Speaker Sitta alikoromea gazeti la RAI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Speaker Sitta alikoromea gazeti la RAI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mambo Jambo, Jun 19, 2009.

 1. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Speaker wa bunge la jamhuri ya muungano katika bunge la leo wakati wa matangazo amevikoromea vyombo vya habari vinavyokiuka maadili na kupotosha wananchi at the same time kusababisha chuki kati ya bunge na wananchi, amelitaja gazeti la RAI linalo milikiwa na mbunge wa Igunga Bw Rostam Aziz kuwa ni gazeti lisilofuata maadili ya uandishi wa habari na mara nyingi limekuwa likiandika lugha chafu na kulikashifu bunge, akitoa mfano amesema gazeti hilo toleo la jana limeandika kuwa bunge la Tz ni bunge mfu, amempa jukumu katibu wa bunge kufuatilia jambo hilo na sheria kali kuchukuliwa.


  MJ
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Sitta alitakiwa kujibu hoja na sio kutoa vitisho vinavyo undermine freedom of speech.
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Swali ni moja tu kwa Mh. Sitta:

  -- Kama siyo Bunge Mfu, kwanini Budget 2009/10 imepita ilihali kuna kasoro kibao zimeainishwa na kujadiliwa na wabunge wenyewe, haswa kuhusiana na posho za safari na chai??
   
 4. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Tunarudi kule kule kwenye ze utamu baada ya kutundika picha za boss, jamaa (bunge) walikuwa kimya wakati magazeti yanaandika habari mbaya kuhusu watu wengine, sasa limetajwa bunge ndiyo wanaamka.

  Only in bongo


  MJ
   
 5. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu, sidhani kuwa anatakiwa kujibu hoja baada ya kutukanwa kwa chombo kama Bunge. Hoja hujibiwa kwa tuhuma zinazotolewa kiungwana. Tuhuma hizo hizo zikitolewa kwa utangulizi wa "Bunge la Tanzania ni Bunge Mfu" au sentensi za namna hiyo, zina zima majibu yoyote halali ambayo yangeweza kutolewa, na kusababisha hatua za kisheria kuchukuliwa.

  Ukitaka kupata majibu ya hoja yoyote uliyonayo kutoka kwa mamlaka yoyote, ni lazima uweke wazi hoja yako, utumia utaratibu na ustaarabu unaoweza kumfanya yeyote unayetaka atoe majibu hayo kushawishika kukujibu bila kuwa offended. Na kutokana na majibu yake ndipo inaweza kubainika ukweli wa shutuma zozote. RAI ilitakiwa ijue kuwa Bunge linao uwezo wa kulichukulia hatua kali za kisheria na bila kufurukuta.

  Ila kwa system ya sasa, lolote linawezekana.
   
 6. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kulikoromea gazeti la RAI ni kuzuri kwa sababu tu kwamba gazeti hilo mara kadhaa limekuwa likitumiwa vizuri sana na RA kuwapaka matope makada wa upinzani na wale walioko mstari wa mbele kupambana na ufisadi.

  Lakini hapo hapo Spika Six aangalie sana asije jikuta akijijengea tabia ya kutumia madaraka yake kupambana na media houses.
   
 7. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,471
  Trophy Points: 280
  Wakuu nadhani habari iliyomchefua spika ni hii hapa, hebu tuiangalia kama kweli inachafua au mzee 6 ameghafilika tu  Wasomi wachambua ubinafsi wa wabunge

  :: Wakosoa namna wanavyochangia bajeti
  :: Wasema wanatazama uchaguzi ujao pekee
  :: Profesa Baregu aliita bunge la ‘marehemu’

  Na Sarah Mossi

  BAADHI ya wasomi wamekosoa aina ya uchangiaji mjadala wa bajeti ya Serikali ya mwaka 2009/2010 unaofanywa na wabunge wakidai uchangiaji huo haulengi kuisaidia serikali katika kuinua uchumi wa kitaifa, badala yake unatazama kuwanufaisha wabunge ‘kisiasa’.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili juzi, wasomi hao walisema, mjadala wa bajeti unaofungwa leo mjini Dodoma haukulenga kutazama maslahi ya kunyanyua uchumi wan chi badala yake wabunge walitumia kila nafasi waliyopata kujinufaisha wao kisiasa kwa kuzungumza lugha tamu zinapendwa kusikika na wapiga kura.

  Mmoja wa wasomi hao ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) Dk Richard Mushi aliliambia Rai kuwa; wabunge wengi hawakutazama jukumu lao la kutoa hoja za kitaifa badala yake wanawaza kuhusu uchaguzi mkuu unaofanyika mwakani.

  Mhadhiri huyo alisema; “tungetegemea wabunge wasimame na kuzungumzia masuala kama fedha za Halmashauri ziongezwe, suala la barabara na sio kuzungumzia masuala yao ya majimbo pekee,” anazungumza na kuongeza:

  "Kule bungeni kuna watu wachache wazuri sana, lakini sasa hivi wana presha kubwa ya kuchaguliwa mwakani na wanazikumbuka zile ahadi walizotoa katika uchaguzi mkuu uliopita."

  Msomi mwingine aliyezungumza na Rai ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Mwesiga Baregu ambaye alisema; sasa hivi wabunge hawawezi kuzungumzia masuala ya kitaifa kwa kuwa wanawaza zaidi majimbo yao.

  Kufuatia hali hii, Profesa Baregu alifafanua kuwa, mahudhurio ya wabunge kwa sasa ni hafifu pia ukilinganisha na mabunge mengine yaliyopita na hii inatokana na hali ya wabunge kuwa na mguu mmoja ndani ya bunge na mwingine nje ya bunge.

  “Hili si bunge la kujenga taifa. Ni la mkao wa uchaguzi wa mwakani, hata mahudhurio unayaona. Watatoka kwenda kwenye majimbo yao, hili ni bunge marehemu kwani nyoyo na fikra za wabunge zinatazama uchaguzi tu,” anasema Profesa Baregu na kuongeza:

  "Sijui kama uwezo wao wa kuzungumzia masuala ya kitaifa kama ni mdogo ama vipi...Lakini ninachoweza kusema kwamba safari hii wanazungumza wengi na hata wale wanaolala hawatalala kwenye bunge hili. Akili zao zimeanza kuota kurudi ama kutorudi.

  "Na hili angalau vyombo vya habari mmeliona mapema na mnapaswa kulipigia kelele, labda wanaweza kurudi," anasema Profesa Baregu.

  Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni Mchumi Kitaaluma, aliliambia Rai kuwa wabunge katika bunge hili wameonyesha upeo mdogo wa mambo ya kitaifa.

  "Lakini wengine wanaelewa wanachofanya, lakini wao ni wanasiasa wameweka mbele maendeleo ya maeneo yao. Wanataka wasikike kile wanachofanya sasa na tutarajie hilo na hapatakuwa na chochote cha kufanya na wao kama wanasiasa watataka wananchi wawasikie, hili ni jambo la kisiasa," anasema Profesa Lipumba.

  habari zaidi hapa
   
 8. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #8
  Jun 19, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mimi sioni tatizo lolote as far as neno mfu, marahemu si tusi kikamusi!! Na sio kweli kwamba kwa wenzetu weupe ambako kuna demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari 'matusi' dhidi ya vyama, serikali na hata viongozi huwa makali zaidi ya hapa kwetu? Iweje basi tujidai tunapigania kuelekea katika nchi yenye demokrasia ya kweli na uhuru wa vyombo vya habari wakati hatuna uwezo wa kupokea ukweli pale tuambiwapo?

  kweli ukweli huuma..............
   
 9. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2009
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mambo yanayokwenda nje ya maadili ya uandishi lazima yakemewe kwa nguvu zote....
  Namfagilia sana spika Sita kwa jinsi anavyoliongoza Bunge la miaka hii...

  Its real PROFESSIONAL
   
 10. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,897
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  These guys now have lost direction kabisaa. Too much issues hata sijui tuongeelee lipi kuhusu hawa wajamaa. But i believe one day mambo yatabadilika tuu and that day is just near!
   
 11. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mimi bado naona Spika kama anaona bunge halikutendewa haki kwa kuitwa mfu, basi angetolea ufafanuzi wa jambo lililopelekea kuitwa mfu na siyo kumtupia mpira katibu wa bunge. Mbona wakati gazeti la serikali "Taifa Letu" lilivyoandika kwamba wabunge wapanga kumkwamisha Kikwete alifoka na kuitaka serikali ijibu. MAJIBU yamewahi kutolewa hadi leo? Kwa hili pia RAI haitafanyiwa lolote na wala haitajibu. Massage Sent.
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,599
  Trophy Points: 280
  Ni haki yake kusema na kulikoromea.....maana nao wamezidi sana wanaandika kama hakuna mwenye nyumbaa kuwakemeaa
   
 13. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Hapa kuna mambo matatu;

  1. Zile sifa dhidi ya bunge kuwa ndiyo chombo kinachoaminika na wananchi zina wakera sana mafisadi (Kina Rostam ambae pia namiliki Rai) kwani wanajua fika lina pata sifa kwa kuwaandama. Sasa wanarudisha makombora ili nalo lichafuke hasa 6 na kikosi chake cha kina Mwakyembe.
  2.Spika anajua kuwa mashambulizi hayo yanamlenga yeye binafsi na kikosi chake hasa kutokana na hasira za mafisadi dhidi ya bunge, naamini lingekuwa gazeti lingine asingehamaki kiasi hicho! anajua Rostam yuko nyuma ya hili.
  3.Baadhi ya Wachangiaji humu JF wanachangia kwa sababu kweli wana uchungu na nchi hasa baada ya kuona bajeti mbovumbovu imepitishwa kirahisi tu na bunge letu. Lakini naamini wangejua ajenda ya RAI naamini wangegeuka!

  Mwisho, lengo la wanaolikandia bunge kwa kuputisha bajeti mbovu na lengo la gazeti la Rai dhidi ya bunge ni vitu viwili tofauti kabisa
   
 14. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Jamani kama kuna kaupepo ka kupindisha hii habari, ni kweli sita amekoroma ila amekoromea magazeti yote tena chanzo ni gazeti la mwananchi la jana lilichapisha picha ya wabunge ilikuwa kama imewafanya waonekane wana kiss(spika anadai imefanyiwa ujanja wa kamera) na kwenye picha hiyo pia kwa nyuma anaonekana baba wa mbunge huyo(wa kike). Kwa hivyo spika alisema kuna baadhi ya magazeti yanapigana jihadi na bunge ndio akatolea mfano gazeti la rai na habari ya bunge mfu.
   
 15. s

  sarahmossi Member

  #15
  Jun 19, 2009
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ah yetu macho!
   
 16. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #16
  Jun 19, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  He sarah upo msalimie sana deus
   
 17. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  tatizo letu bwatanzania tuko overly sensitive.Bunge jifu (si mfu kwani si mtu) inaweza kuwa description ya hali halisi ya bunge letu, wala si tusi.

  Kama unaona mtu anatoa maneno ya dhihaka, humjibu, unakaa kimya.Ukishamjibu umesha validate maneno yale, na ukishaya validate unatakiwa kuya address moja baada ya jingine.Bunge letu si jifu kwa sababu a be che de na kuendelea.

  Kuja na vitisho katika ulimwengu huu wa utandawazi kunaonyesha jinsi gani Spika Sitta alivyojikita katika ukiritimba wa miongo iliyopita.Hata kama Rostam amechemsha, kwa kumnyamazisha bila hoja Sitta anachemsha zaidi.
   
 18. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa nini Mmiliki R.A. asichukuliwe hatua? Nyie wabunge mnaolipwa na R.A. mtathubutu kumchukulia hatua za kisheria?

  Ufedhuli wote alioufanya R.A. unafumbiwa macho. Iko FEDHA!!!!. Hata kukwapua zile za EPA mchana kweupeeee hakuchunguzwi na hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa. Mhe. Sitta fahamu una-deal na mwamba!!!!! ********* wa Igunga. Siku za karibuni ata-claim ni descendant wa MIRAMBO mtemi wa Wanyamwezi, na hamtamfanya lolote!!!
   
 19. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #19
  Jun 19, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Nnachoona hapa ni kwamba vitu vinakuwa judged kwa minajili ya nani kasema, chochote atakachosema Rostam ni ufisadi, hata kama katika spin zake hizo atasema a truism.

  That our bunge is a rubber stamp is a truism, sasa kinachobishwa ni nini?

  Hayo mambo mengine ya picha zilizokuwa photoshopped awapeleke kwenye baraza la habari, sio kuleta mipasho.Spika mzima hana aibu.

  Sitta anasahau kuwa rungu lake la uspika linaishia kwenye bunge, akitoka nje muhimili wa nne hawezi kuufokea, watamlima yeye na bunge lake sawasawa.

  This speakers power seems to be going to his head now.What's next, is he going to ask every paper to submit their drafts for his approval?
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Jun 19, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mkuu STEVED
  Niko na wewe katika hili.
   
Loading...