Songs Battle: Kamua (TMK) Vs Hii Leo (East Coast)

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
843
1,363
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 kulikuwa na makundi mengi ya bongo fleva yaliyokuwa yanafanya vizuri.

Miongoni mwa makundi hayo ,TMK wanaume na EASTCOST team yalikuwa juu,.Makundi haya yalikuwa yanaongozwa na juma nature na Crazy JK kwa pamoja.

Makundi haya yalikuwa na uhasama mkubwa xana, na hii ilidhirika katika mashairi ya nyimbo zao. Japo mi ni mtu mzima kidogo, lakini nilikuwa nafuatilia kwa karibu makundi hayo.

Leo nimejaribu kuziangalia nyimbo mbili ambazo ni za majibishano na zinazoonesha kuwa TMK na EASTCOST Walikuwa na upinzani mkali. Nyimbo hzo ni KAMUA to TMK Wanaume na HII LEO toka east cost team

Je katika nyimbo hzo JE? mnaona vipi, nikimaanisha nani/Nyimbo ilimzidi mwenzie katika vipengele vifuatazo

1.UKALI WA BEAT : Kati ya hzo nyimbo mbili ipi ilikuwa na beat kali?

2.UKALI WA MASHAIRI: Nyimbo ipi ilikuwa na mashairi makali?

3. KUMCHAMBA/KUSHINDA BATTLE: Ni nyimbo ipo iliweza kutoa maneno ya kejeli makali , na kushnda battle ya rap? Yani kama watu wanatoleana maneno yupi alimzidi mwingine

4. VIDEO KALI

5. UWAKILISHAJI WA NYIMBO JUKWAANI

Big up to bongofleva
 
Hiyo Kamua hata mistari yake nishaisahau hata video nimeisahau sahau..mara sijui KR anajaribu kuvaa kiatu cha mtoto..mara nature yupo kwenye mkokoteni..zilikua akili za cha ukucha hizo!

Hii leo ikipigwa club leo lazima watu waruke majoka..Beat kali, Video kali, MCs hodari. Kwanza verse ya Gk funga habari!

..wananiita bitozi kisa navaa ma Fubu afu na drive Bima...
 
watu wanarudi na watu wanakwenda dhamira ikizidi hata msuli utafungwa mkanda. haiitaji mjadala.aliedanda treni kwa mbele ndiye anaejua mjini shule
sio kwamba mi sipendi harufu ya kuku wa kienyeji bali pumzi nyingi naona muhimu wa kuhoji...daaahh Deo Corleone una mistari mkuu..salute
 
Last edited by a moderator:
Haitwi jk ni gk leo ndio kazi ya kiume najiuliza kama leo ndio ingekuwa inatoka pamoja na hii ya ney wa mitego cjui kama ingepigwa, mi nionavyo wanamuziki wa tz walianzia juu sana wanaokuja wote hawawezi kufika levol hizo
 
......Miongoni mwa makundi hayo ,TMK wanaume na EASTCOST team yalikuwa juu,.Makundi haya yalikuwa yanaongozwa na juma nature na Crazy JK kwa pamoja.......
JK = GK { King Crazy GK }
......... Nyimbo hzo ni KAMUA to TMK Wanaume na HII LEO toka east cost team..........
KAMUA - Ni wimbo wa GWM na Si TMK wanaume

Turudi kwenye mada -Tujikubushe kwa kuzisikiliza nyimbo zenyewe kwanza
KAMUA - GWM ( TMK )

HII LEO - Crazy GK ft A.Y & Mwana FA (East Coast)

My Take
HII LEO - niliipenda zaidi, Hebu sikiliza mistari ya Mwana FA
 
Last edited by a moderator:
Ungepambanisha NYUMBANI NI NYUMBANI Vs HII LEO ungeeleweka zaidi, KAMUA hao ni GWM. Ila hata hivyo still hii leo iko poa zaidi kwangu maana sichokagi kuisikiliza, tofauti na hizo za wanaume sikumbuki mara ya mwisho nimezisikiliza lini, kwenye HII LEO verse ya AY naikubaligi sana jamaa alivyodondoka mule, yule ndo AY nayemuelewa sio huyu wa sikuhizi
 
Back
Top Bottom