SONGWE: Mwanamke afa maji alipokuwa akivuka mto huku amelewa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Wanamke mmoja (35) mkazi wa kijiji cha Iyula kata ya Msia wilayani Mbozi mkoani Songwe amekutwa amefariki dunia baada ya kuangukia katika mto mdogo wa Jodan uliopo katika mtaa wa Keselia kwenye Halmashauri ya mji wa Tunduma mkoani Songwe.

Richard Mwampashe ni kaka wa marehemu ambaye anasema dada yake alikuja kuhani msiba wa mtoto wake na kwamba kwa mara ya mwisho mwanamke ameaga kwenda ng'ambo ya kijiji jirani kwenye vilabu vya pombe ambapo hakuweza kurudi nyumbani baadae ikabainika alifia mtoni.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Songwe Mathius Nyange amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema marehemu alienda kulewa pombe ambazo zilimzidi kiasi cha kushindwa kuvuka daraja na kuteleza kisha kupoteza maisha ambapo mwili wake umehifadhiwa katika kituo cha afya Tunduma kwa uchunguzi zaidi.

Baadhi ya wananchi wamesema marehemu alikunywa pombe kupindukia na kushindwa kuvuka daraja hilo huku wakilalamikia muundombinu mbovu wa daraja ambapo tukio hilo limetokea na kuitaka serikali iufanyie marekebisho.ili kuepusha matukio ya aina hiyo.

Aidha kamanda Nyange ametoa wito kwa jamii kuepuka unywaji wa pombe uliokithiri kiasi cha kushindwa kujitambua.

Chanzo: ITV
 
Sijui mume wake alikuwa wapi, kumuachia mkewe anywe alewe chakari hadi kutojitambua na kurudi usiku?! Sijui kama huwa habakwagi njiani...
 
Huwa ninatafakari sana kwanini haya yote yatokee na kipindi hicho!
Kama wewe ni mfutatiliji wa mambo utagundua kila mara mauti huwakuta watu pale ambapo utakuta wameenda kwenye arobaini ya ndugu yao, matanga ya ndugu yao, au kishiriki kumbukumbu za vifo vilivyotokea vya mpendwa wao,,
Tuombe Mshana jr au mzizi mkavu atupatie tafri ya haya matukio kwa nini iwe hivyo?
 
Nchi za wenzetu marehemu angefanyiwa autopsy, kwahiyo ripoti ya dokta ndiyo ingekua inasomwa na huyo kamanda.

Siyo ramli na kusema wananchi walimuona akinywa pombe. Vipi kama njiani alikutana na mtu akambaka na kumuua kisha akamtupa majini ili wote tuulaumu mto na pombe alizokunywa?
 
Nchi za wenzetu marehemu angefanyiwa autopsy, kwahiyo ripotiya dokta ndiyo ingekua inasomwa na huyo kamanda.

Siyo ramli na kusema wananchi walimuona akinywa pombe. Vipi kama njiani alikutana na mtu akambaka na kumuua kisha akamtupa majini ili wote tuulaumu mto na pombe alizokunywa?
Umeonaee....
 
Back
Top Bottom