bigmind
JF-Expert Member
- Oct 28, 2015
- 12,457
- 12,682
Jamani nichukue nafasi hii kabisa kwanza kutangaza interest kuwa nampenda MAMA YANGU kuliko wanawake wote duniani.
Pili nije kwenu nyie maua na viburudisho vya nafsi zetu sisi wanaume (naongelea wanawake).
Hapa ninapenda niwatumie nyie wanawake wa Jamii Forum ambao mimi binafsi nawachukulia km mama zangu, wachumba maana still mimi ni senior bachelor, shemeji maana lazima wengine mbaki kuwa shemeji siwezi kuwaonja wote, wengine wadogo zangu maana siyo wote tunalingana wengine dada zangu kwa umri ila hawakidhi kuwa mama zangu na pengine wengine shangazi zangu kwa sababu ya nafasi na hadhi zenu.
Binafsi nichukue nafasi hii kuwataja wachache nikimanisha kuwakubali hapa jukwaani kwa uwepo wenu na michango yenu inayosimama kuwakilisha sura ya mwanamke wa Tanzania na JF kwa mazingira au mawanda madogo.
Mamdenyi, Misschagga, Lara1, Faiza fox, Heaven sent, Chinchilla Coat, Nifah na EvelynSalt. Hawa wamama wamekuwa kioo cha jf wakibeba sura ya mwanamke wa kitanzania na Africa kwa ujumla.
Pia wapo maunderground ambao hawa kwa vituko na vimbweka hawajambo pia nachukua wasaa huu kuukubali mchango wao; miss Natafuta, Monnica, Paprika, Maabara, Joan, Emmyte na wengine wengi. Niwaombe radhi kwa wale ambao nitakuwa nimekosea majina yenu ya hapa jukwaani, na pia kama sijakutaja siyo kwamba u mdogo hapa JF au hauna mchango mkubwa kwangu na jamii kwa ujumla ila ujue inawezekana ni sababu tu ya kughafrika.
Baada ya kusema hayo niombe kuwaletea MALKIA WANGU WA NGUVU (mama yangu). Binafsi najivunia na kumpenda mama yangu kwa sababu moja tu ni SHUPAVU, JASIRI na MAHIRI.
MAMA YANGU (Anah John) huyu ni mzee kwasasa (70s yrs sasa) amemudu kwanza kutuzaa tukiwa wengi watoto 13 kati ya hao 10 tukiwa hai mpaka sasa na akatulea akiwa peke yake baada ya baba kufariki.
Huyu malkia wangu wa nguvu kwanza ni mdogo wa umbo lakini mwenye juhudi katika kufanya kazi. Malkia wangu asiyejua kusoma ata A anayo elimu ya asili yaani (informal education) alimudu kutulisha kwa kulima watoto 10 mpaka tukawa watu wazima na sasa mdogo ana miaka 28 wote wameolewa na kuolewa isipokuwa mimi tu.
Malkia wangu wa nguvu huyu hakuwahi kujifungulia hospital watoto wote 13, akuwahi kuzalishwa na mkunga wa mtu yeyote zaidi ya kujifungua akiwa peke yake au wakati mwingine akisaidiwa na baba yangu.
Malkia huyu alijivunia DAWA ZA MITI SHAMBA ambazo kiuhakika alimudu kazi ya UDAKIRARI kuwatibia watoto wake 13 (sisi) mpaka tukawa wakubwa isipokuwa watatu (mmoja alikunywa sumu bahati mbaya, mmoja alikufa kwa homa kali ya surua iliyotuvamia nyumba nzima {wototo}). Akiwa hajui kusoma, kuandika wala kuhesabu kwa maana ya namba za kimahesabu mama yangu huyu alimudu kutulea na kutuhudumia kwa mahitaji yote akiwa mzazi mmoja hakika kweli wewe mama yangu ni malkia wa nguvu.
Bila kuchoka alienda shamba tangu saa 12 asubuhi na kurudi saa 8 na kurudi shambani saa 9 mpaka saa 1 jioni haya ndiyo maisha ya mama yangu aliyoishi zaidi ya miaka 50 tangu ujana wake. Na ndani huu muda wa kazi alikuwa mjazito kwa nyakati tofauti ila hakuwahi kuchoka huku akifanya kazi kubwa ya kutuzaa pia kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula na kipato cha familia.
Natoa wito kwa SERIKALI na MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI yanayosaidia wanawake kuelekeza nguvu maeneo ya vijijini kusaidia wamama wa kariba ya malkia huyu (mama yangu) wenye mchango mkubwa kw taifa kwanza kuleta rasimali mhimu kabisa ( rasimali watu/human resources) lakini pia kutoa mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi hii, Tanzania ambayo asilimia 80% wananchi wake wanaishi kwa kutegemea kilimo akina mama wakiwa takribani 70% ndiyo wanaofanya shughuli za mashambani kama wazalishaji wa chakula na wameajiliwa mashambani.
Juhudi za haya mashirika yw haki za kijinsia na serikalli kwa ujumla zimekwama mjini huku wahitaji wakubwa wakibakia vijijini. Niwaombe wadao wote hasa wanawake kuungana katika kujikomboa kifikra (elimu) na kiuchumi ili kupunguza manyanyaso kwenu.
Nakupenda sana Mama yangu UTABAKI KUWA MALKIA WANGU WA NGUVU SIKU ZOTE Mungu akutie nguvu katika magumu unayopitia I LOVE YOU SO MANY TIMES...