faru john junior
JF-Expert Member
- Dec 26, 2016
- 1,596
- 1,717
Tatizo hapo ni kupigwa mawe. Lakini wangerudi salama kusingekuwa na shida japo walivuka mpka
Askari 7 wanamfukuza bodaboda mmoja, ila hawa ndugu sijui hata wanawaza nini
hicho kitabu kinamuongoza polisi jinsi ya kutekeleza majukumu yake Kwa ufadaha bila kuvunja sheriaSIFAHAMU,
Wamevamia malawi?Hao askari polisi hawakusoma PGO kabla ya kuvamia huko Malawi?
Eti waliona piki piki wakaikimbiza wakizani ina magendo.... ujinga mtupu yaani sijui wanakuwa trained vipi hawa jamaa. Hapo utakuta walikuwa wanakimbiza wapate rushwa.Septemba 15 askari Polisi wa Tanzania waliingia Malawi kinyume cha sheria wakimfukuza bodaboda waliyedhani amebeba biashara ya magendo ambapo walipoingia Malawi walipigwa mawe na wamalawi na kuokolewa na Polisi wa Malawi
Askari 7 wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ileje mkoani Songwe wamefukuzwa kazi kwa kosa la kuvuka mpaka na kuingia nchini Malawi wakiwa na mavazi ya kijeshi na silaha za moto kinyume na taratibu za kijeshi
Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe Janeth Magomi amethibitisha tukio hilo
Pia soma: Polisi wa Tanzania wanasa Malawi wakifuatilia wahalifu
21 SEPTEMBER 2021
ILEJE, SONGWE
TANZANIA
ASKARI WA POLISI WATANZANIA WALIOINGIA MALAWI WAFUTWA KAZI, PIA WALIKIMBIA NA KUTEKELEZA SILAHA ZAO
WALIKUWA KATIKA OPERESHENI AMBAYO HAIKUFUATA KANUNI ZA GPO
Askari 7 wa kituo cha Polisi cha Ileje bila kutoa taarifa kokote wala kibali cha IGP wa Tanzania waliingia katika nchi ya Malawi wilaya Chitipa wakidai kufukuzia magendo wakiwa na silaha 2 za SMG kila mmoja ikiwa na risasi 30 na gari moja la jeshi la Polisi la Tanzania.
Kufuatia kitendo hicho walikumbana na wananchi wa wenye hasira kali Malawi kupelekea askari polisi 4 kukamatwa pamoja na silaha mbili, risasi 60 na gari la polisi lenye usajili PT kushikiliwa nchini Malawi.
Askari hawa kwa kushindwa kufuata sheria ya utekelezaji kazi, kupata ruhusa, kutumwa / kupewa idhini halali toka ofisa wa Cheo cha juu kama zilizoainishwa na kanuni za GPO (general police orders), jeshi la Polisi kupitia mkuu wa Polisi mkoa wa Songwe amewafukuza kazi askari kwa kudhalilisha Jeshi la Polisi na pia kuifedhehesha nchi kwa vitendo vyao kufanya kazi bila kufuata GPO zinavyotaka.
Source : MATUKIO DAIMA TV
RPC anasema waliwashtaki hao Polisi kwa kufuata Kanuni zao zinazowaongoza Jeshi la Polisi yaani PGO.
Kesi ya kina RPC Kiangi na wenzake ni ngumu sana, kama hawakufuata Sheria zilizopo kwenye PGO na wao watakuja kushtakiwa na kufukuzwa kazi.
Uko sahihi.Lakin pia pongez kwa wananch wa malawi sio mazombi. Kitendo cha kuwatwanga hao vilaza walioingia kwako ni cha kizalendo na kujielewa..
Njoo sasa huku kwetu kwa mazombi, kule Tarime one time police wakenya walivuka mpaka kuwakamata boda boda waliokuwa wanavuka mpaka kwenda Kenyaa..
Mazombi ya tz yakawa yanasema tu mbona wamevuka mpaka..mbona wanawashika..alaf yamekaa tu kutazama..
Vichwa wa wabongo vimejaa simba na yanga tu..shwaini
Pgo ni(police general orders)PGO ndio nini wakuu?
Hata sheria hawajui. PGO pia hawaifatiAskari wetu wanapaswa kuboreshewa mafunzo. Wana matatizo mengi
Huu ni muongozo wa utendaji kazi(code of conduct) au ni maagizo ya mkubwa wako wa kazi?Pgo ni(police general orders)
Unapewa maagizo na mkubwa wako aliyekuzidi cheo ili ufate maagizo yake.