Soseji za kuchemsha

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
Soseji ni kitafunwa kinachopendwa sana,na hutumika sana kama sehem ya kifungua kinywa.Ni namna nyingine ya kuhakikisha unapata protini kwenye kifungua kinywa.


Hata ivyo soseji huweza kutumika kama sehem ya mlo wowote wa siku,kikubwa ni aina ya upishi au uandaaji ufanane na mlo wenyewe.

kuna namna nyingi sana za kuandaa soseji,unaweza kuchemsha, kukaanga, kuchoma na hata kuoka.

Ingawa kuchemsha soseji ni njia rahisi,ya haraka na uacha soseji na harufu nzuri watu wengi hukosea sana namna ya kuchemsha soseji nakufanya wale soseji zisizokua na ladha nzuri na hazinukii viungo kabisa,na ndio maana utasikia wengi wakisema soseji hazina ladha.Ladha ipo tatizo ni uandaaji.


Njia.

1.weka soseji kwenye sufuria,weka maji kidogo sana kiasi cha kufikia nusu ya soseji zako endapo soseji zote zimegusa sufuria kwa chini (kama ilivyo katika picha).kama unachemsha paketi zima la soseji 12 basi weka maji robo kikombe.


  • ukiweka maji mengi zinapochemka ile ladha nzuri ya soseji hubaki kwenye maji,na kufanya ule soseji zisizokua na ladha wala harufu nzuri
2.Chemsha soseji kwa moto mdogo sana na hakikisha umefunika sufuria.


  • Lengo ni kuhakikisha joto (moto) linaingia ndani ya soseji ili kuivisha.unapofunika unatunza joto lote libaki kwenye sufuria na joto hilo huivisha soseji haraka.
  • Pia kufunika kunafanya harufu nzuri ya soseji isipotee
  • Ni vyema kujua kwamba soseji huiva haraka sana,na huitaji joto dogo tu ili kuiva.

3.Chemsha soseji adi maji yote yakauke .maji yakikauka inamaana utamu wote wa soseji umebaki kwenye soseji.ukiacha maji basi asilimia kubwa ya utamu utabaki kwenye maji


  • Hii ni moja ya sababu kwanini unachemsha kwa maji kidogo sana.
Mpaka hapo tayari kwa kula,utakula soseji zenye ladha nzuri na harufu inayovutia.

MAKOSA MADOGO YA KIUPISHI YANATOSHA KUPOTEZA LADHA YA CHAKULA
 
Hivi hizi BBQ ndio soseji? Maana nimewahi kuchemsha kama hiyo mweeee ile ngozi ngozi ikachubuka kama gamba la nyoka hta sikula
 
Soseji ziko,za aina tafauti, kuna za kuchoma ambazo ukichemsha hazifai. Hizi alizoonyesha dr MziziMkavu zinafaa kuchemsha ama kukaanga (kwa mafuta madogo sana hasa ukitumia a non-stick frying pan.
Hivi hizi BBQ ndio soseji? Maana nimewahi kuchemsha kama hiyo mweeee ile ngozi ngozi ikachubuka kama gamba la nyoka hta sikula
 
Last edited by a moderator:
Soseji ziko,za aina tafauti, kuna za kuchoma ambazo ukichemsha hazifai. Hizi alizoonyesha dr MziziMkavu zinafaa kuchemsha ama kukaanga (kwa mafuta madogo sana hasa ukitumia a non-stick frying pan.

Sawa mkuu, basi huku kuna soseji na hizo bbq mi nkamix kuchemsha vya kuchoma, nkaishia kumwaga
 
Last edited by a moderator:
ni muhimu kusoma label chap chap ukiwa markiti.zile sausage za kuchoma zina spices nyingi sana, ila unaweza kuzikaanga kwa mafuta kidogo sana na moto mdogo sana.

majuzi nimepata surprise hapo, nimechukua tuna fish in salty water nikijua nimebeba my usual tuna fish in olive oil. namimina kwenye frying pan nashangaa ni maji. vitunguu vikalowaaa. vile mwalimu na kungwi wangu farkhina, nikachakachua na hiyo tuna na noodles wala haikuwa kituko.

Sawa mkuu, basi huku kuna soseji na hizo bbq mi nkamix kuchemsha vya kuchoma, nkaishia kumwaga
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom