Songwe, Mbozi: Wakazi wa Ichenjezya Mama hawana barabara, Waiangukia Serikali iwasaidie

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,876
KITONGOJI CHA ICHENJEZYA MAMA WILAYANI MBOZI WAIANGUKIA SERIKALI HAWANA BARABARA,

Wakazi wa kata ya Hasanga kitongoji cha Ichenjezya mama wameiangukia serikali kuwasaidia kupata barabara ya kuwaunganisha na mji wa Vwawa wenye huduma nyingi za kijamii.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho Samali kamendu akieleza jinsi wanavyopata shida ya usafiri wa magari kitongojini mwao amesema hakuna barabara inawaunganisha na mji wa Vwawa na njia wanayopita ni juu ya bomba la Tazama ambapo ameeleza kuwa njia hiyo nayo imeharibika na huwezi kufanya ukarabati wowote kutoka na sheria za utunzaji wa bomba hilo.

"Kitongoji hiki huwezi kupita na gari kama mnavyoona barabara ni mbovu na tumelipeleka Tarura" alisema Mwenyekiti huyo

Ameendelea kueleza kuwa njia halisi ya wao kupita ni njia lilipo daraja ambayo hutokea barabara kuu ya Tunduma na endapo wakitengenezewa barabara itawasaidia wao kuingia mji wa Vwawa kiurahisi.

Mkazi wa Ichenjezya mama Maria Kayuni amesema wao kina mama wanapokuwa wajawazito inawapa shida sana nyakati za mvua na usiku kwani kupata usafiri kwao huwa ni shida na hata boda boda hugoma kuwabeba kutokana na miundo mbinu kutokuwa rafiki njia ni mbovu.

Nae Amani Msangawale mkazi wa kitongoji hicho amedai kuwa yeye hufanya shughuli zake Tunduma na mara nyingi hurudi usiku hivyo inamlazimu kupita poli la shule ya sekondari Vwawa ambapo ndipo wanapolalamikia kuwekewa barabara lakini wanapita kwa hofu kwa miguu na humlazimu kuliacha gari lake mjini kwani hakuna barabara ya kupita nalo kwa sasa ile ya Tazama imeharibika na kujaa tope.

Alipotafuta Meneja wa Tarura Wilaya ya Mbozi Naftar Chaula kwa njia ya simu amesema kuwa ni kweli kitongoji hicho miundo mbinu yake inahitaji kuondoa baadhi ya makazi ili kupitisha barabara na barabara yanayoizungumzia wananchi ya shule ya sekondari Vwawa ni barabara ya waenda kwa miguu ndio maana wamewawekea daraja na endapo itachongwa barabara usalama wa wanafunzi utakuwa ni mdogo sababu barabara itapita shuleni hapo hata hivyo Tarura wanaangali uwezekano wa kuwashauri wananchi waliopembezoni na bomba hilo kupisha ujenzi

IMG_20210202_130140_228.jpg
 
Sio Jimbo la silinde Hilo,Ni la hasunga
Nilitaka kushangaa, naona bwashee hataki kuamini kwamba jimbo ni la Mbunge anayetokana na Chama Tawala.

Bahati nzuri alikuwa Waziri wa Kilimo hadi 2020, kwahiyo alikuwa na connection zote za kuwajengea barabara kwani Waziri wa Tamisemi au Ujenzi alikuwa akikutana nao kwenye baraza la Mawaziri na Bungeni kila siku.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom