Sophia simba hana hadhi ya kuwa waziri, JK kachemsha saaana!!! Nitachambua hili... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sophia simba hana hadhi ya kuwa waziri, JK kachemsha saaana!!! Nitachambua hili...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eliesikia, Nov 26, 2010.

 1. eliesikia

  eliesikia JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Siku ya 18th November 2010 09:56 PM nilitoa post hii kama tetesi... Watu wengi tulikataaa huyu na Meghji kuchaguliwa kwa kigezo cha GENDER ili tuokoe jahazi... Lakini Bahati mbaya Media karibia yote (Ikiwemo 'hata' Mtanzania nao walionahili)
  Nimeamua kurudia hii post ili wadau mjue kuwa wakati mwingine ya msingi tuongee lakini ya kipuuzi tuache.. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ya kijinga tuache lakini yalio mema tuendelee nayo.. Lakini hapa hata watu "fulani" pia nao tuwaache kama sehemu ya mambo ya kijinga...
  BARAZA limetulia saana "Japo kuna wachache wanachafua" this time haswa swala la sura mpya zenye "woga" na ari mpya lakini tuwape muda watusibitishie tunachoamini......

  Kwa sasa Raisi kakosea zaidi kwa kumpeleka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ambayo kimsingi ni mzigo mkubwa kwa mtu kama Sophia... Hebu tujikumbushie ile post yetu kwanza....

  Hoja:
  WAZIRI wa zamani Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Mnyambi Simba, huko nyuma amewahi pia kutoa kauli zenye ukakasi akimshambulia mfanyabiashara (Mengi kuwa sio mwanaCCM )na mmoja wa wafadhili wa chama tawala kilichomweka waziri huyo madarakani.

  Ni huyu huyu Sophia ambaye chama chake kimekanusha matamshi aliyotatoa mbele ya kadamnasi kuwashambulia wabunge wa kuchaguliwa walio mume na mke – John Malecela na Anne Kilango Malecela.

  Ni huyu Sophia mwenye dhamana ndani ya wizara nyeti ya Utawala Bora, yenye wajibu wa kusimamia mienendo ya watumishi wa umma, iliyo chini ya Ofisi ya Rais.

  Ni huyu Sophia Simba, Habari za uhakika(Nipashe Jumapili) zinadaiwa kuwa zipo tuhuma kuwa Simba, amezuia mradi mkubwa wa ufugaji kuku wa asili kutoka nchini Ubelgiji kwa kuukalia mkataba bila kuusaini. Ilidaiwa kuwa juhudi za kuletwa kwa mradi huo zimefanywa na Katibu Mkuu wa UWT, Husna Mwilima, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Liege cha nchini Ubelgiji. Maudhui makubwa ya mradi huo endapo utekelezaji wake utaanza, utasaidia kuwapunguzia umaskini wanawake katika umoja huo hasa wenye kipato cha chini na pia kutunisha mfuko wa UWT.

  Ni Sophia ndiye anayewajibika katika kusimamia na kutekeleza kiapo chake cha utii na kumshauri vema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika masuala mbalimbali yenye maslahi kwa taifa, bila migogoro yoyote.

  Ni huyu Sophia, ambaye ndani ya chama chake, amekabidhiwa dhamana ya uenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) - wanaokiamini, kukipenda na kukitumikia chama tawala, yaani CCM.

  Ni huyu Sophia aliyedaiwa kumwangushia kipigo, aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Janeth Kahama, wakati wa mchakato na kampeni za kumtafuta mwenyekiti wa wanawake hao kwa njia ya kura.

  Ni Sophia huyu huyu, aliyewahi kukaririwa na vyombo vya habari akiwatetea wafanyabiashara wakubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kuzua gumzo na kuharibu upepo wa nchi wakati huo.

  Sophia Simba, kwangu ni mwanamama anayekurupuka. Ni Waziri asiyejipa muda wa kutafakari na kueleza anachokifahamu. Wakati mwingine nahisi anatumika ama kwa nia ovu au kwa maslahi ya taifa ili kuharibu mwelekeo ama kuwasahaulisha walalahoi kero zinazowakabili.

  Ni Sophia, aliyejaribu kucheza ngoma tofauti ya vita dhidi ya ufisadi iliyoanzishwa na viongozi wa vyama vya upinzani kabla ya kupokelewa kwa shangwe wa wakuu wa chama chake, akiwemo rais aliyemteua kushika nafasi ya uwaziri.

  Ni Sophia aliyewashangaza wasomi na wasio wasomi, pale alipojiinua na kuishambulia familia ya wanasiasa, akiwemo mkongwe, Mzee Malecela.

  Kwenye magazeti ya tarehe 21/06/2010 mwenyekiti wa UWT na pia waziri wa Utawala bora, Sophia Simba, amewashauri wanawake ambao ni wanachama wa CCM kutowapa unyumba waume zao ambao si wanachama wa CCM. .. maanayake: Anaonyesha wazi kuwa Ngono kwake yeye ni jambo muhimu zaidi kuliko kuendelea na misimamo sawia ya kinchi na utaifa.
  Sasa siasa na ndoa vinaendana kweli? Mimi nadhani akili ya Sophia inawaza ngono wakati woote sasa na uwaziri wapi na wapi tena??? Aachwe akatoe huo unyumba anaosema kwa atakaemwomba... kweli huyu ni wakupuuza sana..

  SophiaSimba.jpg


  Ni imani yangu kwamba Sophia anahitaji kubanwa ili aanike tuhuma zote anazozifahamu, pengine atalisaidia taifa na kulirejesha kwenye mstari ili walalahoi waone raha na faida ya kuzaliwa juu ya ardhi ya Tanzania.

  Pamoja na yote, nina ushauri kwa mkuu wake wa kazi. Kwanza amfukuze kwa sababu amejidhihirisha kwamba hafai kuwa kiongozi wa wanyonge kwa sababu ameshindwa kusimamia mienendo ya watumishi wa umma.

  Sophia aanze kufuatiliwa, ahojiwe na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Polisi na Usalama wa Taifa.  Ni Imani yangu kwamba atatenguliwa uwaziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto katika nafasi aliyonayo sasa siku si nyingi, na hapo kutabadili fikira zangu kwamba analipwa fadhila za mema machache aliyoyatenda wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005(kumpitisha JK pale CCM). na sasa 2010 akiwa kama mwenyekiti UWT basi kapata zaidi fadhila za mkuu...

  nawasilisha
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  JK kumbakiza uyu mama lazima kuna kitu au kwa sababu ni chairperson wa UWT?
   
 3. D

  Derimto JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama unaweza kuangalia kwa makini ndani ya ccm utagundua kwa sehemu kubwa imejaa makahaba, madalali, wahuni, mashangingi ya micharukoni na wengi wao ni watu ambao hujipatia kipato cha kiujanjaujanja tu.

  Mimi sishangai kwa yeye kupewa wizara mbona kuna wabovu kibao wamejishikia uma wanakula kwa raha zao.
   
 4. Kitutu JR

  Kitutu JR Member

  #4
  Nov 26, 2010
  Joined: Jul 23, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eliesikia.. We mtu ashawahi fungua vizibo sumwhere na elimu yake darasa la saba kamaliza kwa msaada wa mwalimu mkuu unahisi weledi wake wa kufikiria utakuaje?
   
 5. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Unataka kuniambia Sophia Simba Alishawahi kuwa BAR MEID??? nipe jina la Bar hiyo. Lazima hayo ni maneno ya WALEVI aliokuwa anawahudumia. Dah!!!!!!!! Nipe jina la Bar nimtafute Maneger wake tafadhali atakuwa na mengi ya kutuambia.
   
 6. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu Kitutu JR are Serious?
   
 7. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #7
  Nov 26, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama vigezo hivyo vyote viko kinyume na yote.Tutafute vigezo vingine may be ni mtamu na huroda anaotoa kwa wakubwa unawachanganya akili kunawatu wanavipaji katika huroda kipaji hiki hakipimwi kwa vigezo vingine bali kitandani.MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  aliwahi kuuza bar ya baba yake kule ilala bungoni miaka hiyo
   
 9. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  jina la BAR tafadhali!!!!!!!!!!!
   
 10. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kuna makala iliandikwa cku za nyuma akielezea maisha yake alisema aliuza bar morogoro karibu na uwanja wa sabasaba walipokuwa wakiishi
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nenda Moro pale karibu na stand ya daladala mjini utakuta wazee wanakunywa kahawa waulize watakuonyesha mpaka eneo lenyewe
   
 12. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Shilingi ina pande mbili. Wewe unaandika kwa mtazamo hasi, unaweza kututhibitishia kwamba hamna mazuri huyu mama aliyofanyia nchi hii? Mtoto wako akipata maswali 4 kati ya kumi utamshambulia kwa kuwa yuko chini ya 50% au utamtia moyo kwa hiyo 40% aliyopata ili aongeze bidii? Mimi binafsi sioni sababu ya mtu kuandika mabaya tuu bila kuweka na yale mazuri kama hana chuki binafsi.
   
Loading...