Somo: Unapokuwa na simu zaidi ya moja zingatia hili kwa ustawi wa kampuni, taasisi au maisha binafsi.

Mp19

JF-Expert Member
May 3, 2019
259
715
Habari waungwana?
Napenda kushare nanyi hili jambo dogo ila lina impact kubwa katika ustawi wa taasisi, kampuni, shirika na hata maisha binafsi.
Simu moja inaita, unaipokea hujamaliza maongezi ya pili inaita utafanyeje ili usipoteze fursa zote.
Kwanza lazima ujue kuwa huduma unayoitoa wewe wapo wengine huitoa, hivyo watu huweza kukukimbia ndani ya dk moja tu usipokuwa makini.
Simu ndiyo itakayoweza kukushusha au kukuinua.
Fanya hivi; Ukipigiwa simu haraka pokea kwa unyenyekevu huku ukionyesha utayari, ongea na aliyekupigia na pindi simu hiyo hiyo ukipigiwa na mtu mwingine au simu B imeita usiache kupokea kwa kujisemea nina salio nitampigia hapo utakuta tenda (kazi) imeshakwenda kwa mwinhine.
Cha kufanya, mwombe yule unayeongea naye akusubiri kwa dk angalau mbili, moja au tatu kisha utampigia, hapo sasa pokea simu B kisha msalimie kwa sauti ya utayari halafu utapima urefu wa mada yake. Kama fupi ongea naye mumalizane kama ndefu kiasi naye mwombe dk kadhaa za kukusubiria.
Hapo sasa utatudi kwa simu A then utamaliza kwa simu B au C.
Hakuna mtu mwenye akili timamu akakubali kukupa dk 2 kisha akamtafuta mtu au kampuni nyingine ndani ya muda ulioomba ahudumiwe bali atasubiri.
Asante kwa kusoma ujumbe huu.
 
Inawahusu sana. Kwa ustawi wa taasisi zao.
Endapo inawahusu hebu fikilia hii hapa.
...
Unapo piga simu kwa mhudumu wa kampuni ya simu unakaa kwa muda takribani dakika kadhaa bila kupokelewa, baadaye anapokea na unapomueleza jambo lako,
....
Anakwambia hebu subili au piga simu baadaye nitakusaidia zaidi.
....
Niambie unapata picha gani hapo?
 
Endapo inawahusu hebu fikilia hii hapa.
...
Unapo piga simu kwa mhudumu wa kampuni ya simu unakaa kwa muda takribani dakika kadhaa bila kupokelewa, baadaye anapokea na unapomueleza jambo lako,
....
Anakwambia hebu subili au piga simu baadaye nitakusaidia zaidi.
....
Niambie unapata picha gani hapo?
Hii wale wa kampuni za simu haiwahusu kulingana na wingi wa wanaowahudumia, maana akikuweka pending lazima ile kwako hawezi kukukumbuka tena.
Hii customer care wa kampuni na taasisi ndio inawahusu zaidi
 
Back
Top Bottom