Sophia Mjema: Ilala yakamata wanafunzi hewa 599 katika shule 6

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
1-34.jpg


Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala wakati alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya hiyo ambapo uchunguzi wa wanafunzi wengine hewa bado unaendelea.

2-11.jpg


Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akisisitiza jambo wakati alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala wakati alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya hiyo, Kulia ni Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Bw. Edward Mpogolo.

3-7.jpg


Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala wakati alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya hiyo.

…………………………………………………………………………………………………..

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema ametangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya ya Ilala ambazo hakuzitaja, Mjema amesema baada uchunguzi huo kumegundulika wanafunzi idadi hiyo ya ambapo wahusika wote watachukuliwa hatua za kinidhamu lakini pia sheria itachukua mkondo wake kwani hayo ni makosa kama yalivyo makosa mengine

Wilaya ya Ilala ina shule za sekondari za serikali 46 na za sekondari 49 ukiacha shule za taasisi binafsi ,zoezi la ukaguzi bado linaendelea katika shule zote za msingi wilayani humompaka Septemba 1 mwaka huu ndiyo litamalizika.

Akizungumzia suala la Madawati mkuu wa wilaya huyo amewapongeza wadau wote waliochangia madawati mpaka kuhakikisha uhaba wa madawati katika wilaya ya Ilala unakwisha huku kukiwa ziada ya madawati 2821

Ameongeza kuwa kazi kubwa inayofuatia kwa sasa ni kuongeza vyumba vya madarasa ambapo kazi hiyo inaendelea vizuri .

Mh. Sophia mjema pia amemshukuru Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuanzisha mkakati wa wadau kuchangia madawati jambo ambalo limesaidia tatizo hilo kushughulikiwa kikamilifu na wadau mbalimbali, lakini pia akampongeza Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda kwa usimiamizi thabiti wa utekelezaji wa mkakati huo jambo ambalo limesaidia wilaya ya Ilala kumaliza kabisa tatizo la uhaba wa madawati katika shule za zake za msingi
 
Wanafunzi hewa au school dropouts ambapo wizara ya vijana inatakiwa iangalie sababu zake. Ni tatizo hili sio kitu cha kujivunia kabisa uku Ummy, Kigwa, Ndalichako na serikari kwa ujumla sio aspect wanazojali kuziangalia. Wapo more concerned na publicity uchwara
 
Yaani hii nchi maendeleo ni ndoto....hakuna mikakati kabisa utafikiri wote tumezaliwa jana....

Yote hii ni sababu hatujui nani afanye nin
Kila siku tunaaminishwa au kumbiwa habari mbaya tuuuuu kama vile hapakuwepo na viongozi hapo Kabla..
 
Ni uongo hakuna wanafunzi hewa, najua ninachokisema!
 
Safi sana mama yetu, hongera sana
Mwalimu mkuu au afisa elimu or whoever is responsible na student registration ana interest gani ya kuwa na wanafunzi hewa hakuna posho zozote wala budget za shule azipelekwi kwa idadi ya wanafunzi.

If anything asilimia kubwa ya hizo namba ni wanafunzi walioacha masomo Ndalichako atupe majibu maana ili ni tatizo kwenye hiyo wilaya sio kuonea wafanyakazi tu.
 
Duh! Wanafunzi hewa,wafanyakazi hewa wanasiasa hewa madokta hewa ,wapenzi hewa , madikteta hewa, wanasheria hewa ,ndoa hewa ,wastafu hewa tubadili na jina la nchi sasa iwe tanzahewa
 
Mwisho wa siku watoro wataitwa wanafunzi hewa, halafu mbona kama ana haraka sana! Shule ziko 95 bado hajakagua 89! Keshakuja kwenye kipaza sauti ili awawahi wengine au!
 
Wanafunzi hewa au school dropouts ambapo wizara ya vijana inatakiwa iangalie sababu zake. Ni tatizo hili sio kitu cha kujivunia kabisa uku Ummy, Kigwa, Ndalichako na serikari kwa ujumla sio aspect wanazojali kuziangalia. Wapo more concerned na publicity uchwara
Well
Was about to ask on the same! Tunatofautishaje hewa vs dropouts?
 
Wafanyakazi hewa. Walimu hewa. Wanafunzi hewa.
Kila kitu hewa. Hadi wamalize ukaguzi 'hewa' miaka mitano imeshapita.
 
Nimejaribu kufuatilia Kwa umakini hichi wanachoita ni wanafunzi hewa sio wote ni hewa, wanafunzi wanaacha shule kwa kasi ya Ajabu, wengine wamehama, wengine watoro, wengine wamemaliza, wengine wanakufa sasa kabla hata ya mkuu wa shule kuwaondoa shule inavamiwa na mikamera na waandishi Wa habari kibao! Hii serekali itafika mahali itaparaganyika
 
Nimejaribu kufuatilia Kwa umakini hichi wanachoita ni wanafunzi hewa sio wote ni hewa, wanafunzi wanaacha shule kwa kasi ya Ajabu, wengine wanachama, wengine wamemaliza, wengine wanakufa sasa kabla hata ya mkuu wa shule kuwaondoa shule inavamiwa na mikamera na waandishi Wa habari kibao! Hii serekali itafika mahali itaparaganyika
Mkuu ndio kusema kuna mkurupuko ktk hili?

Kama ulivyosema,nilidhani systematic verification ingefanyika ili kutenganisha cases tofauti mfano watoro sugu,walioacha,waliohama bila kutoa taarifa,waliofariki na finally "waliochomekwa" kwenye attendance book na register mbalimbali ingawa hawajawahi kusoma shule husika ili tufike pahala precisely tuseme idadi ya wanafunzi hewa
 
Well
Was about to ask on the same! Tunatofautishaje hewa vs dropouts?
Zinawatosha wao wenyewe sio kuongoza nchi.

Hii inaitwa kukariri at best wanafunzi hewa = dropouts.

Hakuna faida ya kuwa na wanafunzi hewa mashuleni faida ya hili zoezi ni kumuweka Ndalichako na wengine wenye majukumu ya interest za vijana serikarini on the spotlight at least this time for the right reasons.

Zoezu liendelee nchi nzima na tuone raisi atachukua hatua zipi kwa mawaziri wenye dhamana iwapo tatizo likibainika sugu watu awawezi kutafuta kazi rahisi na kuzikimbia technical aspects za wizara wanazodai wamesomea.
 
Kuna tatizo kubwa ktk kuliripoti hili suala. Ukweli hausemwi.
 
Back
Top Bottom