Spare za magari kutoka South Africa

Forbes1990

JF-Expert Member
Apr 14, 2018
513
990
Habari wadau,

Kuna rafiki yangu anaishi South Africa nilimpa wazo la tufanye partnership ya yeye kuwa ananiagizia spare za magari Tanzania, kwa magari ambayo vipuri vyake kwa Tanzania ni ghali au upatikanaji wake ni mgumu.

Ameniambia kwa South Africa spare za magari kama BMW au Range sio ghali sana. Sasa naomba wenye uzoefu wa biashara hii mnipe muongozo namna biashara inavyoenda kwa ujumla.

Yaani aina ipi ya magari spare zake ni ghali na ni dili kama zikija.

Asanteni sana.
 
Kwauzoefu wangu south ukitaka kuagiza ni lazima ufanye oda maalumu maana wakikuleta spare zinakuwaga na utafauti kidogo na gari zilizotoka ulaya na japani, hii imeshawahi kututokea kwenye ford ranger na Scania na land rover
 
Asante Sana mkuu , kwa hiyo tahadhari..
 
Kwauzoefu wangu south ukitaka kuagiza ni lazima ufanye oda maalumu maana wakikuleta spare zinakuwaga na utafauti kidogo na gari zilizotoka ulaya na japani, hii imeshawahi kututokea kwenye ford ranger na Scania na land rover
Nadhan unatakiwa umielezee vizuri ili aelewe unaposema oda maalumu na kuletewa vifaa ambavyo vinautofauti, unamaanisha nn mkuu? Kwamba anatakiwa afanyeje wakati anaweka oda yake?
 
Back
Top Bottom