kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,406
- 7,188
Mwendo wa kurudisha shughuli za makao makuu dar umeonekana mara baada ya kuaga dunia magufuli na mama samia kua rais. Swala la kuhamia dodoma limekua gumu kwa miaka zaidi ya arobaini hadi alipoingia magufuli.
Kitendo cha rais samia kuonekana kwa kupenda au kushauriwa kufanya shughuli za kiserikali dar kila wakati ndio inasababisha viongozi wengine kurudi dar kila mara. Inajulikana majengo na mazingira ya makao makuu bado kukamilika lakini magufuli alijua bila msuli huwezi hamisha makao makuu kwenda dodoma kwa kua tabaka la viongozi wa tanzania karibu wote wana makazi na vitega uchumi dar. Ukichunguza utakuta wabunge karibu asilimia zaidi ya 60 wana makazi dar. Watu wa dar ndio huenda kugombea ubunge karibu kwa majimbo yote.
Hili la kuhamia dodoma linahitaji musuli wa rais na nidhamu kwa watendaji wake. Kama ni shughuli za kibalozi rais akiwafuata dar watahamia lini dodoma? Shughuli za kibalozi hua makao makuu ya taifa. Si lazima wajenge nyumba.
Ubalozi wakibanwa kwenda dodoma kwa shughuli zao watapanga majengo na kuhamia dodoma.