Songwe: RC Mwangela amesema wakandarasi wanaosuasua kukamilisha miradi ya maji kwa wakati kukamilisha chini ya Jeshi la Polisi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,876
RC MWANGELA: WAKANDARASI KUKAMILISHA MIRADI YA MAJI CHINI YA POLISI

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Brg. Jen. Nicodemus Mwangela amesema wakandarasi wanaosuasua kukamilisha miradi ya maji kwa wakati kukamilisha chini ya Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Mkoa amesema hayo, 15 Mei 2020 alipofanya ziara na Kamati ya Usalama Mkoa ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na Mkandarasi Wilaya ya Songwe, Mradi wa Mkwajuni wenye thamani ya TZS Milioni 762, Galula TZS Milioni 679 na Totowe TZS Milioni 257 na kukuta haijakamilika wakati pesa zipo. "Wakandarasi hawa tutafanya kama tulivyofanya kwa Mkandarasi wa Iyula mpaka sasa maji yanatoka" Mhe. Nicodemus Mwangela.

Pia, Mkuu wa Mkoa amesema ifikapo 30 Juni 2020 miradi yote itakuwa inatoa maji.

Wakati huhuo amepongeza miradi inayotekelezwa kwa force akaunti chini ya RUWASA kuwa na ufanisi mzuri.

Wakandarasi ambao wanasuasua kukamilisha miradi ni COYESA mradi wa Totowe, Fajitech wa Galula na Febec wa Mkwajuni.
IMG-20200515-WA0042.jpg
IMG-20200515-WA0043.jpg
 
Aache usanii hamna miradi Ina urasimu Kama hiyo ya maji...

Huu Ni ujinga, polisi asimamie mkandarasi? Kwa Sheria gani na kwa taaluma ipi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom