South korea wameshambulia kitu kilichodhaniwa kimetumwa na North korea.

Sokoro waito

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
2,201
2,598
Leo North korea imedhaniwa kutuma chombo cha anga ambacho hakijafahamika hadi sasa, south korea imetumia mashine gun kushambulia chombo hicho kilichokuwa kimevuka mpaka wao, lakini hawajasema kama wamekipiga au kimewatoroka! Source:www.express.co.uk
 
Naona wameanza kujitekenya na kujicheka wenyewe.
Kim Hana muda wa kutuma vitu vya kuichunguza Korea kusini maana anaijua nje ndani.
 
Hahahahahah nimechekaje jamani
mkuu hii inafurahisha huenda hata walichoshambulia ni yule ndege pori aitwaye tai wakidhani ni drone au missile ya N/korea, tofauti na hapo bhasi watakuwa wanatafuta kiki.
 
Huyu Kiduku atakipata anachokitafuta sasa, anazidi kuvuka mipaka sasa
mkuu una uhakika gani kama kweli walichokiona kilitumwa na n/korea maana hat s/korea wenyewe hawakusema ni kitu gani, walikipiga au kiliwatoroka? Huenda ni propaganda tu au fake news.
 
Inatafutwa kwa nguvu namna ya kuilaumu Korea ya kaskazini! Marekani wamerusha drone wenyewe halafu wanasingizia kuwa ni kitu kilichorushwa na Korea ya kaskazini!
Halafu ililengwa siku ambayo baraza LA umoja wa mataifa linakaa kujadili suala LA Korea kaskazini kurusha missile!
Marekani ameamua kuanzisha uongo kama ili kupata sababu za kulishawishi baraza ili liongeze vikwazo!
 
Wameizima wamesema yawezekana inaweza kua ni balloon ya kusambaza propaganda.
Ni jambo la kawaida, hata kusini kuna watu wengi hua wanafunga vitu kwenye balloon kama barua na video za kumkashifu mapanki alafu wanayatuma kwenda north.
 
Mimi nadhani NK watakuwa walituma TOY kwenda angani, halafu SK walivyo na hofu na NK wakadhani ni chombo cha kivita wakaanza kukishambulia.
 
Lile tambo lililofugwa na mmarekani halikugundua ata kuwa kiduku kawatumia msg kuwa mmefungia mtambo hewa ambao ninaweza kuukwepa na kuwachapa!!
 
dude h8lo hapo
 

Attachments

  • VID-20170520-WA0051.mp4
    3.3 MB · Views: 28
Back
Top Bottom