uvuvi, iwe ni nishati na madini nk, na pia sheria kuu ya mazingira ya mwaka 2004 haziwezi kufanya kazi bila kuwepo utashi wa watunga sera na watoa maamuzi.

Mwisho kabisa, huwa nafikiria kuwa njia rahisi ya kulinda mazingira yetu ni kuwa mwana harakati maana kwa kufanya hivi utalazimisha hoja kuingia masikioni kwa wasiopenda kusikia.
 
Attachments

  • Tibaijuka bungeni.mp4
    2.5 MB · Views: 65
Ndugu Conservator nakupongeza kwa kufikiria kumshika mkono yatima mazingira angalau naye apate mtetezi japokuwa sina uhakika kama atapata kweli!

Nianze kwa kusema suala LA mazingira ni mtambuka lakini u mtambuka huu umebakia kwenye maandishi tu si kwa vitendo.

Ukiweka utetezi wa mazingira katika vitendo ni mgumu kutokana na kwamba hifadhi ya mazingira ni kikwazo katika uchumi, ndio maana hata trump kajitoa kwenye Paris accord ili kulinda uchumi wa viwanda.

Lakini si trump tu hata Tanzania tuna rais asiyejari mazingira, kama tulivomsikia hivi karibuni kwa nyakati mbali mbali akisema "mwekezaji atakayeona ardhi inamfaa kujenga kiwanda ajenge tu halafua aone nani atamnyima kibali" hii ina maana kwamba tathimini ya athari za mazingira haitafanywa mahala kiwanda kinapojengwa Ila kibali kitolewe kwa amri ya rais tena kiwanda kikiwa tayari kinafanya kazi.

Lakini pia tumemsikia akisema mradi wa umeme wa rufiji falls lazima uendelee pamoja na kwamba unapingwa na wataalamu wa mazingira, ukiacha hayo kuna hotel nyingi A kitalii zinazojengwa mbugani na kupelekea athari za mazingira na ecology.

Suala kubwa ni mgongano wa maslahi ya kiuchumi na maslahi ya hifadhi ya mazingira.
Pili ni kwakuwa athari za mazingira social impact ni kwa mtu wa hali ya chini zaidi kuliko wa hali ya juu hivyo watunga sera na watoa maamuzi hawaguswi kwa kiasi kikubwa na athari hizi.

Kutokana na hivyo basi, hata kama kila sekta iwe ya Mali asili, iwe kilimo na uvuvi, iwe ni nishati na madini nk, na pia sheria kuu ya mazingira ya mwaka 2004 haziwezi kufanya kazi bila kuwepo utashi wa watunga sera na watoa maamuzi.

Mwisho kabisa, huwa nafikiria kuwa njia rahisi ya kulinda mazingira yetu ni kuwa mwana harakati maana kwa kufanya hivi utalazimisha hoja kuingia masikioni kwa wasiopenda kusikia.

Aisee Mkuu. Kwakweli Nakushkuru sana.
Hakika tunahitaji wanaharakati watakaoweza kusimama mstari wa mbele kutetea mazingira.

Thank you, I'm real inspired.
 
Watunga sera wetu hawajawahi kusaidia kwenye uhifadhi wa mazingira. Wengi wana personal interests kwenye maeneo ya hifadhi na mara zote hupingana na mapendekezo ya wataalamu. Bungeni Prof Tibaijuka ambaye ashawahi kuwa Executive director wa UN Habitat, Waziri wa ardhi nyumba na makazi ametoa mchango wake akisema haiwezekani 28% ya ardhi ya Tanzania iendelee kuwa hifadhi. Huyu ni professor amekuwa msimamizi, mtunga sera na mdau mkubwa kwenye masuala ya matumizi ya ardhi kwa muda mrefu anakuja na ushauri kama huu wale wa KKK watatoa ushauri gani?

Tangu lini solution ya watu kuongezeka iwe kuwagawia maeneo ya hifadhi? Prof wa aina gani huyu? Wakati akiwa waziri wa ardhi alifanya nini kuhakikisha matumizi bora na endelevu ya ardhi? Ama hakuliona hili? Hapo alipo anajua kabisa hifadhi zote zikigawiwa bado hazitatosha, sio kwa ufugaji wa kuhama hama na makundi makubwa ya mifugo.

Kwakweli mkuu, mimi imefika mahali sina imani na kitu mtu alichosomea au kukifania kazi.. Harakati inaanzia ndani.

Imenisikitisha sana
 
Back
Top Bottom