Sony Experia Z

mojoki

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
1,314
290
Hello good people

Ninayo sony experia Z, hii simu nilinunua mpya kabisa dukani na nikatumia kwa zaidi ya miezi 3... Ghafla Hasubuhi naamka nikashangaa haisomi network nikajaribu kuirekebisha hapa na pale wap...

Nikaamua mwisho wa siku ku update operating system huko ndo ikawa balaa tupu kwa sababu simu ikawa na tatizo la kuzima na kuwaka, nikaamua kuipeleka kwa fundi maarufu posta fundi Sele, fundi sele akachemka nikampeleke Sirleaornad david ( Ni mdau pia humu JF), Jamaa akafanikiwa kuirestore operating system na ikawa inawaka na kuonyesha Application zote kama mwanzo lakini tatizo la NO SIMCARD likabKi pale pale, Nilichokuja kugundua this time hata ukijaribu kuangalia IMEI kwa kubonyeza *#06# inaonyesha blank kwamba simu haina IMEI

Ukiingia kwenye settings kuangalia baseband pia hamna kitu, sijajua hili ni tatizo gani na nitalitatua vipi ukizingatia simu nimenunua karibia 1.4 ndugu wadau

Kwa sasa simu naitumia kwa ajili ya Camera na kuangalia movies tu (Hapa sasa hivi nimetoka kuangalia series ya Suits "Mike ross grandma amefariki" and jamaa ndo alikua ametoka kumnunulia Apartment) , I feel sad for him..."Louiss lazima Atakua Mhaya mzungu"

Kama kuna fundi mwenye ujuzi au mtu aliyewahi patwa na tatizo kama hilo na amefanikiwa kutatua naomba msaada tafadhali

Nawasilisha
 
Hebu nenda jisajili xda developers forums, halafu angalia kama unaweza pata custom rom na kernel na ufanye installation upya.
 
Dah pole ndugu. Wasi wasi ndio akili nilikuwa naipenda sana hii simu lakini niliingia uoga baada ya kwenda international forum mbalimbali.
 
pole mkuu,
kuna ndugu yangu alikuwa anatatizo kama lako. alifanya kila ishu ya ku factory na hata ku root.

tatizo hapo ni wewe uliweka line (sim card vibaya), vipini vya kusomea line havigusi bati ya dhahabu ya sim card vizuri.

nilimtengezea ndugu yangu kwa kunyanyua vipini vya simu (sim card slot reader) na ishu ikasoma network.

sikushauri ufanye wewe mwenyewe, lakini hebu chunguza kwanza sehemu ya kuweka sim card uone kama vipini vipo sawa. kawaida vipini vipo vitatu ukiona viwili ujue kimoja kimelala au kimekatika. kama bado kipo kazi ni rahisi ya kukiinua tu na network itasoma.

hope nimekusaidia.
 
Unataka kuniambia mkuu vipini kukaa vibaya ndo visababishe hadi nishindwe kuona IMEI ya simu
 
Hebu nenda jisajili xda developers forums, halafu angalia kama unaweza pata custom rom na kernel na ufanye installation upya.

Ok Mkuu ndo nipo huko na post swali
 
Unataka kuniambia mkuu vipini kukaa vibaya ndo visababishe hadi nishindwe kuona IMEI ya simu

hapo sijuwi, lakini simu kama iphone huwezi kupata imei (njia rahisi ya *#06#) bila sim card. tatizo sio software mkuu labda kama wewe unajua ulijaribu kufanya modifctn yeyote ile hadi umepoteza imei
 
Hilo tatizo limenikuta hata mm kwenye Nokia N8. Hadi leo hii nimeipaki haifanyi kazi kwenye network.
 
hapo sijuwi, lakini simu kama iphone huwezi kupata imei (njia rahisi ya *#06#) bila sim card. tatizo sio software mkuu labda kama wewe unajua ulijaribu kufanya modifctn yeyote ile hadi umepoteza imei

iPhone unaweza kuangalia IMEI bila simcard mkuu, sio iPhone tu simu yoyote
 
Mkuu hiyo SUITS uliyoangalia ni season ya ngapi? Unaweza kunipa link ya kuidownload

Season 1 ilitoka 2011
Season 2 ikatoka 2012
Season 3 imetoka 2013

Nilikua naangalia season 2 episode 10 on my way to season 3

U can download via torrent, just andika google "Suits season 1 complete torrent"

Au tembelea kikckass torrent webisite
 
Asante sana, kuna series nyingine unazozijua kama hizo {zakiprofession, intelligence etc}?
 
iPhone unaweza kuangalia IMEI bila simcard mkuu, sio iPhone tu simu yoyote

simu zote wa weza kuangalia imei bila sim card lakini njia ya ku dial *#06# haikubali kwa iphone kama haina simcard labda uende settings na about
 
Pole mkuu,mimi ndio maana nimeamua kuachana na majina ya simu eti Samsung Mara HTC hii zote ni product ya mchina na wanabambika hasa siku hizi.
 
Du! nashindwa kuamini nilichokisoma kuhusu sony. Maana hawa jamaa bidhaa zao ziko makini maana mimi nabadilisha model tu za sony.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom