Somo muhimu la maisha kupitia Makada watatu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,704
Sehemu ya pili muhimu imeshapita. Maamuzi yaliyotolewa na kamati kuu. Sakata lilianzia pale mazungumzo binafsi yaliyovujishwa. Zikafuatia tuhuma. Kishapo barua za kulalamika na hatimaye kuitwa kwenye kamati ya maadili.

Mpaka hapo walikuwa pamoja. Walikuwa wamoja, lakini wakaanza kuachana siku ya tukio. Huyu mmoja akatii na kuwahi. Hawa wawili wakawa wanasuasua. Pengine kuna mmoja alikuwa anambembeleza mwingine. Itajulikana tu

Watoa maamuzi kidogo wakajiongeza. Wakaona tukiwaacha hawa wakawa wamoja watatusumbua sana. Sasa tufanyeje!? TUWATAWANYE. Waache waingie mlango mmoja lakini tuwafanye kila mmoja atoke na mlango wake. KWISHA HABARI YAO!

Mmoja akaomba msamaha kwa maandishi. Mmoja akapewa KARIPIO kali. Mmoja akatimuliwa.

Chungu hakiinjikwi na figa moja ama mawili, ni matatu.

Moja, ni binafsi haina majuto. Haina shirika. Mbili, ina ukinzani. Inaweza kuleta lawama na moja.

Tatu, ni wingi. Ni kikowa. Maamuzi si thabiti tena na majuto huwa mengi.

Wametawanywa. Wakatawanyika. Sasa kila mtu na lwake. Tunaambiwa kwenye misahafu: Siku ya mwisho watakutwa wawili kondeni. Mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.

Maamuzi na aina za adhabu, vimewatengenisha, vimewanyamazisha na pengine vimewafarakanisha!

SOMO MUHIMU LA MAISHA
Katika maisha kuwa wewe. Usimtegemee mtu, usitegemee maamuzi ya wengine. Kuwa na maamuzi binafsi kwakuwa haya pekee ndio utakayoweza kuyatetea na kuyasimamia. Usiwe bendera fuata upepo.

Usiyumbishwe. Usikubali wengine waamue badala yako. Usishawishike na kushawishiwa.

Kwanza kuwa na misimamo binafsi kabla hujakubali maamuzi na misimamo ya kikoa.

Hili litakusaidia sana shida itakapotokea mbeleni. Hapo ndio utakapoona rangi halisi za watu. Ila kama ulishafanya maamuzi binafsi hutaumia wala kuteseka sana.

Jambo la kikoa linapofanikiwa na kutimia kamwe hatuwezi kuwaza upande wa pili.

Lakini jambo hilo linapogeuka kuwa batili na mambo kuharibika. USALITI huanzia hapo.

Si kila mtu ana kifua kama ulichonacho wewe. Si kila mtu ana uwezo wa kuhimili pressure kama ulivyo wewe.

Si kila mtu ana uwezo wa kusimania maamuzi kama ulivyo wewe. Wengine wakitikiswa kidogo tu wanafunguka. Wengine wakifinywa kidogo tu hawabakishi kitu

Kuwa wewe! Baki wewe! Kama hujanielewa mrejee yule aliyesema:

I HAVE FAMILY TO FEED NOT A PUBLIC TO IMPRESS.

MSALITI...
USALITI...

Jr™️
 
Hayo uliyoyaongea yanafahamika mzee baba, ni kanuni.

Jambo lolote la hila ama uhalifu ukifanywa na watu zaidi ya mmoja, matokeo yake huwa ni mgawanyiko na ubatili, mambo yanapobumburuka kila mmoja hutetea nafsi yake.
Kuna msemo wanatumiaga majambazi...'heri nikukane ama nikusaliti ufungwe wewe, mimi nitakuletea sabuni jela, kuliko tukifungwa wote tutakosa msaada'....
Ndiyo yaliyotokea kwa wakongwe hawa!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
Ngoja vumbi litulie kuanzia kesho tutaona sinema nyingi mpya

Jr
IMG_20200301_125635.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanga haijawahi zalisha watu jasiri kiuongozi. Ukiwa pamoja na mswahili tegemea usaliti wa chini kwa chini. Mzee kalinda matumbo ya familia yake.
Hahahaha! Mzee kaangalia future ya makamba junior katika siasa za Tanzania,kaona atamuharibia kijana wake.akaona isiwe tabu kuomba radhi kwa walioshika mpini na maamuzi ya nani awe nani katika uongozi wa taifa hili.
 
Back
Top Bottom