South African Western Cape Premier Helen Zille cites Nelson Mandela, Chinua Achebe, Ali Mazrui and G

kajembe

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
862
500
Waziri Mkuu wa Western Cape Afrika Kusini, Helen Zille, amejitetea bungeni kwa kuwataja – Nelson Mandela, Chinua Achebe, Ali Mazrui, na Godfrey Mwakikagile – baada ya kushambuliwa kwa yale aliyoyasema kuhusu ukoloni. Ameandika yafwatayo, “Why I raised the subject of colonialism in Twitter: Helen Zille”, in Times Live, 6 April 2017:

“If anyone genuinely (i.e. without animus or a private agenda) thought I was actually defending, justifying or praising colonialism, I apologised unreservedly and stressed that this was not so.

Many prominent people have repeatedly made the same point as I, including Nelson Mandela, Chinua Achebe, Ali Mazrui, Godfrey Mwakikagile and even a current matric history text book.

So why the mass hysteria when I made exactly the same point?”

Source:

Why I raised the subject of colonialism on Twitter: Helen Zille – The Times ....
www.timeslive.co.za >> The Times

Suala hilo limejadiliwa katika magazeti ya Afrika Kusini pamoja na vyombo vingine vya habari nchini humo, pamoja na nje, miongoni mwao na BBC na Aljazeera.

Licha ya Mandela ambaye amenukuliwa na Helen Zille katika hotuba yake bungeni, Western Cape, kuhusu ukoloni, ambayo iko hapa chini, hawa wengine aliowataja – Professor Ali Mazrui, Chinua Achebe, na Mtanzania mwenzetu Godfrey Mwakikagile – wamesema au wameandika nini kuhusu ukoloni mpaka waziri mkuu huyo wa Cape Province ameona umhimu wa kuwataja kutetea kauli yake?

Ifwatayo hapa chini ni hotuba ya Helen Zille katika bunge la Cape Province akijitetea kuhusu kauli yake ya ukoloni ambayo anasema inaungwa mkono na Mandela, Achebe, Mazrui, Mwakikagile na Manmohan Singh ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu wa India (2004 – 2014):
Link hapo chini
From the Inside: A debate of urgent national importance | Daily Maverick
 

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,863
2,000
Mwandishi wetu mdini muongo muongo Mohamed Said hajamtaja?
Duduwasha,
Huenda ni hasad, chuki, roho mbaya na mengine mengi yanayokufanya
ukatokwa na adabu na ustaarabu ikawa huwezi kufanya mjadala wa
heshima.

Ikiwa unadhani unaweza kunikejeli kwa hakika hotoweza na wasomaji
hapa watakuwa mashahidi.

Hellen Zille mbona pia hakukutaja wewe?
Zille anitaje mie kwa lipi na wapi tunakutana?

Lakini nitakufahamisha jambo.

Ali Mazrui tukiandikiana na tulikuwa sote wawili tumeunganishwa na watu
ambao mimi ni rafiki zangu.

Mmoja ni ndugu yake Sal Davis (Shariff Salim Abdallah) na mwingine ni
mwanafunzi na rafiki yake Dr. Harith Ghassany.

Kuhusu Godfrey Mwakikagile simfahamu binafsi lakini namjua kwa kumsoma
na yeye ananijua kwa kunisoma.

Sijui nimekuudhi kitu gani na sijui nini unakitafuta kwangu.
 

Duduwasha

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,713
2,000
Duduwasha,
Huenda ni hasad, chuki, roho mbaya na mengine mengi yanayokufanya
ukatokwa na adabu na ustaarabu ikawa huwezi kufanya mjadala wa
heshima.

Ikiwa unadhani unaweza kunikejeli kwa hakika hotoweza na wasomaji
hapa watakuwa mashahidi.

Hellen Zille mbona pia hakukutaja wewe?
Zille anitaje mie kwa lipi na wapi tunakutana?

Lakini nitakufahamisha jambo.

Ali Mazrui tukiandikiana na tulikuwa sote wawili tumeunganishwa na watu
ambao mimi ni rafiki zangu.

Mmoja ni ndugu yake Sal Davis (Shariff Salim Abdallah) na mwingine ni
mwanafunzi na rafiki yake Dr. Harith Ghassany.

Kuhusu Godfrey Mwakikagile simfahamu binafsi lakini namjua kwa kumasoma
na yeye ananijua kwa kunisoma.

Sijui nimekuudhi kitu gani na sijui nini unakitafuta kwangu.
Mbona Jazba tulia Dawa ikuingue..your not exist punguza fix kwenye majarida yako ..ya copy and paste plus fix haikubaliki my advice kwako si kwamba nakuvunjia heshima wewe ni Mkariakoo mwenzangu tu..
 

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,863
2,000
Mbona Jazba tulia Dawa ikuingue..your not exist punguza fix kwenye majarida yako ..ya copy and paste plus fix haikubaliki my advice kwako si kwamba nakuvunjia heshima wewe ni Mkariakoo mwenzangu tu..
Duduwasha,
Nadhani mwenye ghadhabu ni wewe ambae unakuja na matusi.
Mimi sijakutusi zaidi nakupa indhar kwa hiyo tabia yako.

Mimi sina haja ya kumkopi yeyote labda kama ni nukuu.
Najiweza kwa kuandika fikra zangu mwenyewe.

Ila ninachokiona kwako na chuki na ghadhabu wewe unaita
''jazba.''

Na si kama wewe ni wa kwanza kughadhibishwa na kalamu
yangu.

Kitabu cha Abdul Sykes kimewachoma wengi sana.

Mngependa mbakie na ile historia ya Chuo Cha Kivukoni ambayo
iliwafuta wengi wa mashujaa wa uhuru wa Tanganyika na waasisi
wa TANU.

Ikiwa una hoja ya kujadili na tujadili kejeli na lugha za kibabe kwangu
si mahali pake.

Unao uwezo na wewe andika kitabu cha historia ya uhuru unayoona
wewe ndiyo stahili.

Tutakusoma.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom