South Africa: President Jacob Zuma agrees to resign his office with immediate effect

Zuma aliingia madarakani kwa kumtia kishindo mwenzake Thabo Mbeki ajiuzuru. What goes around comes around, sasa yamemrudia yeye mwenyewe, na hayohayo pia yatatokea kwa Cyril Ramaphosa muda mchache ujao. Waliongoza harakati za kumng'oa Jacob Zuma madarakani kabla ya wakati wake kumalizika ni mashabiki na wafuasi wa Thabo Mbeki kama hatua ya kulipiza kisasi. Hivyo watakaomforosha Ramaphosa madarakani kabla ya muda watakuwa wafuasi wa Jacob Zuma, vicious cycle hadi hapo watakapoweza kuibadili Katiba yao.

Epukeni uongozi wa visasi vitawarudia wenyewe kwa namna hii au ile!!
 
Vuguvugu limeanzia Kusini mwa Africa linakuja kwa kasi sana katika jumuiya hii ya SADC
 
Nawapongeza viongozi wa ANC kwa kusikiliza kilio cha wananchi wa Afrika Kusini na Wanachama wao.

Nampongeza Rais Jacob Zuma kwa kujali maslahi mapana ya Chama chake na Taifa lake kwa kuamua kujiuzulu.

Liwe somo kwa viongozi wa nchi na vyama katika nchi za Afrika ikiwemo Tanzania
 
View attachment 695852

Rais wa South Africa Jacob Zuma ametangaza kuachia wadhifa wake wa Urais leo Februari 14, 2018

Zuma ametangaza leo wakati akitoa ujumbe kwa wananchi kupitia runinga

Mapema chama chake cha ANC kilimtaka Zuma kuachia madaraka au la sivyo kusubiri uamuzi wa kura za maoni uliokuwa ufanyike Bungeni Alhamisi ya tarehe 15

Zuma mwenye miaka 75 aliyeongoza nchi hiyo kuanzia mwaka 2009 amekuwa akipata shinikizo la kujiuzulu na kumuachia uongozi Rais ANC na Makamu wa nchi, Cyril Ramaphosa

Pia Zuma amesema hajafurahishwa kwa namna Chama chake kilivyomfanyia
======

South Africa's embattled President Jacob Zuma has resigned his office with immediate effect.

He made the announcement in a televised address to the nation on Wednesday evening.

Earlier, Mr Zuma's governing ANC party told him to resign or face a vote of no confidence in parliament on Thursday.

The 75-year-old has been under increasing pressure to give way to Deputy President Cyril Ramaphosa, the ANC's new leader.

Mr Zuma, who has been in power since 2009, faces numerous allegations of corruption.

His resignation came at the end of a long speech in which he said he disagreed with the way the ANC had acted towards him.

He said he did not fear a motion of no confidence, adding: "I have served the people of South Africa to the best of my ability."

BBC
Ni bora amejithathmini mapema na kuondoka bila shuruti vinginevyo angeondolewa kwa aibu kama Mugabe. Bado Museveni. Hivi hawa vichaa wa kiafrika wakiingia madarakani vichaa vyao huongezeka mara dufu?
 
Wabunge na wawakilishi wa anc aibu kwao kkwani Malema alipambana mwanzo mwisho lakini wao walimuona chizi n.a. kuona anc ni kubwa kuliko SA. Aibu kwenu wabunge wa anc wote..
 
Aliondolewa ROBERT Mugabe,Sasa Zuma atafuata Mfalme Mswati ,Kabila,Kagame ,Mseveni then who next...........
 
Wengine wanajitathimini na kuona bora waondoke ila huko nchi ya zimbobo wanatumia darasa la saba na fa fa fa fa fa fa fa kutaka kuongezewa muda kutoka miaka 5 hadi 7 kwa temu.

Trump pana mahala yuko sahihi japo siyo katika mambo yote.

Kweli mkuu hii nchi ina mambo mengi ya kushangaza. Na baada ya kuona jambo hili watu wengi hawalipendi wameona waanzie chini kwa chini kwa kuwadanganya wasomi wetu uchwara eti wawaongezee muda wa kustaafu so called professors na senior doctors wanaofundisha vyuoni. Hii ni janja siasa ili wakiibua la wanasiasa kuongezewa muda, hawa wanaojiita wasomi wakose pa kusemea maana watawahoji mbona mlipoongezewa muda wa kustaafu hamkukataa? Miaka sitini kustaafu ni sahihi hata uwe professor - wapo vijana nao wapewe hizo nafasi ili nao waweze kupanda na kufikia huo uprof.
 
Morgan!! Who is Morgan
Main
opposition leader wa Zimbabwe. Next time una google tu 'morgan dies' basi unapata clues. Mfano mimi sikua na taarifa baada ya kuona post ya mdau uliyem-quote nikaandika hayo maneno nikapata taarifa kamili.
 
Zuma's nine years term has been worse rulling with challenges lost of accountability with allegations of corruption scandals all these forced pressure inside ANC to leave the presidential office since wednesday.
 
Muosha huoshwa walishasema wahenga hapo mwanzo, na kipimo kile utakacho mpimia mwingine ndichi hicho utakachopimiwa.
 
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametangaza rasmi usiku huu kujiuzulu nafasi yake ya Urais na kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa waliompa wakati alipokuwa madarakani.Tukio hilo limerushwa live na TV ya afrika kusini SABC.
Hivi inakuwaje Unaona Uzi umeanzishwa na Mwingine kuhusu kujiuzulu kwa Zuma nawe unaingia kwenye uzi huo huo na kuleta habari ileile!!!?
 
Back
Top Bottom