Sophia Simba: Sijawahi shutumu CHADEMA kupata misaada kutoka nje

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
Waziri Sophia Simba amekanusha kutoa tamko la kushutumu Chadema kupata misaada wa fedha kutoka nchi za nje kwa ajili ya kuleta machafuko nchini.

amesemea
- hajui shutuma hizi zimetokea wapi, na
-Chadema ndio wameanzisha shutuma hizo kwa manufaa yao wenyewe.
-hana uhusiana na nchi za EU au njia yeyote inayomuewezesha kupata hizo habari
za ufadhili wa Chadema.

Lakini Mb John Mnyika wa Chadema amesema Sophia Simba amekaririwa mara tatu na vyombo vya habari , ikiwemo TBC1 akisema Chadema inapokea fedha kutoka nchi za nje kwa lengo la kuleta machafuko nchini.

Utetezi huu wa Mh Sophia Simba umekuja baada ya balozi wa EU nchini Bw Tim CLarke kukanusha taarisha hizo kwamba kuna nchi 5 za EU zinazo fadhili CHADEMA (kwa malengo yoyote), kwani katiba ya EU hairushi wanachama wake kufhadhili vyama vya siasa.

SOURCE : The Citizen
 
hivi huyu mama ana akili kweli huyu au ana matatizo ya akili?sialijitokeza kwenye tv na sura lake mipoda lukuki akaanza kubwabwaja kuwa chadema wanapokea hela toka nje kuleta vurugu??
 
SOPHIA SIMBA NI BAADHI YA WANACHAMA WA CCM AMBAO TUNAWAOMBEA SANA WAENDELEE KUWEPO NA WAENDELEE KUPEWA NAFASI ZA JUU NDANI YA CCM KWANI HAWA NDIO WANAOIUA CCM NA CHADEMA ITAPATA NAFASI KUBWA TANZANIA KUTOKANA NA AINA HII YA VIONGOZI WA CCM

HII NI TYPE YA MAKAMBA,CHILIGATI,KIKWETE NA ROSTAM,VIVA MAMA SOPHIA ENDELEA KULIKOROGA SISI TUNAKUSOMA

kazi kweli kweliiiiiiii
 
hivi huyu mama ana akili kweli huyu au ana matatizo ya akili?sialijitokeza kwenye tv na sura lake mipoda lukuki akaanza kubwabwaja kuwa chadema wanapokea hela toka nje kuleta vurugu??

She just used this philosophy wrongly: If you have any news, do not say it. If you have to say it do not say it in public. If you have to say it in public, do not write it. If you have to write it, do not sign it. If you have to sign it, then be ready for the consequences.
U know she said it in public without writing it knowing she can just deny it; but she forgot that electronic media is retrievable.
 
Moja ya hulka ya viongozi wa CCM ni kukanusha kauli zao wenyewe....huyu mama nilimshuhudia mwenyewe akisema haya TBC1 akiwa na yule second lady
 
Unategemea nini hapo, kwa kichwa maji kama huyo?
Zaidi ya mipasho ikiongozwa na kijoti JK wao wanaitikia tu naiwe nomaa!!
hahahahahaaaa.
 
Ama kweli CCM ina limbukeni wengi...Sophia Simba.....na wengineo wengi kama yeye....CCM dead indeed...
 
hivi huyu mama ana akili kweli huyu au ana matatizo ya akili?sialijitokeza kwenye tv na sura lake mipoda lukuki akaanza kubwabwaja kuwa chadema wanapokea hela toka nje kuleta vurugu??

huyu mama si mtu wa kumjadili hata kidogo,mara nyingi matamko yake ni sawa na mtu alipepigwa nusu kaputi,mwacheni kama alivyo,hiyo ndiyo ccm!,hapo ndiyo ujiulize aliyemteua na kurudia tena yeye ana akili gani!?
 
Mi nshasema watu ni waoga sana, wanaogopa kusema ukweli wakidhani misaada itasimamishwa. Lakini mimi nilishaweka wazi. Baadhi ya watu na vyombo vya habari vinapotosha umma kuhusu hili swala. Swala hapa si nani anamfadhili nani bali ufadhili kwaajili ya kufanya nchi ionekane haitawaliki. Ukweli ni huu Balozi wa Denmark hapa nchini alianza harakati zake kule Zanzibar kupitia CUF akashindwa ingawa alileta chuki na kusababisha maafa makubwa tu sasa anataka kuleta hilo bara kwa kupitia CHADEMA. na hapa wanazunguka kama ilivyo marekani inavyotumia USAIDS kufanya kazi za CIA Denmark wanatumia shirika la actionaid na Global Platform Tanzania. Kuna kipindi nilisema nadhani hata Jamii Forum wanajua, sasa wameandaa makongamano ambayo ni mazuri na ninayakubali kama yalivyo maandamano yanayofanywa na CHADEMA ingawa tu maazimio ndiyo ninamashaka nayo. Tarehe 31/03/2011 kutakua na discussion on social media as a political tool Islam na Maxence wa jamii forum watasilisha mada on two biggest corruption scandals nitahudhuria ili kuona mdenish anatoa mwonngozo gani kupitia mawakala wao.
 
She just used this philosophy wrongly: If you have any news, do not say it. If you have to say it do not say it in public. If you have to say it in public, do not write it. If you have to write it, do not sign it. If you have to sign it, then be ready for the consequences.
U know she said it in public without writing it knowing she can just deny it; but she forgot that electronic media is retrievable.
for sure, many of these ruling party CCM officials are not aware with what technology has delivered to this world. Remember the former Zanzibar president with Majira newspaper incident! Watakula ujinga wao
 
Waziri Sophia Simba ... mara tatu na vyombo vya habari , ikiwemo TBC1 akisema
Nadhani hakusema.

Mwaka 2011 bado tunabishana na mtu amesema hakusema, na unasema kasema kwenye TV?

Weka evidence ya quote ya maneno yake au video clip tuone, tukate fitina. Vinginevyo hakusema!
 
Amesahau kusema alisema kwa mawazo yake binafsi, sio ya kichamachama au kiserekali serekeali!!
 
Mi nshasema watu ni waoga sana, wanaogopa kusema ukweli wakidhani misaada itasimamishwa. Lakini mimi nilishaweka wazi. Baadhi ya watu na vyombo vya habari vinapotosha umma kuhusu hili swala. Swala hapa si nani anamfadhili nani bali ufadhili kwaajili ya kufanya nchi ionekane haitawaliki. Ukweli ni huu Balozi wa Denmark hapa nchini alianza harakati zake kule Zanzibar kupitia CUF akashindwa ingawa alileta chuki na kusababisha maafa makubwa tu sasa anataka kuleta hilo bara kwa kupitia CHADEMA. na hapa wanazunguka kama ilivyo marekani inavyotumia USAIDS kufanya kazi za CIA Denmark wanatumia shirika la actionaid na Global Platform Tanzania. Kuna kipindi nilisema nadhani hata Jamii Forum wanajua, sasa wameandaa makongamano ambayo ni mazuri na ninayakubali kama yalivyo maandamano yanayofanywa na CHADEMA ingawa tu maazimio ndiyo ninamashaka nayo. Tarehe 31/03/2011 kutakua na discussion on social media as a political tool Islam na Maxence wa jamii forum watasilisha mada on two biggest corruption scandals nitahudhuria ili kuona mdenish anatoa mwonngozo gani kupitia mawakala wao.

Hongera we ni mtu mhimu sana ambae utatusaidia sana wengine jinsi ya kuchambua hoja,big up man.
 
Nadhani hakusema.

Mwaka 2011 bado tunabishana na mtu amesema hakusema, na unasema kasema kwenye TV?

Weka evidence ya quote ya maneno yake au video clip tuone, tukate fitina. Vinginevyo hakusema!

Hukumsikia....evidence ni sisi tuliomsikia
 
Kama umemsikia wewe ni witness, sio evidence. Tunataka evidence.

Na iwe video clip, maana mmesema kasemea mbele ya camera.

Na mmesema amesema mara tatu, kwa hiyo mtakuwa na video clip tatu, weka evidence ya video clip moja tu!
 
Back
Top Bottom