Airfryer
JF-Expert Member
- Sep 17, 2021
- 430
- 1,032
Nimefika mkoa wa Ruvuma hapa mjini Songea baada ya miaka 18 tangu mwaka 2004, sioni mambo mapya kabisa wala ukuaji wa mji.
Hapa mjini naona majengo ni yale yale tu zaidi majengo kidogo sana yameongezeka kama pale opposite na Bank ya NMB zamani tulisema ni eneo la TANESCO. Kitu gani kinazuia majengo marefu hapa Songea mjini?
Huu mji kwa maendeleo ya vitu naona ni negative growth hasa infrastructure, zaidi ya miaka 18 niliyoondoka huku no changes!
Boda boda zipo nyingi sana hapa mjini tofauti na wakati huo nilipoondoka, sijajua watu wanatembea kwa umakini kiasi gani maana boda boda na watu ni kama idadi sawa au ngoma droo hapa mjini.
Soko la majengo kule zamani tuliita mitumbani hakuna mabadiliko makubwa sana zaidi ya bara bara za hapa na pale lakini wakati huo kulikuwa na lami yenye mashimo mashimo.
Mjini hakuna barabara za maana zaidi ya barabara itokayo bombambili mpaka Mbinga huko. Mji haujapanuka kabisa, Unatembea nusu saa tu umemaliza, hakuna sehemu za kuvutia na sehemu za mitoko zaidi ya bar.
Songea ukisema leo natoka ni kwenda bar, hakuna amsha amsha niliyoiona hapa Songea mjini.
Wazoefu wa miji, huu mji una tatizo gani?
Nilipita Njombe imebadilika sana sana tofauti na Njombe ile ya miaka 18 iliyopita. Hii ni Songea mjini lakini ni kama upo kwenye wilaya za ndani ndani huko za baadhi ya mikoa.
Soko la hapa Songea Mjini hata silielewi vizuri ni kasoko kadogo sana na kamejibana sana, kwanini wasiliamishe soko hilo?!
Kulikuwa na kampeni za kujenga masoko na stand wakati wa JPM, sijajua kwanini waliamua kuacha soko la mtindo huu.
Kuna stand mpya lakini haivutii kabisa kabisa zaidi ya kuweka lami, hakuna jengo kubwa la maana la abiria kwenye stand mpya.
Wamejenga stand mpya mbele ya msamala ukitokea mjini lakini bado wamefeli vibaya sana ni kama kituo cha daladala hivi.
Bar zipo zipo sana labda ndio sehemu ya starehe lakini hazina quality inayotakiwa kwa watu wala bata na matanuzi.
Mikoa hii ya kusini kuna tatizo kama hata stand mikoa walipata nao pesa za mgao wamejenga stand nzuri na za kisasa sana.
Kwa hiyo Songea hata ukapeleka mabilioni ya pesa za Serikali bado huu mji unalala usingizi tu, Kwa miaka 18 niliyotoka nimesikitika sana.
Jumatatu naelekea Lindi, nipo mapumzikoni hivyo natembea tembea kwenye hii mikoa nilianzia safari Dodoma.