Songwe: Waziri Kindamba apongezwe kwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza Tanzania kutambua Mifugo katika halmashauri zake zote

Mwanahabari wa Taifa

JF-Expert Member
May 27, 2020
1,450
799
IMG-20221027-WA0230.jpg

IMG-20221028-WA0120.jpg
Wasalaam JF,

Mkoa wa Songwe wenye halmshauri tano za Tunduma, Momba, Mbozi, Ileje na Songwe ndio Mkoa pekee nchini unaondesha zoezi la Utambuzi wa Mifugo kielekroniki katika halmashauri zake zote.

Wakati baadhi ya mikoa ikiwa haijaanza kabisa Utambuzi huu wa Mifugo, Mhe Waziri Kindamba Mkuu wa Mkoa wa Songwe na team yake tayari wanaendelea na zoezi hili katika halmashauri zake zote.

Mtakumbuka Rais Samia Suluhu Hassan tayari alikwisha ingia mkataba na nchi za falme za kiarabu kwaajili ya wao kununua nyama na Mifugo toka Tanzania.

Tarakimu zisizo Rasmi zinaitaja Tanzania kuwa ndio nchi ya pili baada ya Ethiopia kuwa na Mifugo mingi ambayo inasemekana kuwa ni Sawa na nusu ya idadi ya Watanzania.

Pamoja na Tanzania kuwa na Mifugo mingi Kama nchi hatujawahi kunufaika na faida zote zitokanazo na Mifugo kisawa Sawa ndio sababu Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan anakwenda kufanya mabadiliko makubwa kwenye sekta hii hasa baada ya Usajili huu.

Uzoefu wa bei za ngo'mbe kimataifa unaonesha huenda ngo'mbe anayeuza TZS 500,000 leo hapa Tanzania baada ya Usajili huenda akauzwa hadi Ughaibuni US$ 1,086 au TZS 2,500,000.

Kama ilivyo kawaida yake Rais Samia yeye anatengeneza fursa ili kutufungulia dunia tuchukue kile kinachotufaa na kustahili,Hili la Utambuzi wa Mifugo ni jambo jema liungwe mkono na kila mwenye ngombe, Mbuzi, kondoo na Panda.

Naye Masanja Jilala mfugaji toka kata ya Usongole Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe anasema "Sisi tunamshukuru Sana Rais kutuletea hili zoezi la kuweka hereni kwani Mifugo yetu tumekuwa tukinyonywa Sana kwenye bei Ila Kama tutauza nje ya nchi tunajua lazima bei iwe juu kidogo"

Hongera Waziri Kindamba na team yako, Hakika mnastahili pongezi.

Mwanahabari wa Taifa,
 
Hongera Sana kwa mkuu wetu wa mkoa wa Songwe, anafanya kazi nzuri Sana na ya kutukuka Tangia alipohamishiwa mkoani kwetu akitokea mkoani njombe, hata suala la usafi nalo amekuja kuhakikisha Songwe inakuwa Ni Safi muda wote na kila eneo linakuwa na hewa safi
Nasikia Jamaa ni mchapakazi Sana
 
Nasikia Jamaa ni mchapakazi Sana
Ni mchapa kazi Sana, Songwe tunasema Asante kwa mama Samia kutupatia huyu mkuu wa mkoa anayejuwa kazi iliyomfanya aletwe huku mkoani Songwe, hasa ukizingatia kuwa mkoa huu Ni mchanga tangia kuanzishwa kwake, Naiona Songwe ikipaa sana kimaendeleo, tunaomba mh Rais amuache hapa Hapa Kama mkuu wa mkoa.
 
Ni mchapa kazi Sana, Songwe tunasema Asante kwa mama Samia kutupatia huyu mkuu wa mkoa anayejuwa kazi iliyomfanya aletwe huku mkoani Songwe, hasa ukizingatia kuwa mkoa huu Ni mchanga tangia kuanzishwa kwake, Naiona Songwe ikipaa Sana kimaendeleo, Tunaomba mh Rais amuache hapa Hapa Kama mkuu wa mkoa
Mkuu hebu njoo inbox
 
Ni mchapa kazi Sana, Songwe tunasema Asante kwa mama Samia kutupatia huyu mkuu wa mkoa anayejuwa kazi iliyomfanya aletwe huku mkoani Songwe, hasa ukizingatia kuwa mkoa huu Ni mchanga tangia kuanzishwa kwake, Naiona Songwe ikipaa Sana kimaendeleo, Tunaomba mh Rais amuache hapa Hapa Kama mkuu wa mkoa
Kazi iendelee Songwe.Utambuzi ndio roho ya mfugaji kwa Sasa
 
Back
Top Bottom