Sophia Simba: Richmond haikulipwa hata senti tano

Mwenda_Pole

JF-Expert Member
Jul 5, 2008
281
66
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Bi. Sophia Simba, amesema suala la kufikishwa mahakamani watuhumiwa wa Richmond bado lina utata kwani kampuni hiyo haikulipwa hata senti tano.

Kauli hiyo ya Waziri Simba ni mpya na inatofautiana na taarifa zote zilizowahi kutolewa kuhusu kampuni hiyo hadi kusabisha kuvunjwa mkataba wake huku baadhi ya mawaziri akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, kujiuzulu kutokana na utata katika mkataba wake na gharama za uendeshaji.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Simanjiro Bw. Christopher Ole Sendeka bungeni jana, Waziri Simba alisema watuhumiwa wa EPA na IPTL wanashughulikiwa kisheria na kwamba hawezi kujibu lolote kuhusu hatma yao kwa kuwa anakatazwa na Sheria za nchi.

“Nadhani Mheshimiwa Mbunge anatambua kwamba Serikali inafuatilia kwa karibu masuala hayo na EPA ipo mahakamani, siwezi kuzungumzia lolote, suala la Richmond ipo katika hatua mbalimbali na lina utata kwa kuwa haijalipwa hata senti tano," alidai Bi. Simba na kusababisha wabunge wengi kuguna.

Katika swali lake la nyonge, Bw.Sendeka aliitaka Serikali kuchukua hatua za utashi wa kisiasa kwa kuwachukulia hatua za haraka watuhumiwa wa Richmond, EPA na IPTL ili kuweka nchi katika sura nzuri ya kupambana na rushwa.

Source: Majira 10 June 2009
 
Huyu mama nahisi nae ni moja wa mawaziri kihiyo kupata kutokea tz!issue hapo sio malipo,hapo issue kubwa ni jaribio la akina Lowassa kutaka kutenda uhalifu! wa kutuibia raslimali zetu!
Mama Simba tambua kuwa kuwekwa mtu hatiani sio tu lzm afanikiwe kuiba,ila hata kama tu utaonyesha dalili ya kutaka kuiba mahakama inaweza kukuweka hatiani,cha kufanya mama Lion sio kupayuka bali wafikishe mahakamani hawa vigogo na mahakama ndiyo iamue.plz heshimu utawala wa kisheria kama wizara yako unayoiongoza inavyosema
 
Huyu mama na yule sijui Ghasia wakifungua midomo yao natamani kijufungia chumbani. Yaani akiongea yeye ni utumbo mtupu.

Richmond hawajapata fedha wakati mdogo wake Muhammed Gire yupo Mahakamani, jee anafanya nini....?? Huyu ni ndugu na Iddi Simba? Na kama ni ndugu i hope Iddi Simba atamwambia anyamaze sababu anaiaibisha famalia.
 
Huyu mazaa anamatatizo makubwa kweli kweli. Aidha njaa , au hiyo oblongata imejaa usaha.

Mfamaji nadhani ni yote mawili kwa kiwango kikubwa ni hilo la pili. For the past few months huyu mama naona it's better asiwe anaongea completely kuliko hayo yanayomtoka kinywani mwake maana ni aibu kwetu sote kama watz. Maana kuwa na waziri wa aina yake lazima sisi wote pia somehow tuwe nashida ya oblongata zetu pia.
 
Haiwezekani kuwa suala la Richmond kuwa gumu kwasababu tu kwamba hawakulipwa hata senti moja. Haiwezi kuwa sababu kwakuwa

1. Nia na utaratibu wa kuingiza Richmond nchini peke yake inatosha kutumika kuchukua hatua za kisheria kwa waliohusika.

2. Kuna watu wameshaanza kushtakiwa kwa kosa hilo na kesi zinaendelea mahakamani.

3. Kuna vipengele vya kisheria vinavyoweza kutumika kushughulikia suala hilo.

4. Wahusika wanajulikana na nia yao imetambulika katika utekelezaji mzima wa mchakato wa kuipa Richmond/DOWANS mkataba wa kufua umeme kinyume cha taratibu zote za manunuzi ya serikali.

Waziri anataka kusema nini hasa?
 
Mfamaji nadhani ni yote mawili kwa kiwango kikubwa ni hilo la pili. For the past few months huyu mama naona it's better asiwe anaongea completely kuliko hayo yanayomtoka kinywani mwake maana ni aibu kwetu sote kama watz. Maana kuwa na waziri wa aina yake lazima sisi wote pia somehow tuwe nashida ya oblongata zetu pia.

Hapana siyo wote! huyu ni mbunge wa kuteuliwa na pili mawaziri huteuliwa na ......... (mwingine anaweza kumalizia)
 
huyu mama,HAPANA!
angekuwa kijana mdogo wa kiume ningechelea kusema MIRUNGI HIYO!
sasa kwa umri na STATUS YAKE,dah!MUNGU ANISAMEHE SANA
 
Huyu mama anatoa majibu hayo kwa kuwa yeye na tajiri yake wanaamini kuwa maswali ya kina Sendeka ni sawa na kelele za mlango kwa mwenye nyumba. Tutarajie majibu hayo hadi siku tutakapothubutu kuongeza wawakilishi wa kweli wa wananchi bungeni!
 
Bank Kuu ilitoa pesa ili LC (Letter Of Credit) ifunguliwe kwa niaba ya Richmond. LC ilifunguliwa kupitia HSBC (Hong Kong Shanghai Banking Corporation) kutoka CRDB. muuzaji baada ya kupata LC alidispatch mzigo; na ndiyo fedha zililipwa. Mzigo ulilipwa; sasa hapo si pesa ilitumika? Nani atakupa mzigo bila kulipwa pesa yake siingekuwa default hapo?
CCM!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hivi hospitali ya "Milembe" bado ipo?

Nafikiri kabla hatujamjibu huyu mama hoja yake, angefikishwa Milembe kwanza.
 
Jamani huyu Mama ashakua Director wa AICC ambayo EL alishakua Director je kuna tatizo na watu waliowahi pita AICC kwenye issue za uadilifu?
 
Albeit Einstein aliwahi kusema,namnukuu kwa ung'eng'e,''If you don't have time to read,you don't have time to Lead'' Albeit Einstein

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba huyu mwanamke hajasoma,hana muda wa kusoma na kwa maana hiyo hana muda wa kuwa kiongozi. Kwa kifupi ni kuwa hafai kuwa kiongozi.

Frankly speaking I hate this mamaa! Huwa sielewi ni vigezo gani JK anatumia kuteua mawaziri wake. Baraza lote la Mawaziri wanaonekana kana vile hawajaenda shule au wana mtindio wa ubongo.

Sofia Simba sijamsikia akaongea point hat siku moja yeye ni mtu wa pumba siku zote.
Kauli zake mara nyingi zinakuwaga na utata na zinatia kichefuchefu. Juzijuzi tu alikurupuka kuhusu matamshi ya Mfanyabiashara Reginald Mengi kuhusu mafisadi papa na sasa tena hili la Richmond ameshaanza kuchemsha.

Kuna maswali ambayo napenda nimhoji huyu kigagula Sofia:

(1)Hivi kama Richmond haikulipwa hata senti moja ni kitu gani kilimfanya JK akavunja Baraza la Mawaziri na hatimaye kumweka pembeni rafiki yake kipenzi Edward Lowassa???

(2)Ile capacity charge iliyokuwa inalipwa kila siku kiasi cha Tshs. 150m zilikuwa zinapelekwa kwenye akaunti ya nani na wapi?

(3)Je, hii mitambo ya Richmond iliyoko pale Ubongo ambayo TANESCO walitaka kuinunua juzi ina maana haikuwahi kulipiwa????

Kama huyu mama atakuwa na majibu ya maswali haya na athibitishe kuwa hakuna senti iliyolipwa Richmond basi atakuwa ni extra genius ambaye JK anapashwa ampe Uwaziri wa Fedha!!!!
 
kama hamna wanawake wenye uwezo wa kuongoza, JK weka wanaume kulikoni kutuwekea sofia simba ua hawa ghasia

kweli wanawake wa TZ this all what u have got
 
Mimi nafikiri wapigakura watayafanyia kazi majibu yake ya kejeli 2010.Tuone kama atanunua Ubunge kama Umwenyekiti wa Umoja wa Wanawake.Na hata JK akipata tena Urais hawezi kuwarudisha kwa vituko vyao.
 
Huyu waziri kwa kufuka ndiyo mwenyewe. Tatizo viongozi wakifika huko juu, wanaona watu wote wa chini malimbukeni.
 
Issue hapo sio malipo,hapo issue kubwa ni jaribio la akina Lowassa kutaka kutenda uhalifu! wa kutuibia raslimali zetu!

Mama Simba tambua kuwa kuwekwa mtu hatiani sio tu lzm afanikiwe kuiba,ila hata kama tu utaonyesha dalili ya kutaka kuiba mahakama inaweza kukuweka hatiani,cha kufanya mama Lion sio kupayuka bali wafikishe mahakamani hawa vigogo na mahakama ndiyo iamue.plz heshimu utawala wa kisheria kama wizara yako unayoiongoza inavyosema

Kala ndoano ya mafisadi huyu mama.Hana jinsi ila kurudisha fadhila kwa kutetea ufisadi.
Cha kusikitisha ni kuwa Waziri wa Serikali ya Tanzania anatetea uvunjaji wa Sheria au attempt to defraud the Government.Sasa uwaziri huo ni kwa faida ya Taifa lipi?
 
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Bi. Sophia Simba, amesema suala la kufikishwa mahakamani watuhumiwa wa Richmond bado lina utata kwani kampuni hiyo haikulipwa hata senti tano.

Watasema lolote ili kuupotosha umma wa Watanzania katika kuelekea kwenye kinyang'anyiro cha 2010.

Huyu Mama kwa kusema uwongo tena bungeni ilibidi afukuzwe kazi haraka sana. Kuna ushahidi wa kutosha kuhusu malipo mbali mbali yaliyofanywa dhidi ya Richmond na mengine huyo papa fisadi Rostam alikuwa akiyafukuzia TANESCO na hazina pale alipokuwa akiona malipo hayo yamechelewa.
 
Back
Top Bottom