Special for men: Mwanamke anahitaji yafuatayo kutoka kwa mwanaume

Eddy Tarimo

Member
Nov 27, 2016
27
38
KUTATULIWA MATATIZO
Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke.

KUBEMBELEZWA
Wanawake hupenda kubembelezwa pale wanapokuwa na huzuni, wengi wao hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa.

KUWA NAMBA MOJA
Safari ya penzi la mwanamke haishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Jambo la tatu ambalo wanawake wengi huhitaji ni kuwa namba moja au kupendwa. Wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla. Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, Malaya au kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya.

KURIDHISHWA KWENYE TENDO
Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako. Ni wajibu wa mwanaume kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo. Utundu unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako.

MAZUNGUMZO
Wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, huku wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, hii ikiwa na maana kuwa wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine. Kwa msingi huo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza mawazo yao. Kama una mpenzi wako mpe uhuru wa kuzungumza na kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali.

Kingine ongezea hapo.
 
Hayo yote ni kweli kabisaa na kwa kuongezea, ningependelea kuongezea pamoja kutia msisitizo hapo kwenye Mazungumzo: Wanaume wengi sana wanakosea kwa kukwepa kuwasikiliza wanawake hasa wale ambao ni wapenzi wao, kuna baadhi yao wako radhi wabishane na wanaume wengine kuhusu mpira hata kwa masaa 2 au zaidi lakini hawako tayari kusikiliza jinsi siku ya mpenzi wako imeendaje akikuelezea jioni baada ya kurejea. Inauma sana
Binafsi namsikiliza sana wangu japo naona kama haitoshi sababu nafikiri kwa jinsi nnavyoendelea na yeye ndiyo anazidisha; lakini sijawahi kumwambia zaidi ya kumtania tuu nafikiri ni sababu ya kabila lake na nature pia inachangia.
Ni hayo tuu.
 
Huo ni Utumwa wa kujitakia... haiwezekani labda awe kimada lakini sio mke kuna baadhi ya vitu viawezekana kwa kiasi tu ukizidisha ni tatizo jipya unazalisha
 
Wanaume Weng hudhan wanawake ni complicated kwa kuwa wako tofaut tofaut km maua kila moja na rang yake saiz yake na haruf yake,pamoja na tofaut hz wanawake kisaikolojia na kihisia wanafanana sana sabab ya homon malez na makuz ndo huwatofautsha kidogo kwenye kujitambua na kujithamin!
Mwanamke Hata awaje ukitaka kumloga umjali "caring", mpe muda yan tenga muda wakukaa nae,kuongea nae na kumsiliza km ulivosema mkuu!
km ni mkeo usiri wa aina yeyote ili ukiukaribisha utakuaribia kuliko kawaida usimfiche kitu akigundua kuna mambo unamficha anakosa kujiamin au kuwa na iman na safar yenu ya ndoa au mapenz!
Dharau huvunja ndoa nying kuliko michepuko!kudharauliwa na mwanaume alompa maisha yake humfadhaisha sana mwanamke kwan inamadhara sana kihisia "emotional abuse" kuliko hata kumpiga kwan maneno hayatokag upes kwenye kumbukumb kwa hyo chunga kaul zako,body language nk!
 
Shikamoo.
 
1.mpe hela..2.mpe hela.3.mpe hela..atafika kileleni kila siku..utakuwa # moja wake kila siku. We poteza muda tu hutafuti hela uko busy kutenga masaa mawili kila siku kumsikiliza mlimbwede wako..wakija watu na deep pockets haooo sha sha sha

Ukimfanya Mwanamke km bidhaa "object to be bought"nae atakuchukulia km mnunuz " buyer" ndio mana siku usipoweza mnunua wewe watamnunua wengne si ndo ilivo hata sokon!
ndo mana mtoa mada amesema ukitaka kupendwa na mwanamke kuyapata mapenz yake ya dhat hajazungumzia ukitaka kuupata mwili wake mkuu! na ingekua ni hela kwel bas ndoa zisingekuwepo au wangeoa kina dangote tu!rejea uzi plz!
 
Mkuu unajua kuwa wanawake wengi sana hapa duniani wameolewa ama wana mahusiano na watu wasiowapenda? (wamelazimika kwa sababu moja ama nyingine chiefly uchumi)..Je wanaume walioa hao wanawake (ama wenye mahusiano nao) wanajua kuwa hawapendwi (well mapenzi haswa toka moyoni)? Umeelewa nilichokuwa namaanisha?
 
Shikaamooni wakubwa kwa mwanamke uwe na cash tu kubembeleza peleka kwa Marlow, kikubwa wallet tena mkuu si umebase kwa wanawake wa kileo
Hapo hapo wewe provide cash tu aaah mengine yatakuja utapendwa wewe utafikiri ndio umebeba uhai wake
 
Wanaume Weng hudhan wanawake ni complicated kwa kuwa wako tofaut tofaut km maua kila moja na rang yake saiz yake na haruf yake,pamoja na tofaut hz wanawake kisaikolojia na kihisia wanafanana sana sabab ya homon malez na makuz ndo huwatofautsha kidogo kwenye kujitambua na kujithamin!
Mwanamke Hata awaje ukitaka kumloga umjali "caring", mpe muda yan tenga muda wakukaa nae,kuongea nae na kumsiliza km ulivosema mkuu!
km ni mkeo usiri wa aina yeyote ili ukiukaribisha utakuaribia kuliko kawaida usimfiche kitu akigundua kuna mambo unamficha anakosa kujiamin au kuwa na iman na safar yenu ya ndoa au mapenz!
Dharau huvunja ndoa nying kuliko michepuko!kudharauliwa na mwanaume alompa maisha yake humfadhaisha sana mwanamke kwan inamadhara sana kihisia "emotional abuse" kuliko hata kumpiga kwan maneno hayatokag upes kwenye kumbukumb kwa hyo chunga kaul zako,body language nk!
True dat
 
Ukimfanya Mwanamke km bidhaa "object to be bought"nae atakuchukulia km mnunuz " buyer" ndio mana siku usipoweza mnunua wewe watamnunua wengne si ndo ilivo hata sokon!
ndo mana mtoa mada amesema ukitaka kupendwa na mwanamke kuyapata mapenz yake ya dhat hajazungumzia ukitaka kuupata mwili wake mkuu! na ingekua ni hela kwel bas ndoa zisingekuwepo au wangeoa kina dangote tu!rejea uzi plz!
Very low level of thinking nashukuru umenisaidia kuwaelewesha
 
Mkuu unajua kuwa wanawake wengi sana hapa duniani wameolewa ama wana mahusiano na watu wasiowapenda? (wamelazimika kwa sababu moja ama nyingine chiefly uchumi)..Je wanaume walioa hao wanawake (ama wenye mahusiano nao) wanajua kuwa hawapendwi (well mapenzi haswa toka moyoni)? Umeelewa nilichokuwa namaanisha?
Mkuu mimi nimekuelewa sana unachomaanisha.
 
Wanawake wa siku hizi wanabadilika kila dakika, msijisumbue sana kuwa mnawaridhisha kila tu hao ni binadamu wana interest zao
 
Huo ni Utumwa wa kujitakia... haiwezekani labda awe kimada lakini sio mke kuna baadhi ya vitu viawezekana kwa kiasi tu ukizidisha ni tatizo jipya unazalisha

Mh km unaona utumwa utakua umeoa mtu ambae humpendi!kwa mtu unaempenda hamnaga jambo gumu kulifanya labda linalohatarisha maisha au afya !sijaona kigum kwa mke hapo halaf et labda kwa kimada really are u serious!?
 
Wako tofauti sana lakini kwa ujumla..., wanapenda sana hayo ambayo mtoa mada ameyaelezea, kuhusu pesa inategemea na mazingira aliyopo na vipi ukishampatia za kutosha?
 
Back
Top Bottom