Uchaguzi 2020 Songwe: Dkt. Magufuli afanya kampeni Tunduma, afuta tozo ya mama kamandoo

Hapo Magufuli amefanya jambo la maana sana
Dada mshukuru Lissu aliye address ilo tatizo. Kama si yeye kulipigia kelele mzee baba angeagiza lini habari hiyo. Hiyo ndo faida moja wapo ya VYAMA VINGI. Marekani imeendelea kwa sabab ya mfumo huo. Umejionea debate ya juzi mzee Trump alivyokuwa anatolewa makamasi na Babu Biden. Tunachokitana ni maisha bora dada. Leo mitandao ya cm inavyoshindana inakuwa afueni kwa sisi watumiaji, maisha yangekuwaje kama Voda angekuwa peke yake. CCM imetikiswa ndo inajisalimisha kwa watu kwa nkia hizo.
 
Magufuli acha kutusimanga na maji..tutachimba visima na kupata maji maana hayo maji sio mali yako bali Mwenyezi Mungu alitoa kwa watu wotee..waovu na wema ili wayatumie. Unamkosea sana Mungu kwa maneno yako hayo..nenda katubu Magufuli.
 
Kama magufulu anakataa kupeleka maendeleo kisa mbunge ni mpinzani basi asipokee na kodi za wapinzani
 
Hapo Magufuli amefanya jambo la maana sana
Sana kwa kweli, sasa tusubiri kuona vifo vya akina mama na watoto vikiongezeka, kwa kuwa wanajiamulia, waende kliniki au la, hakuna ulazima wala umuhimu.
 
Nasubiria Lissu atoneshe kidonda cha mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Magufuli: mimi bado ni raisi na kuanzia leo wanafunzi wote hawatalipia mikopo yao.

kutekenywa ukatekenyeka
Atasema anawashangaa waliopanga asilimia 15
 
jee unafahamu ziara anazofanya ni za kiraia kama Mwenyekiti wa CCM, ila yeye mwenyewe anaweza kuamua ni wakati gani anakua alama ya SEVOREIGNTY ya Watanzania kipindi hichi cha kampeni.

bora ungeongea kiswahili kitupu.....hapo umeboronga kwa kiingereza cha kishenzi
 
Back
Top Bottom