Soyinka Aichana Green Card Yake, Ni Baada ya Kutoa Ahadi Hiyo Iwapo Trump Angeshinda Uchaguzi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
Soyinka Aichana Green Card Yake, Ni Baada ya Kutoa Ahadi Hiyo Iwapo Trump Angeshinda Uchaguzi




MWAFRIKA wa kwanza kupata Tuzo la Nobel ambaye ni raia wa Nigeria anayeishi nchini Marekani, Wole Soyinka (pichani juu), ametimiza ahadi ya kuichana green card yake kama alivyoahidi hapo awali iwapo Donald Trump angeshinda urais wa Marekani, shirika la habari la AFP limeeleza.

Mwezi uliopta, mshindi huyo wa tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka 1986, alisema kuwa angeichana green card, ambayo humpa mtu kibali cha kuishi nchini Marekanai ikiwa Donald Trump angechaguliwa kuwa rais wa Marekani.



Donald Trump.

Soyinka aliyezaliwa Julai 13, 1934 nchini Nigeria na kupata elimu yake Uingereza, aliliambia Shirika la AFP mjini Johannesburg kuwa kutokana na ushindi wa Trump, basi ametekeleza alichokisema.

“Tayari nimeishafanya, nimetoka Marekani, nimefanya kile nilichosema kuwa nitakifanya, nimechana green card yangu , nimerudi sehemu ninayostahili kuwa,” alisema Soyinka.

Hata hivyo Soyinka hawashauri watu wengine wanaoishi Marekani kufuata uamuzi wake huo aliouchukua.chanzo.GBP
 
Huyu hana tofauti na mimi aliposhinda Magufuli nilichana kitambulisho changu cha Mtanzania lakini nimekwenda kuomba kipya baada ya kusema kile cha mwanzo kilipotea.o_O;):p
 
Back
Top Bottom