Songea: Mkurugenzi wa manispaa ya Songea na diwani wa kata ya mjini wamewekwa mfukoni na mfanyabiashara

D2050

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
1,902
1,067
Mkurugenzi wa wanispaa ya songea, diwani wa kata ya mjini, serikali yote ya mtaa wa mjini wamewekwa mfukoni na mfanyabiashara anaefahamika kwa jina la DUMA.

Viongozi hawa wote wanafaham fika taratibu za mipango miji ya manispaa ya songea nyumba zilizo katikati ya mji zinatakiwa kujengwa ghorofa.

Wamiliki wengi wa nyumba za katikati ya manispaa ya songea wanashindwa kuzikarabati nyumba zao kwasababu wananyimwa vibali vya ukarabati huo. Inapelekea nyumba hizo kuuzwa kwa bei nafuu kwa wafanyabiashara wenye pesa zao wakiwa naimani wao watajenga hizo ghorofa wanazozitaka serikali.

chakushangaza sasa kumekuwa na utowaji rushwa wapokeaji ni viongozi wa serikali inayojinadi inapinga rushwa. Nyumba iliyopo mtaa wa ccm kata ya mjini karibu na ofisi za ccm wiliya songea mwanzo wenye nyumba walitaka kuikarabati lakini walinyimwa kibali.

Wakaamuwa kuuza hiyo nyumba leo aliye nunua hii nyumba amepewa kibali cha ukarabati je kunanini hapa? inamaana vibali vinatolewa kwa wenye pesa tu? je nyumba zilizopo bado hazijakarabatiwa nao watapewa vibari kuanzia sasa?mkurugenzi wa manispaa na diwani mnapaswa kuchunguzwa na takukuru.
 
Mleta mada ana mawazo ya kimaskini alafu yeye anadhani ni ya "kijamaa"......Tafuta pesa wewe ili anawe umuweke mfukoni mwenyekiti wa mtaa!
 
Mleta mada ana mawazo ya kimaskini alafu yeye anadhani ni ya "kijamaa"......Tafuta pesa wewe ili anawe umuweke mfukoni mwenyekiti wa mtaa!
tatizo siyo pesa au umasikini sheria kama inakataza ukalabati wa nyumba basi iwe kwa watu wote wenye pesa na wasiyo na pesa
 
tatizo siyo pesa au umasikini sheria kama inakataza ukalabati wa nyumba basi iwe kwa watu wote wenye pesa na wasiyo na pesa
ndio maana nikakwambia tafute pesa ili nawe uhonge upate kibali cha kukarabati nyumba yenu
 
Kwann mliuza then uje jf kulalamika kwann ukuja jf tukupe ushauri mkakope mjenge ghorofa
tatizo siyo pesa au umasikini sheria kama inakataza ukalabati wa nyumba basi iwe kwa watu wote wenye pesa na wasiyo na pesa
 
Kwann mliuza then uje jf kulalamika kwann ukuja jf tukupe ushauri mkakope mjenge ghorofa
kinachoangaliwa hapa ni sheria zifuatwe sina kinyongo na anaekarabati nyumba yake aliyonunua kwa pesa yake,hapa nilichokileta kusiwe na matabaka katika kutekeleza sheria za mipango miji.huyu anaruhusiwa kuezeka na kuikarabati kwasababu anapesa za kuhonga.jana kuna mtu alikataliwa kwasababu hakuwa na pesa za kuhonga.
 
Hapo ni kuziona mamlaka za juu ukiwa na ushahidi unasidiwa maana kila bosi serikalini ana bosi wake ushindwi kusaidiwa

Mkurugenzi wa wanispaa ya songea,diwani wa kata ya mjini,serikali yote ya mtaa wa mjini wamewekwa mfukoni na mfanyabiashara anaefahamika kwa jina laDUMA. Viongozi hawa wote wanafaham fika taratibu za mipango miji ya manispaa ya songea nyumba zilizo katikati ya mji zinatakiwa kujengwa ghorofa.wamiliki wengi wa nyumba za katikati ya manispaa ya songea wanashindwa kuzikarabati nyumba zao kwasababu wananyimwa vibali vya ukarabati huo.inapelekea nyumba hizo kuuzwa kwa bei nafuu kwa wafanyabiashara wenye pesa zao wakiwa naimani wao watajenga hizo ghorofa wanazozitaka serikali.
chakushangaza sasa kumekuwa na utowaji rushwa wapokeaji ni viongozi wa serikali inayojinadi inapinga rushwa.nyumba iliyopo mtaa wa ccm kata ya mjini karibu na ofisi za ccm wiliya songea mwanzo wenye nyumba walitaka kuikarabati lakini walinyimwa kibali.wakaamuwa kuuza hiyo nyumba leo aliye nunua hii nyumba amepewa kibali cha ukarabati je kunanini hapa? inamaana vibali vinatolewa kwa wenye pesa tu? je nyumba zilizopo bado hazijakarabatiwa nao watapewa vibari kuanzia sasa?mkurugenzi wa manispaa na diwani mnapaswa kuchunguzwa na takukuru.

Umbea ni shida sana.... halaf zaidi ni mbaya ikiwa ni mtoto wa kiume....
 
Hapo ni kuziona mamlaka za juu ukiwa na ushahidi unasidiwa maana kila bosi serikalini ana bosi wake ushindwi kusaidiwa
wakubali tu nyumba zote zikalabatiwe ktk ya mji
 
Back
Top Bottom