Sophia Simba: Richmond haikulipwa hata senti tano

Mimi nafikiri wapigakura watayafanyia kazi majibu yake ya kejeli 2010.Tuone kama atanunua Ubunge kama Umwenyekiti wa Umoja wa Wanawake.Na hata JK akipata tena Urais hawezi kuwarudisha kwa vituko vyao.

Mmaroroi, huyu mama anauhakika wa kuwa Mbunge 2010 bila kugombea wala kuomba kura kwa ajili yake, kuteuliwa wala kujigusa kwa namna yoyote kisiasa.

Ni Mbunge kwa kuwa tu, amekuwa Mwenyekiti wa UWT-CCM. Anaweza kukosa nafasi hiyo endapo tu chama kingine isipokuwa CCM kikishinda uchaguzi mkuu wa 2010 kwa kishindo cha Tsunami (more than 80% or so). Vinginevyo yeye ana uhakika wa Ubunge na endapo JK akiwa Rais, basi atapata na Uwaziri. Ndio maana hana haja ya kufikiria na kusema. Anasema tu.

Kwani tutamfanyeje bwanaaaa!!
 
huyu ana kichaa... kwa hasara nchi iliyoingia kwanini wasishitakiwe?
 
Hivi taifa liliingia hasara ya mabilioni mangapi kwa kukosa umeme kwa wakati kama tulivyoahidiwa na Richmond. Pamoja na hayo nauliza katika kipindi hicho:-
1. Watanzania wangapi walikufa.
2. Viwanda vingapi vilishindwa kufanya kazi ama kufungwa.
3. Kampuni ngapi zilipata hasara za mabilioni.
4. Ofisi ngapi za serikali hazikuweza kufanya kazi.
5. Watalii wangapi walivunja safari zao za kuitembelea Tanzania.
6. Wafanyakazi wangapi walipoteza ajira.
7. Familia ngapi ziliathirika kwa njia moja ama nyingine.

Duh, Sophia Simba - Waziri wa Utawala bora, Mbunge wa kuteuliwa na JK na Mwenyekiti wa Wake wa CCM.
images

Haya yawezekana tu Tanzania - nchi ya upendo, amani na utulivu.
kwingineko hilo domo lingetiwa kufuli.

Huyu mama anatutafuta nini watanzania?RA alipokuwa ana BoT akifoka kuwa anataka alipwe pesa haraka na alilipwa anataka kusema nini??siku zao zinahesabika kabisa hasa vibaraka kama SS.....muache tuu na ukilaza wake pumba.com
 
Huyo ndo Sophia Simba,mtoto wa mjini ati!..Kazi kweli mama wewe,unaaibisha serikali yako na wananchi wako!
 
Nani hajui kama mama simba kichwa chake kimajaa maji????????????
Nadhani najuta kumfahamu, apelekwe milembe
 
Huyu mama anatutafuta nini watanzania?RA alipokuwa ana BoT akifoka kuwa anataka alipwe pesa haraka na alilipwa anataka kusema nini??siku zao zinahesabika kabisa hasa vibaraka kama SS.....muache tuu na ukilaza wake pumba.com

Ana baraka zote za mkulu wa nji hii kusema anayosema. Kwamba siku zao zinahesabika I doubt it. Labda miaka 48 mingine ijayo. Kwa kumuungiza RA natarajia Game Theory ataibuka wakati wowote na kumtetea huyu mwendawazimu Sofia shangingi la Tandale kwa Mtogole.
Masatu uko wapi njoo utupe upande wa pili wa shilingi maana post zote nilizosoma zina upande wa sura ya nyerere tu, wapi upande wa mwenge?
 
Huyu mama ni mbunge wa kuteuliwa, na Raisi wa JMT, kwa sifa ambazo Raisi hapaswi kuulizwa, alimradi mchaguliwa ni member wa chama pekee chenye haki ya kutawala nchi.
Ndiyo maana utaratibu wa wabunge wa kuteuliwa, kwa lengo la kuongeza idadi ya wanawake wa CCM wawe wengi kulingana na wanaume haufai. Unatuletea vihiyo Bungeni, na sophia simba ni mfano mzuri unaong'aa!
 
Waziri wa Utawala bora kasema Richmond haikulipwa watu hawataki!! Mnataka hadi aseke Kikwete?

...si ndio hapo, sijui kwanini watu badala ya kuangalia 'ze BIG picha' wao wamekazania kukimbizana na 'vivuli'...aaarrrghhh, mnaniudhi kweli watanzania wenzangu!

hamuwezi kuunganisha dots (pesa za EPA -Richmond -uchaguzi wa 'urahisi', kisha takrima ya mabilioni ya nanihii...) kuweza kung'amua Chama cha nanihii ndicho kilicholipwa?

hebu mie, 'mdomo usije ponza kichwa!'
 
Tehe teh tih mosquito bwana nawe du! sasa wewe una mdomo au sindano? mhh mhh lol
 
Kwa ufupi huyu mama hafai hata kuwa katibu kata. Nadhani kuna haja wabunge wanaoteuliwa wapewe mtihani maalum.

Utumbo wote anaongea ni matokeo ya vyeo vya kupeana kama karanga.
 
Huyu mama nahisi nae ni moja wa mawaziri kihiyo kupata kutokea tz!issue hapo sio malipo,hapo issue kubwa ni jaribio la akina Lowassa kutaka kutenda uhalifu! wa kutuibia raslimali zetu!
Mama Simba tambua kuwa kuwekwa mtu hatiani sio tu lzm afanikiwe kuiba,ila hata kama tu utaonyesha dalili ya kutaka kuiba mahakama inaweza kukuweka hatiani,cha kufanya mama Lion sio kupayuka bali wafikishe mahakamani hawa vigogo na mahakama ndiyo iamue.plz heshimu utawala wa kisheria kama wizara yako unayoiongoza inavyosema

....Sofia Simba is a lost opportunity....!
 
Kwa ufupi huyu mama hafai hata kuwa katibu kata. Nadhani kuna haja wabunge wanaoteuliwa wapewe mtihani maalum.

Utumbo wote anaongea ni matokeo ya vyeo vya kupeana kama karanga.

Mh, hofu yangu ni iwapo huyo anayewateua wabunge wake anaouwezo wa kutunga mitihani.
 
kama hamna wanawake wenye uwezo wa kuongoza, JK weka wanaume kulikoni kutuwekea sofia simba ua hawa ghasia

kweli wanawake wa TZ this all what u have got

Unaponda wanawake bure ndugu. Kwani majority ya viongozi Tanzania ni wakina nani? Baraza la mawaziri majority kina nani? Bunge majority kina nani? Kwa nini kila mwanamke akichemsha lazima iwe kwa sababu ya jinsia yake? Wanaume wangapi wameliponza taifa? Wanao tuhumiwa na ufisadi wengi wao ni jinsia gani? Wewe sema tu Sophia Simba anachemsha kwa sababu IQ yake ndogo lakini kusema wanawake wa Tanzania ni viongozi wabovu wakati majority ya viongozi wabovu tunaona ni wanaume it's wrong.
 
Kwa ufupi huyu mama hafai hata kuwa katibu kata. Nadhani kuna haja wabunge wanaoteuliwa wapewe mtihani maalum.

Utumbo wote anaongea ni matokeo ya vyeo vya kupeana kama karanga.

Kisa cha kuweka wabunge wa kuteuliwa ni kupachika watu ambao hawaja chaguliwa na wananchi bila kufuatiza kigezo chochote. Hii CCM ina tumia sana kuweka watu wao ambao wanajua wakigombea majimboni kama wengine hawawezi kupigiwa kura.
 
Mimi nafikiri wapigakura watayafanyia kazi majibu yake ya kejeli 2010.Tuone kama atanunua Ubunge kama Umwenyekiti wa Umoja wa Wanawake.Na hata JK akipata tena Urais hawezi kuwarudisha kwa vituko vyao.

Ni mbunge wa kuteuliwa kwa maana haendi kuomba kura popote. Ubunge wa kuteuliwa unapewa na rahisi na hamna kigezo chochote maalumu kinacho tumika kumpa mtu ubunge wa kuteuliwa.
 
Huyu mama na yule sijui Ghasia wakifungua midomo yao natamani kijufungia chumbani. Yaani akiongea yeye ni utumbo mtupu.

Richmond hawajapata fedha wakati mdogo wake Muhammed Gire yupo Mahakamani, jee anafanya nini....?? Huyu ni ndugu na Iddi Simba? Na kama ni ndugu i hope Iddi Simba atamwambia anyamaze sababu anaiaibisha famalia.

..wakati mwingine, labda tumshauri Rais atambue kuwa wachumba waendelee kuwa wachumba, mashemeji, waendelee kuwa mashemeji, na viongozi wateuliwe kuwa viongozi. Mizigo ya Simba na Ghasia ni matokeo ya mkanganyiko wa kuteua bila kutambua iwapo wanaoteuliwa ni wachmba, viongozi au mashemeji.
'Bagambila balinsi'...... zibueni masikio msikie!
 
Back
Top Bottom