Songea: Aliyekuwa mgombea Ubunge Joseph L. Fuime afukuzwa uanachama wa CHADEMA

kistwangara

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
656
94
Na sasa baada ya kujiridhisha pasipo shaka yeyote kwamba Joseph L. Fuime aliuza matokeo ya ushindi wake wa UBUNGE kupitia CHADEMA uchaguzi mkuu 2015 katika Jimbo la Songea Mjini sasa amefukuzwa UANACHAMA wa CHADEMA Rasmi. Na sasa anachokifanya kuhakikisha anavuruga chama wilaya ya Songea Mjini. Amewakusanya vijana na baadhi ya wafuasi wake kushinikiza arudishwe kwenye chama. Jambo ambalo siyo sahihi na hata haya mambo yanayorushwa na Bwana Andrea wa kata ya Mshangano kwa kujiita mwanahabari ni kujaribu kufcha ukweli huu.


JINZI ALIVYOUZA USHINDI KWA LEONIDAS GAMA WA CCM
Taarifa kwa wapenda maendeleo na wote wasiojua ukweli kuhusu yalitokea kuhusiana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa ubunge jimbo la songea mjini yaliyotangazwa siku ya jumatatu tarehe 26/10/2015.

Figisu za kushindwa uchaguzi au kuporwa ziliaza mapema sana kabla ya kutangazwa kwa matokeo ambapo lilijitokeza kundi kubwa sana la wanaccm wakiimba na kuashiria kwamba mgombea wao alikuwa ameshinda uchaguzi ule. Lakini baadae ilijulikana kwamba mgombea wa chadema alikuwa ameshinda uchaguzi ila kulikuwa na mbinu ya kuhakikisha anatangazwa aliyeshindwa Leonidas Gama.

KUHUSU MGOMBEA WA CHADEMA NDUGU JOSEPH L. FUIME
Hakika mgombea wa chadema alishinda uchaguzi ule ila aliuza ushindi kwa LEONIDAS GAMA ambaye ndiye mbunge wa Songea Mjini kwa sasa, na hii inajidhihirisha kutokana ushahidi wa kimazingira na tofauti ya takwimu za matokeo yaliyowasilishwa kwenye chama na timu ya kampeni ya Mgombea wa chadema ndugu Joseph L. Fuime.

USHAHIDI WA KIMAZINGIRA
" Kutokuwepo kwa mgombea wa chadema Bwana Joseph Fuime kwenye kituo cha majumuisho ya mwisho katika ofisi za manispaa, Kutokupatikana kupitia mawasiliano ya simu kwa namba zake zote siku ya majumuisho,
" kutokukabidhi kwenye chama nakala halisi za matokeo ya kila kituo cha kupigia kura katika jimbo alilogombea yaani fomu Na. 21B
" Kufungua kesi bila kushirikisha chama, na hatimaye kesi kufutwa.

KUTOKUWEPO KWENYE KITUO
Kitendo cha yeye kama mgombea kutokuepo kwenye kituo cha majumuisho na kumuacha wakala wake wa majumuisho ndugu JONAS KAWELELA aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kilichofutwa cha St. Joseph ilikuwa ni picha ya awali na wazi inayodhihirisha ufedhuli wake alioufanya kwa wapigakura wa jimbo la songea mjini.

Hata juhudi za kumtafuta ziligonga mwamba kwani kwa muda wote wa majumuisho licha ya yeye kutokuwepo pia simu zake za mkononi kwa namba zake zote hakupatikana mpaka ilipotimu saa 11 jioni ndipo alipatikana na kusema kwamba alikuwa nyumbani licha ya kwamba viongozi na RB walikuwa wakifika nyumbani na kuambiwa hayupo

KUTOKUKABIDHI NAKALA ZA MATOKEO
Hili nalo ni ushahidi wa kutosha kwamba aliuza ushindi, kwani baada ya uchaguzi kilifanyika kikao cha tathmini katika ofisi za chama wilaya ambapo kamati tendaji ya wilaya, timu ya kampeni na yeye mwenyewe Fuime alikuwepo katika kikao hicho. Ambapo wakala wake bwana Kawelela alithibitisha kwa chama pasipo shaka kwamba Fuime alishinda ubunge na wangepabambana hadi tone la mwisho kuhakikisha wanapata shindi kwa kwenda kufungua kesi mahakamani.

Naye Joseph Fuime hakukanusha jambo hilo, lakini baada ya maelezo ya wakala kwa viongozi waliwataka timu ya kampeni kukutana na secretariati ya chama wilaya wakiwa na nakala original za matokeo za kila kituo na kujumlisha kwa pamoja ili kujiridhisha kama kweli tulihinda ili chama kiweze kutoa taarifa kwenye ngazi za juu kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kisheria, kabla hata ya kufanyika hilo viongozi walishangazwa sana kukuta taarifa zimezagaa mitaani kwamba Fuime J. Amefugua kesi mahamama kuu!

Viongozi walipoona waliyoagiza hayakufanyiwa kazi waliamua kuwaita timu ya kampeni ambayo ilikuwa na viongozi watano kutoka kamati tendaji ya wilaya ya songea mjini na wengine toka chuo cha ST. Joseph Ruhuwiko ambao walitokana na uteuzi wa mgombea mwenyewe ili kukamilisha idadi ya watu kumi. Hawa hapa chini ni wajumbe waliotokana na chama:-

1. Rhoda Komba - m/kt wa BAWACHA wilaya
2. Seif A. Seif - m/kt Baraza la wazee wilaya
3. Milanzi - mjumbe wa kamati tendaji
4. Ajaba nditi - mjumbe wa kamati
5. Omary Hassan - alikuwa m/kt BAVICHA wilaya kabla ya kujiuzuru nafasi yake.
Nakuwaelekeza kwamba wanatakiwa kukabidhi nakala halisi za matokeo ili majumuisho yafanyike ili chama kiweze kijiridhisha na hata kutoa hali mbaya ambayo ilishajitokeza kwa wazi kwamba bwana Fuime ameuza.

Hilo halikufanyika kwani wajumbe wa timu walirudi na majibu mepesi kwamba nakala alikwa nazo mgombea na kila walipomfuata hawakumkuta, hadi pale katibu wa wilaya alipoandika barua kwa Bwana Fuime kumtaka kukabidhi nyaraka hizo kwenye chama haraka iwezekanavyo, Hata hivyo barua hiyo haikujibiwa. Hata hivyo chama kilimvumlia na kumtumia barua nyingine ya kukumbusha barua ya awali nayo haikujibiwa. Baada ya ukimya huo chama kiliingiwa na shaka kwamba pengime kulikuwa na mpango ovu dhidi ya hizo nakala na kwamba kwa nini hataki kukabidhi kwenye chama?

Kiliitishwa kikao cha dharura cha kamati tendaji ambapo wajumbe walikubaliana katibu kumwandikia barua ya kumtuhumu kwa mambo yafuatayo baada ya kuonyesha darau kwa viongozi wa chama na chama:-

1. Kwa nini hakuwepo kwenye kituo cha majumuisho pale ofisi za manispaa yalipokuwa yanafanyikia majumuhisho hayo licha ya sheria za uchaguzi kumtambua kama wakala namba moja?

2. Ni kwanini hakujibu barua za chama zilizoandikwa kwake licha ya kuzipokea kwa dispatch?

3. kwa nini hataki kukabidhi nakala za matokeo (Fomu Na. 21B) ya uchaguzi mkuu wa 2015 za kila kituo cha uchaguzi?

4. kwa nini alifungua kesi ya uchaguzi bila kutoa taarifa rasmi ya maandishi kwenye chama licha ya kushauriwa na chama kufanya hivyo kwenye kikao cha tarehe 27/10/2015?
Baada ya barua hiyo hakuna kilichofanyika ndipo chama kilipofikia hatua ya kumsimamisha uana chama wake hadi pale atakapojibu barua na kukabidhi nakala zake.
Baada ya hatua hizo aliandika barua na kwenda hadi makao makuu na kutaka kukata rufaa ambapo alipeleka barua yake hiyo makao makuu bila hata kunakilisha kwa ngazi ya wilaya, mkoa na kanda.

Baada ya barua hiyo tarehe 13/4/2016 kilifanyika kikao kwa agizo la katibu mkuu kwa uwakilishi wa Mkurugenzi wa organaizesheni na mafunzo wa CHADEMA ndugu Kigaila Benson kilichokutanisha kamati tendaji ya wilaya ya songea; bwana Fuime; na baraza la uongozi la mkoa.
Kikao kiliaza kwa kusomewa barua ambayo alipelekwa makao makuu ya chama bila viongozi kufahamu. Kila hoja ilijibiwa ingawa kimsingi haikuwa ya kukata rufaa bali ilikuwa ya majungu dhidi ya viongozi wake.

Aliulizwa na Kigaila kuhusu tuhuma alizopewa na chama wilaya kama ifuatavyo:-

1. Kuhusu kutokuwepo kwenye kituo cha majumuisho - alikiri kwamba ni kweli hakuwepo, alipoulizwa kwanini hakuwepo? - alijibu ni kwasababu alishajua matokeo ya kwamba ameshindwa baada ya kujumlisha matokeo ya vituo vyote kwa kushirikiana na timu yake ya kampeni usiku wa saa 7 wa kuamkia siku ya jumatatu tarehe 26/10/2015 hivyo hakuona umuhimu wa kuwepo kwenye kituo. ikiwa ni tofauti na maelezo yaliyotolewa na meneja kampeni wake kwenye kikao cha tarehe 27/10/2015 kwamba bwana Fuime alishinda ila ameporwa ushindi na wangetumia hadi tone la mwisho la damu yao katika kudai haki yake na siku hiyo hakukanusha ikiwa naye alikuwemo kwenye kikao.

Na alipoulizwa ikiwa aliutaarifu uongozi juu matokeo ya huo usiku? - alikiri hapana. ila alitegemea wale wajumbe wa kamati ya kampeni wangalisema kwenye chama, ili viongozi waweze kuwajulisha wanachama na pengine hata wasingeumizwa kwa kupigwa na mabomu kama ilivyotokea siku ya jumatatu ile. Alipoulizwa baada ya yeye na timu ya kampeni kujumlisha

walipata matokeo yapi? - alijibu ni yale yaliyotangazwa na mtangaza matokeo pale manispaa.
Aliulizwa hayo matokeo walijumlishia wapi? - alijibu walijumlishia nyumbani kwake, aliulizwa kwanini walijumlishia nyumbani kwake na siyo ofisini? - alijibu kwamba awali muongozo wa chama uliwataka kuandaa ngome ambapo shughuli zote za uchaguzi na kampeni zingefanyikia hapo, na kwamba ngome ilipatikana lakini hawakuweza kumudu gharama, hivyo aliamua kuweka ngome nyumbani kwake.

Aliulizwa Je alitoa taarifa kwenye chama kwamba ameamua kuweka ngome nyumbani kwake ili wamshauri? - alijibu hapana hakutoa taarifa kwa viongozi wa chama. Aliulizwa kwa nini? Alikaa kimya kuashiria hakuwa na majibu ya swali lile.

2. kuhusu kutojibu barua - alikiri kupokea barua zote ila hakutaka kuzijibu ila alitaka aitwe, jambo ambalo lilitafsiriwa ilikuwa ni dharau ya dhahiri kwa uongozi wake halali wa wilaya.

3. Kuhusu Kutokabidhi nakala - alikiri kwamba ni kweli ila alisema kwamba zilikuwa mahakamani zilipelekwa kama EXBIT. lakini ikumbukwe kesi ilifutwa kabla ya kuaza hatua ya kusikiliza na hayo yanathibitishwa na nakala ya ufunguaji wa kesi ya mahakama kuu ambayo haina mahali ambapo inaonesha kwamba nakala ziliwasilishwa mahakama kuu Pale mkoa wa Ruvuma.

4. Kuhusu kufungua kesi bila taarifa rasmi kwenye chama - alisema yeye alijua kwamba kwa namna iliongelewa kwenye kikao cha tarehe 27/10/2015 ilitosha na hakuwa na sababu ya kupeleka taarifa rasmi tena kwa maandishi kwenye chama. Alipoulizwa ikiwa ilikuwa muhimu kujulisha chama kuhusu kesi kwa barua? - alijibu haikuwa na umuhimu.
MAELEZO YAKE MENGINE BINAFSI (nyongeza)
Alisema kwamba watu wanamtuhumu kwamba amechukua hela mil. 300, na kwamba milion mia tatu (mil. 300) ni fedha nyingi sana watu wasiongee ongee hivyo. [hapa kuna walakini maana hakubisha kwamba hakuchukua ila alisema kwamba hiyo mil. 300 ni nyingi sana kumbe inawezekana alichukua lakini siyo kiasi hiko]
MAAZIMIO YA KIKAO YALIYOTOLEWA NA NDG. KIGAILA MKURUGENZI WA OGANAIZESHEN NA MAFUNZO TAIFA
Baada ya kikao kile maazimio yalikuwa ni kwamba bwana Fuime anatakiwa kujibu barua zote alizoandikiwa na chama; kukabidhi nakala za Fomu Na. 21B kwenye chama ndani ya siku 14, tangu tarehe ya kikao.

UTEKELEZAJI WA MAAZIO NA NDUGU JOSEPH L. FUIME
Baada ya kikao kile hakuna hatua za makusudi zilichuliwa na mhusika kwa siku 14 alizokuwa amepewa na ndg Kigaila bali alikabidhi photocopy za nakala na siyo nakala orijina Fomu Na. 21 kuptia kwa mzee Mwasote na Bwana Octavian tarehe 28/06/2016 ikiwa ni karibu miezi miwili.
Mara baada ya kupokelewa zile copy za nakala uongozi wa wilaya kupitia kwa secretariati yake walipitia nakala moja baada ya nyingine na kuzijumlisha ambapo majibu yake ilikuwa ni
" Waliopiga kura walikuwa 77,554
" Zilizoharibika 1,220
" Mgombea wa chadema 40,786
" Mgombea ACT-Wazalendo 436
" mgombea wa CCM --

ukichukua (77,554 - 40,786 =36,768 ); (36,768 - 436 = 36,332 ); (36,332 - 1,220 = 35,112); hii maana yake ni kwamba figure ya mwisho ya 35,112 ndizo kura alizopata mgombea wa CCM ambapo kwa jibu jepesi lisilohitaji kwenda shule ni kwamba Mgombea wa Ubunge wa CHADEMA JOSEPH L. FUIME alishinda uchaguzi ule ila aliuza.

Matokeo haya kupitia kwenye nakala yalitofautiana yale yaliyowasilishwa na timu ya mgombea ambayo yalikuwa ni yale yaliyotangzwa na msimamizi wa uchaguzi wa manispaa (mkurugenzi), ambapo hili timu ya kampeni ilikili katika repoti yao kwamba walilazimika kuchukua matokeo yale kwa kuwa mgombea alikatalia kutoa nakala, ila hili jambo hawakueleza kwenye ripoti na ndo maana walichukuliwa hatua kuhusika kuhujumu uchaguzi ule.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA UONGOZI DHIDI YAKE
Na sasa baada ya kujiridhisha pasipo shaka yeyote kwamba Joseph L. Fuime aliuza matokeo ya ushindi wake wa UBUNGE kupitia CHADEMA uchaguzi mkuu 2015 katika Jimbo la Songea Mjini sasa amefukuzwa UANACHAMA wa CHADEMA Rasmi. Na sasa anachokifanya kuhakikisha anavuruga chama wilaya ya Songea Mjini. Amewakusanya vijana na baadhi ya wafuasi wake kushinikiza arudishwe kwenye chama. Jambo ambalo siyo sahihi na hata haya mambo yanayorushwa na Bwana Andrea wa kata ya Mshangano kwa kujiita mwanahabari ni kujaribu kufcha ukweli huu.

Ushauri wetu sisi wapenda mabadiliko ni kwamba kuna kila sababu kuwaeleza akina Halifa, Rhoda, Mustafa, Haule, Zamaradi wajue wanafanya kazi ya Mtu na siku ukweli huu ukijulikana watakuwa wapoteza sifa kubwa sana kwa usaliti wanaoufanya dhidi ya wapigakura wa Songea Mjini ambao walimpigia kura nyingi sana Fuime akawauza.

Tumependa kuanika mambo haya ili wakubwa wajue maana kinachoonekana ni kama viongozi wanalaumiwa lakini ukweli ndo huo hatuwezi kuona chama kinavurugwa na mtu mmoja anayejiita ana wafuasi wengi huku akijua kwamba aliuuza matokeo ya uchaguzi ule.
^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^Mwanaharakati*******************************
 
KUHUSU MGOMBEA WA CHADEMA NDUGU JOSEPH L. FUIME
Hakika mgombea wa chadema alishinda uchaguzi ule ila aliuza ushindi kwa LEONIDAS GAMA ambaye ndiye mbunge wa Songea Mjini kwa sasa, na hii inajidhihirisha kutokana ushahidi wa kimazingira na tofauti ya takwimu za matokeo yaliyowasilishwa kwenye chama na timu ya kampeni ya Mgombea wa chadema ndugu Joseph L. Fuime.

USHAHIDI WA KIMAZINGIRA
" Kutokuwepo kwa mgombea wa chadema Bwana Joseph Fuime kwenye kituo cha majumuisho ya mwisho katika ofisi za manispaa, Kutokupatikana kupitia mawasiliano ya simu kwa namba zake zote siku ya majumuisho,
" kutokukabidhi kwenye chama nakala halisi za matokeo ya kila kituo cha kupigia kura katika jimbo alilogombea yaani fomu Na. 21B
" Kufungua kesi bila kushirikisha chama, na hatimaye kesi kufutwa.
mnashindwa halafu mnakuja na ngonjera za kijinga.....alilipwa shilingi ngapi ili kufidia mshahara,marupurupu na mafao ya ubunge ambayo atayakosa miaka mitano ya ubunge?.
 
Huu ndio uzuri wa chadema hakuna mkubwa kuliko chama ukileta upuuzi unapumzishwa ujitafakari.
Aaaa basi sawa ..cjui mkubwa atatoka lini au yye mfalme wa Morocco hadi afeee..
Acheni upumbavu,mnashindwa halafu mnakuja na ngonjera za kijinga.....alilipwa shilingi ngapi ili kufidia mshahara,marupurupu na mafao ya ubunge ambayo atayakosa miaka mitano ya ubunge?.
 
aende mahali pengine panapomfaa ,kuna vyama vingine vimeundwa na wasaliti wengi wa demokrasia,kwa ajili ya domokrasia na tumbo.aende huko atarandana nao
Hiyo ni kweli kabisa,nilishangaa sana Ccm kushinda pale songea mjini,watu walichoka kabisa na Nchimbi.
 
Wacha tuisome namba eeeeeeee nyinyiem mmbele kwa mmbeleeeee napita tu wadau.
 
In short run anaweza kuwa amepata vimilioni kadhaa vinavyoweza kumsaidia kujenga japo nyumba lakini visivyoweza kujenga makazi. Possibly ana familia na ailichokifanya mwaka 2015 huenda watakaokuwepo 2050 wakakikumbuka na kuweza kujua ni aibu kiasi gani itasababishwa na usaliti wake. Siasa za usaliti zinaishia kwenye usaliti!
 
Imeandikwa...atakuwa pale..Milele ?au the holy constitution has no act for king to step out.?
Hajawahi kulazimisha bali anachaguliwa, kwanini linawakera sana yeye kuwepo?! Hapa anazungumziwa huyu alieuza ushndi changia hili.
 
Back
Top Bottom