Sonona (Depression): Jinsi ya kupambana nayo na kumsaidia mwathirika

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,858
7,846
Wadau, tulianza kwanza kwa kuangalia Maana ya Sonona (Depression) huku pia tukiangazia jinsi ya kumtambua mwenye Sonona. Unaweza kusoma hapa zaidi – UGONJWA WA SONONA (DEPRESSION): Usiyoambiwa na jinsi ya kupambana na tatizo hili

Leo tunaangazia jinsi ya kupambana na Sonona na kumsaidia mwathirika wa tatizo hili.

Zingatia masuala haya kumi:

1) Jipangie ratiba ya kufanya kazi zako pindi tu utakapohisi una dalili za Sonona.

2) Jiwekee na kujipangia malengo katika maisha yako. Usikate tamaa, weka matumaini yako juu ya kila kitu unachopanga katika maisha, usifikirie yaliyopita kwani unatakiwa ujipange upya na kufanya mambo mazuri na makubwa zaidi

3) Ongea na mtaalamu wa Afya ya akili au Daktari kuhusu hali yako. Pia, jaribu kuongea na mtu wako wa karibu unayemuamini kuwa anaweza kukusikiliza.

4) Jizoeze kufanya mazoezi ya viungo, hata kwa kutembea kwa angalau dakika kumi na tano kila siku huku ukitembelea maeneo mbali mbali hasa yenye watu wa rika tofauti tofauti.

5) Jisomee vitabu vya dini na vingine vingi vya kuhusu mambo mbalimbali kimaisha na yatakayokufanya ufurahie maisha.

6) Hakikisha unapata mlo kamili, kwa sababu chakula ndio dawa muhimu na yenye nguvu zaidi

7) Jitengee muda mwingi wa kupumzika, kama unaona haupati usingizi unatakiwa ujiwekee muda wa kwenda kitandani huku ukitoa kila kitu ambacho kinaweza kukuharibia ratiba yako ya kulala, vitu kama TV, vitabu au simu.

8) Fikiria zaidi kuhusu majukumu na uwajibika katika maisha yako

9) Epuka kuwa mtu wa kukaa peke yako kwa muda mrefu. Jichanganye na watu mbalimbali. Kama ni muumini wa dini, pia shiriki katika sala na maombi, shiriki pia katika sala/ibada za pamoja

10) Jaribu kujifunza vitu vipya kama vile lugha mpya, kufanya vitu ambavyo ulikuwa haujawahi kuvifanya kama vile kushiriki michezo aina tofauti na uliyoizoea n.k.

Maelezo muhimu kwa mwathirika, ndugu, rafiki, jamaa na familia

Mosi:
Ugonjwa wa Sonona matibabu yake yanapatikana, muone daktari au mtaalamu wa Saikolojia (Clinical psychologist) au daktari wa afya ya magonjwa ya akili (Psychiatrist) au hata daktari wa kawaida.

Pili: Sonona siyo uchovu, uvivu wala uzembe; mgonjwa hapendi kuwa hivyo na hawezi tu kujisahaulisha au kujichangamsha! Na pia, sio kwamba anajifanyisha au analeta uzembe, bali ni sehemu ya ugonjwa (It is part of the pathological process)

Tatu: Ni muhimu kuhakikisha ugonjwa unatibiwa kwani ukikaa kwa muda mrefu dalili zinaweza kuzidi na kuwa mbaya zaidi na kumfanya mgonjwa hata asiongee kabisa, asile kabisa kwa siku kadhaa, awe anasikia sauti ambazo watu wengine hawazisikii, kuona vitu ambavyo watu wengine hawavioni; na hata kufanya jaribio la kujiua (suicide attempt) na wengine hufanikiwa kabisa kutimiza azma yao hiyo.

Nne: Sonona ina tabia ya kujirudia mara kwa mara, mtu mwenye historia ya kupata Sonona, anakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata tena hali hiyo hasa kama ataacha matibabu au hatafuata ushauri atakaopatiwa au kama hatakuwa na uangalizi wa kutosha (support) kutoka kwa watu wake wa karibu (wanaomzunguka).
 
Im not soo sure about the content,but certainly it is a good topic...ukiweza ku create awareness at community level more chances waathirika kupata msaada when in crisis.... asante mkuu..
 
Back
Top Bottom