Labrujita
JF-Expert Member
- Jun 12, 2015
- 399
- 126
Uongozi wa harakati za mageuzi ya aina yoyote ile unahitaji busara, hekima, ujasiri, na kujitoa kwa hali na mali lengo likiwa ni kufikia kilele cha mageuzi lengwa pasipo kudhuru wafuasi na watu wengine ambao kimsingi wanakuwa wameamua kuunga mkono.
Ni ukweli ulio dhahiri kwamba tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini chama cha wananchi CUF, CHADEMA na NCCR Mageuzi vimekuwa mwiba mchungu kwa watawala kwa maana ya sera, mikakati na kukubalika kwake katika ardhi ya Tanzania.
Kwa muda mrefu sasa vyama hivi vyenye nguvu na ambavyo ni tishio kwa ustawi wa watawala vimekuwa vikihujumiwa kwa namna tofauti ikiwa ni mkakati wa aidha kuvidhoofisha au kuviua kabisa kama ambavyo iliwahi kujidhihirisha kwa baadhi ya vyama huko nyuma huku njia kuu ikiwa ni kununua viongozi wa juu na kupenyeza mapandikizi.
Binafsi nawaomba viongozi wa vyama vya upinzani na wakereketwa wengine wa mageuzi nchini kutokubali kuwa sehemu ya USALITI wa dira na dhamira ya dhati katika kufikia lengo. Niwatie moyo viongozi wote na hakika tuwakatae tena hadharani viongozi aina ya Profesa Lipumba ambaye alikimbia familia wakati wa shida na kuamua kurejea wakati ambao naweza kuuta wakati wa jaribio jingine baada ya lile la awali kutozaa matunda.
Kama viongozi watasimama na kutuongoza wafuasi na wananchi kwa ujumla katika kweli ni dhahiri tunahitaji akina Lipumba na Dr Slaa wasiopungua milioni 50 ili kuua nguvu hii ya mageuzi iliyomea mioyoni mwa watanzania tulio wengi.