eliesikia
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 787
- 755
Siku ya 18th November 2010 09:56 PM nilitoa post hii kama tetesi... Watu wengi tulikataaa huyu na Meghji kuchaguliwa kwa kigezo cha GENDER ili tuokoe jahazi... Lakini Bahati mbaya Media karibia yote (Ikiwemo 'hata' Mtanzania nao walionahili)
Nimeamua kurudia hii post ili wadau mjue kuwa wakati mwingine ya msingi tuongee lakini ya kipuuzi tuache.. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ya kijinga tuache lakini yalio mema tuendelee nayo.. Lakini hapa hata watu "fulani" pia nao tuwaache kama sehemu ya mambo ya kijinga...
BARAZA limetulia saana "Japo kuna wachache wanachafua" this time haswa swala la sura mpya zenye "woga" na ari mpya lakini tuwape muda watusibitishie tunachoamini......
Kwa sasa Raisi kakosea zaidi kwa kumpeleka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ambayo kimsingi ni mzigo mkubwa kwa mtu kama Sophia... Hebu tujikumbushie ile post yetu kwanza....
Hoja:
WAZIRI wa zamani Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Mnyambi Simba, huko nyuma amewahi pia kutoa kauli zenye ukakasi akimshambulia mfanyabiashara (Mengi kuwa sio mwanaCCM )na mmoja wa wafadhili wa chama tawala kilichomweka waziri huyo madarakani.
Ni huyu huyu Sophia ambaye chama chake kimekanusha matamshi aliyotatoa mbele ya kadamnasi kuwashambulia wabunge wa kuchaguliwa walio mume na mke John Malecela na Anne Kilango Malecela.
Ni huyu Sophia mwenye dhamana ndani ya wizara nyeti ya Utawala Bora, yenye wajibu wa kusimamia mienendo ya watumishi wa umma, iliyo chini ya Ofisi ya Rais.
Ni huyu Sophia Simba, Habari za uhakika(Nipashe Jumapili) zinadaiwa kuwa zipo tuhuma kuwa Simba, amezuia mradi mkubwa wa ufugaji kuku wa asili kutoka nchini Ubelgiji kwa kuukalia mkataba bila kuusaini. Ilidaiwa kuwa juhudi za kuletwa kwa mradi huo zimefanywa na Katibu Mkuu wa UWT, Husna Mwilima, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Liege cha nchini Ubelgiji. Maudhui makubwa ya mradi huo endapo utekelezaji wake utaanza, utasaidia kuwapunguzia umaskini wanawake katika umoja huo hasa wenye kipato cha chini na pia kutunisha mfuko wa UWT.
Ni Sophia ndiye anayewajibika katika kusimamia na kutekeleza kiapo chake cha utii na kumshauri vema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika masuala mbalimbali yenye maslahi kwa taifa, bila migogoro yoyote.
Ni huyu Sophia, ambaye ndani ya chama chake, amekabidhiwa dhamana ya uenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) - wanaokiamini, kukipenda na kukitumikia chama tawala, yaani CCM.
Ni huyu Sophia aliyedaiwa kumwangushia kipigo, aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Janeth Kahama, wakati wa mchakato na kampeni za kumtafuta mwenyekiti wa wanawake hao kwa njia ya kura.
Ni Sophia huyu huyu, aliyewahi kukaririwa na vyombo vya habari akiwatetea wafanyabiashara wakubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kuzua gumzo na kuharibu upepo wa nchi wakati huo.
Sophia Simba, kwangu ni mwanamama anayekurupuka. Ni Waziri asiyejipa muda wa kutafakari na kueleza anachokifahamu. Wakati mwingine nahisi anatumika ama kwa nia ovu au kwa maslahi ya taifa ili kuharibu mwelekeo ama kuwasahaulisha walalahoi kero zinazowakabili.
Ni Sophia, aliyejaribu kucheza ngoma tofauti ya vita dhidi ya ufisadi iliyoanzishwa na viongozi wa vyama vya upinzani kabla ya kupokelewa kwa shangwe wa wakuu wa chama chake, akiwemo rais aliyemteua kushika nafasi ya uwaziri.
Ni Sophia aliyewashangaza wasomi na wasio wasomi, pale alipojiinua na kuishambulia familia ya wanasiasa, akiwemo mkongwe, Mzee Malecela.
Kwenye magazeti ya tarehe 21/06/2010 mwenyekiti wa UWT na pia waziri wa Utawala bora, Sophia Simba, amewashauri wanawake ambao ni wanachama wa CCM kutowapa unyumba waume zao ambao si wanachama wa CCM. .. maanayake: Anaonyesha wazi kuwa Ngono kwake yeye ni jambo muhimu zaidi kuliko kuendelea na misimamo sawia ya kinchi na utaifa.
Sasa siasa na ndoa vinaendana kweli? Mimi nadhani akili ya Sophia inawaza ngono wakati woote sasa na uwaziri wapi na wapi tena??? Aachwe akatoe huo unyumba anaosema kwa atakaemwomba... kweli huyu ni wakupuuza sana..
Ni imani yangu kwamba Sophia anahitaji kubanwa ili aanike tuhuma zote anazozifahamu, pengine atalisaidia taifa na kulirejesha kwenye mstari ili walalahoi waone raha na faida ya kuzaliwa juu ya ardhi ya Tanzania.
Pamoja na yote, nina ushauri kwa mkuu wake wa kazi. Kwanza amfukuze kwa sababu amejidhihirisha kwamba hafai kuwa kiongozi wa wanyonge kwa sababu ameshindwa kusimamia mienendo ya watumishi wa umma.
Sophia aanze kufuatiliwa, ahojiwe na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Polisi na Usalama wa Taifa.
Ni Imani yangu kwamba atatenguliwa uwaziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto katika nafasi aliyonayo sasa siku si nyingi, na hapo kutabadili fikira zangu kwamba analipwa fadhila za mema machache aliyoyatenda wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005(kumpitisha JK pale CCM). na sasa 2010 akiwa kama mwenyekiti UWT basi kapata zaidi fadhila za mkuu...
nawasilisha